Saturday, 19 April 2014

One Minute Woman! Msaada.

Pole na majukumu ya kutuelimisha
asante kwa ushauri wako ulionipa nitaufanyia kazi.

Napata wakati mgumu sana tuwapo kwenye 6x6 kwani nawahi sana kufika Kileleni, Yaani within 1min tayari nakuwa nimefika na nikishafika nakosa hamu kabisa ya kuendelea.


Hata mpenzi akiniandaa upya nashindwa na sijisikii raha yoyote hata akiendelea. Hamu huja tena mpaka nilale na kupitiwa usingizi nikiamka ndio naweza kunyegeka tena.

Hata ikitokea nikachelewa kufika haizidi dakika 5. Hali hii inaninyima raha sana sana kwani sipati raha ya kushiriki mapenzi kwa muda mrefu.


Mpenzi wangu anateseka sana mara nyingi humuacha akiwa hajafika hufikia hatua hulia.

Nahofu ipo siku atachoka na hii hali na kutafuta mtu mwingine kwa sababu amevumilia hii hali kwa miaka mingi, pia najihisi na kuona aibu napokuwa nae kwani tunaishi mbali mbali kukutana ni mara chache mfano kila baada ya miezi 3 lakini bado simridhishi.

Nakuwa na hamu sana sana ya kufanya mapenzi ila tukianza tu nafika.

NISAIDIE.

************

Dinah anasema: Ahsante na shukurani kwa Ushirikiano.


Umenifanya nicheke! Asa nani analia, wewe au yeye? Hihihihi nani ataka kupunjwa bwana....

Wewe ni mmoja kati ya wale wanawake wachache wenye bahati ya kufika haraka kwa sababu kwa kawaida Mwanamke huchelewa angalau kwa Dakika 10....(One minute Woman ni bahati ila kwa mwanaume hata 3 ni noma)!!


Kuna uwezekano pia "ukame" ndio unakufanya ufike haraka kwa sababu unashindwa kujizuia.

Ila kuu hapa naliona ni ukosefu wa Mawasiliano, mnatakiwa kuzungumza kwa uwazi na wote kwa pamoja mshirikiane.

Hiyo hali sio tatizo ni wewe tu kuifunza Akili/Mwili wako namna ya kujizuia mpaka mfike wote kwa pamoja...then mlale, mkiamka muanze tena na kila kitu kitakuwa byee(sio bai ni biyeee).


Tangu mnaishi mbalimbali ni vema kama ukawa unafanya zoezi kwa "unajisaidia" na wakati unakaribia unajizuia mara mbili-tatu alafu unaachia.

Inategemea na "kujisaidia" kwako muhimu ni kuacha kabisa kila unapokaribia kisha kuanza tena...zoezi hili litakusaidia kujua namna ya kujizuia hali itakayokusaidia wakati unapokutana na mpenzi wako. Hilo Mosi.


Pili, Sio kosa wala Dhambi "kujisaidia" angalau mara moja kwa Mwezi ili kupunguza "manyenyere" na siku ikifika ya kukutana na mpenzi wako huenda ukaenda mwendo wa Dakika 10-15 kabla hujafika.


Tatu, ni kuboresha Mawasiliano yenu, zungumza na mwenzio na umuelezee namna unajisikia (kama ulivyoniambia mimi hapa) kwa pamoja mkishirikiana itawasaidia.


Inawezekana Jamaa anajua kucheza na kiungo chake ndio maana unafika haraka, sasa ukizungumza nae huenda akajifunza "alama za nyakati" na hivyo kupunguza ufundi au kuacha ili umsubiri na hivyo kufika pamoja.


Vilevile isijekuwa yeye anajizuia ili ufike kwanza ndio amalizie lakini kwa bahati mbaya unashindwa kumpa ushirikiano mpaka mwisho.


Again! Mawasiliano ni muhimu, (ongea nae) kati yetu yatasaidia yeye kutojizuia kivile mara anapoona "alama za nyakati" na hivyo ukianza kupanda Mlima na yeye anapanda nawewe na ukifika Kileleni nae anaachia....happy days!!


Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

Friday, 18 April 2014

Anachepuka, je ni sahihi kutumia Condom?

Habari dada Dinah.
Natumai umzima wa afya na unaendelea kuendesha gurudumu la taifa.

Nimekua mfatialiaji mzuri wa blog yako na nimejifunza mengi hivyo na mimi leo nikaona si haba nikiomba ushauri kutoka kwako na kwa wasomaji wengine.


Mimi ni mke na mama wa watoto 2. Umri wangu ni miaka 31 na niko kwenye ndoa kwa miaka 3! Naomba kufahamu kama ni sahihi kumwambia mume atumie kinga endapo atahitaji au nitahitaji kufanya nae tendo la ndoa.


Na hii ni kwasababu unaona dalili za kuwa mume wangu ameanza kuchepuka. Sababu zilizopelekea kuhisi hivyo ni kuwa mume analala mzungu wa nne!

Hataki kabisa niguse simu yake na hata nikibahatika akiwa kalala sikuti chochote kwenye inbox wala call history zaidi ya zinazonihusu mimi!


Pia kuna siku amerudi na alama kwenye bega wazungu wanasema 'love bite' huwa anakawaida ya kukaa na vest akiwa home lakin hii wiki alikua anavaa tshirt had wakat wa kulala.

Na akirudi anakua na uso wa mbuzi yaani ameshajihami. Nikimsubiri chumbani nimuulize anakua ana panic na kuishia kususa!

Kwa kifupi mawasiliano yetu ni hafifu sana. Nimegundua ni mtu anayependa 'ndio bwana' kwa kila kitu hii inakua ni ngumu kwa upande wangu kwa sababu maisha ya kihalisia hayapo hivo.

