...Unafanyaje kama tayari umekosea? Wacha haraka tutafika hapo tukimaliza tangulizo...hujambo lakini? Mie, nipo hapa najongea kuwa Mama wa miaka 50 with a toddler. Natamani ningekuwa Twita oh X nikusamulie namna maisha yalivyo in my Forties. anyways, achana na hili.
Nadhani kilamtu anajua namna ya kuchagua mpenzi, mara nyingi sie wa enzi za kati(1900 we did not choose our spouses, we fell in love and do the right thing, you wa leo(2000s) choose just like in the 1800s mnatazama Pesa, afya na jinsi mnavyo kuwa treated on 1st date then do. Mimi sidhani kama tuli-date, we just fell and do(as in start relationship) and learn as we went. Hawa watoto wanafanya vema sana japo baadhi ya watu(the older ones) don't get them, these kids dont want to go through what their parent did, struggle love. Wanataka something different which I support.
Umewahi kuhisi kama vile umekosea kuchagua familia, kwamba unaomba wakwe zako na ukoo mzima wangekuwa wachache labda, wajitegemee zaidi kiakili, kimaamuzi na kiuchumi. Umeshuhudia Mumeo/mkeo anasomesha na kuhudumia watoto wa dada zake, kaka zake, binamu zake na wajukuu zake....ukajisemea khee, ningefanya uchunguzi ningeepuka adha hii.
Mara kwa mara unaona Mmeo anakosa amani, furaha na you know for a fact sababu sio wewe wala Kazi wala Watoto, kwasababu hakuna kitu umefanya/kimetokea kinachoweza kumfanya awe down kiasi hicho. Kwasababu ni mwenza wako na unampenda ni jukumu lako to find out what is going own so that you support him but hawezi kukuambia because ni issue ya ndugu zake, haikuhusu. Bila kujua hali aliyonayo sio tu inakuathiri wewe kama mkewe bali pia watoto. Kama ni mkeo, kwa kawaida sisi huwa wepesi ku-share hata kama tunajua hayakuhusu, tutaongea/lalamika kushusha mzigo....men hawapo hivyo.
Umewahi kushuhudia wake wenzio(mmeolewa familia moja) wanavyosemwa vibaya na kusingiziwa kuwa wamem-badilisha kaka/mdogo wao? Kwamba shemeji zako ambao ni kaka zao wamebadilishwa na wifi zao(na wewe ni wifi pia ila ni mpya?) Kimbia...well too late now.
Zifuatazo ni familia unatakiwa kuziepuka linapokuja suala la kufunga ndoa na ndugu yao;
1-Wapenda Drama, iwe kwenye misiba, sherehe, maradhi au uzazi.
2-Mama na Baba yao hawakufunga Ndoa mpaka watoto(bwana ako na ndugu zake) wamekua na Mama yao kuanza kuwalilia kuwa hakuolewa kwa sherehe hivyo mfanyieni sherehe nyie.
3-Washirikina, wana Imani ya Dini kupilitiliza, wanachukiana(wanaoneana wivu) na wapenda Mikutano, kila jambo lazima kuwe na kikao na jambo hilo liwe la Ukoo.
4-Karibu kila mmoja wao wa kiume alizaa nje ili kupata mtoto wa kiume au wanawake wanatoka na waume za watu au/na walizaa kabla ya Ndoa(na hawajaolewa).
5-Ambao hawajaondoa mavumbi(wengi wao ni wa la saba la Mkoloni, Nyerere, Mwinyi na Mkapa).
6-Wale wanao amini Mali au mafanikio ya ndugu kuwa ni Mali/mafanikio yao pia na vizazi.
7-Ile familia bwana'ko ndio mwanaume pekee halafu wa ni kwanza au mwisho kuzaliwa.
8-Wasujudu mwanafamilia mmoja sababu tu anapesa kuwazidi wengine.
9-Mpenzi kasomeshwa kama "uwekezaji" kwamba afanye ajualo ili kurudisha faida.
10-Mama/Baba anakupa kipaumbele wakati kuna wakwe zake wengine kabla yako.
11-Hawataki ndugu yao afunge ndoa na wewe.
12-Wana maradhi ya kurithi(Ukichaa/Akili, Kisukari, Moyo, Maini, Ukoma, Sikoseli n.k.)
Enzi 1800s mtu akija kuchumbia kwenu, anapewa muda wa kusubiri jibu. Wazazi na ndugu wa karibu wanaanza shughuli ya kutafuta historia ya Familia/Ukoo wa jamaa ili kujua kama kuna hizo hekaheka 12 nilizozitaja na pengine zaidi. Once they find one "fault" which can't be justified out of 12 wanagoma kuoza binti yao kwenu, labda kama wewe ni Tajiri(wanakutoa Mhanga)😁.
Sasa kama tayari umevaba na umo ndoani mwaka wa 7 huu, unafanyaje?
Njoo baadae wiki ijayo,
Bbai.
Comments