Naomba ushauri tafadhali.


*************

Dinah anasema: Ni njema, Ahsante. Shukurani kwa ushirikiano.


Mwanamke! Umepata zaidi ya ushahidi kuwa Mumeo sio mwaminifu, huna haja ya kumuuliza bali ni kumuwahi kwa Talaka.....Kimbiaaaa (Well mimi ndio ningefanya hivyo)


Haya mdada, ni kitu gani hasa kinakufanya uendelee kukaa na huyo mwanaume kama Mumeo? Usiniambie watoto....!!


Achana na mambo ya "nikitaka ngono"....yeye akitaka Ngono mtolee nje ikiwezekana ita Polisi.


Alafu unawezaje ku-even fikiria kufanya mapenzi na mumeo wakati unajua kwa uhakika analala na mwanamke mwingine? Huoni kinyaa?!!


Ni sahihi kutumia Condom na mumeo ikiwa unahisi anatereza nje ya ndoa yenu mpaka atakapopimwa na kupewa all clear!!


Kama Ngono ni muhimu sana kwako mpaka unataka kuendelea kulala na a cheater basi ni vema mtengane ili uwe huru ku-date mtu mwingine(na kutumia Condom) kuliko kuhatarisha maisha yako na huyo Mumeo asiejali hisia za mkewe na watoto wake.


Tuone wengine watashauri vipi, mimi nakushauri ukimbie....


Kila la kheri!
Mapendo tele kwako...

Thursday, 17 April 2014

Tarehe za kuzuia Mimba

Dinah! Mambo? I hope mzima wa afya, unaendelea na majukumu ya hapa na pale.


Mimi mmoja wa fans wako katika blog yako. Samahani, na swali moja nahitaji kufahamu. Nilikutana na mpenzi wangu kimwili na siku hiyo nakutana nae kama tarehe 15.


Yeye alikuwa anaingia Hedhi tarehe 24, na hatukutumia kinga. Then kuna siku nilikuwa napitia blogs nikakutana na kitu kuhusu mwanamke anaweza kutambua siku zake na kujikinga na Mimba.

Ilikuw hivi; kabla ya mwanamke hajaingia hedhi kuna siku 8 za hatari kabla ya tarehe yake ya kuiona hedhi, na kuna siku 8 baada ya hedhi ni za hatari.

Basi nilivyo soma hivyo nikamtext na akanielewa kuwa ni kwel ikabidi tusubiri tuone kama ataingia hedhi tena coz alikuwa anaelekea kuingia tena.

Ilipofika tarehe 24 hakuiona hedhi kwamba atakuwa amepata ujauzito, nilimwambia akapime na jibu aliloniletea aliniambia kuwa ni mjamzito.

Sorry Dinah kuna ukweli wowote juu ya hili? Au ananidanganya coz siko nae karibu.

Thanks.


**************

Dinah anasema: Namshukuru Mungu, ahsante kwa ushirikiano.

Asa wewe sijui nikucheke au nikutukane? Hakika atakuwa na Mimba.....unafanya bila kinga then unaenda kusoma maelezo kwenye blog kisha unajipa Moyo kuwa hatoshika mimba! Who does that?!!....Only Dumbs...KINGA 1st mengine yanafuata dogo!


Huyo alieandika siku 8 kabla na siku 8 baada ya Hedhi bila shaka atakuwa Mwanaume.....ndio hao hao wanaodai kilele kwa mwanamke ni kama kutaka kukojoa mkojo wa kawaida!!!

Ndio, ni kweli kuna siku kwenye mzunguuko wa hedhi ambazo ni Salama (Humimbiki) na Hatari (Unamimbika) lakini tarehe hizi hutoa matokeo yenye uhakika kama Mzunguuko wa mhusika ni wa siku 28 kwamba haubadiliki.

Mzunguuko wa Hedhi wa kawaida wa siku 28 ndio pekee (nadhani) unaaminika(kwasababu ni rahisi kukumbuka).

Siku ya kwanza ya Hedhi ndio siku ya kwanza ya Mzunguuko na Yai hupevuka siku ya 14 tangu Hedhi kuanza.Siku ya kushika Mimba(Hatari) ni siku ya 10, 11, 12, 13, 14, 15 na 16 tangu Hedhi kuanza(sio tarehe kwani hubadilika).....siku Salama na zenye uhakika ni Siku ya kwanza ya Hedhi mpaka ya siku ya 7 ambapo kwa baadhi ya wanawake bado yuwa Hedhini....Siku zilizobaki sio Salama kivile.


Sitopiga mahesabu hapa (sina maelezo ya kutosha kuhusu mzunguuko wa huyo Binti) ila nitakupa maelezo ambayo yatasaidia ili wewe mwenyewe ufanye mahesabu.


Mwanamke anapoamua kutumia tarehe kama Kinga ya Mimba anatakiwa kufuatilia kwa karibu "mahesabu" ya tarehe zake angalau kwa miezi 3 kabla ya kuanza kungonoka bila Kinga.


Kutokana na uzoefu wangu siku kabla ya Hedhi huwa ni hatari kwasababu hakuna anaejua Manii husika zitakuwa hai ndani ya mwanamke kwa muda gani.

Inategemea na afya Manii hubaki hai kuanzia siku 3-7 hivyo unaweza ukapata Hedhi na ile umemaliza tu Mimba ikaingia.....


.....sidhani kama Hedhi inasafisha Manii na pia inategemea Upevukaji wa Yai linalofuata(sometimes hupevuka mapema).

Pole kwa kushtukiziwa Mimba, next time weka tumia Condom kama hutaki mtoto....

Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...