Tongoza Mkeo....

 


Ni kawaida kwako Mume (na jamii kwa ujumla) kutegemea mkeo afanye kila awezalo kuifanya ndoa kusimama utasema kajioa mwenyewe. Kuna siku nikaamua kugugo matatizo ya Ndoani, kila maelezo niliyoyapata kwa Kiswahili na Kiingereza, mzigo wa kuweka mambo sawa wenye Muungano huo alibebeshwa mke.

 

Hakukua na maelezo ya kutosha ambayo yanamsaidia Mume kutatatua matatizo ya ndoa zaidi ya nini afanye akishindwa kusimamisha, Mke na Mama nani nimpende? au nini cha kufanya ikiwa anamaliza haraka? Vipi kuhusu nini cha kufanya ikiwa umemuudhi mkeo? Nini mbadala wa kumnunia/fokea/ignore mke wangu, kitu gani nifanye kukabiliana na mzunguuko wa hedhi wa mke wangu baada ya kupevusha pale anapokaribia Siku zake(sio za kufa bali Hedhi) n.k.? Kuna mengi kwenye ndoa zaidi ya Ego, Mama yako na Uume wako.

 

 Kwenye blog hii tutakumbushana mengi tu ambayo hayahitaji uekisipati wa jinsia bali ni uelewa wa kawaida tu wa kusomana kwa pande zote mbili. Nakumbuka enzi nilipokuwa Twitter kuna wakaka wawili nawaheshimu sana, walikuwa wanazungumzia kuhusu “kuna umri ukifikia mambo kadhaa kwenye ndoa yanakuwa hayana uzito tena, unakuwa unazingatia zaidi  uhakika wa kipato, afya njema na furaha ya familia”, wasingegusia ndoa ningekubaliana nao kuwa kweli baadhi ya marafiki wapenda starehe wanakuwa hawana uzito(unawakwepa), kukaa Baa(au online) baada ya Kazi kila siku kunapoteza thamani(unakunywa ukiwa home(unacheza na wanao).

 

Basi mie na umbeya wangu nikarukia “Convo” nikawauliza inamaana siku hizi hamtongozi wake zenu humo ndoani? Wakachekaa, wakasema huo muda hawana….nikashangaa  hihihihi. Nikawauliza hamuhofii wake zenu kutongozwa huko nje? Kama msemo unavyokwenda, usipompatia nyumbani/ndani, wenzako watakusaidia huko nje.

 

Huenda mkeo hakuambii, ila napenda ujue Kaka yangu mpendwa, Mkeo anahitaji kutongozwa mara kadhaa kwa Mwaka, sio kila siku ila once in a while hasa akiwa kwenye mood mbaya(anakaribia Hedhi)…usimtongoze kama vile ulivyoanzanga miaka 15 iliyopita, mtongoze kulingana na alivyo sasa.

 

Mfuate-fuate(siku hizi ndio mnaita ku-stoku? Unamstokuje mkeo), msumbue kwa kuonyesha mapenzi iwe kwa vitendo au kwa maneno, pia unaweza kumtongoza wakati unamuandaa na wakati tendo linaendelea. Nyumbani(Asili yetu) kuna msemo “ikiwa mumeo hakufuati-fuati kwa maneno kutaka tendo basi ujue kuna tatizo”!

 

Ni muhimu sana kwa mkeo kuona kuwa bado unampenda na kumtamani kama ilivyokuwa awali pamoja na mabadiliko yote aliyopitia kwa sababu yako na kwa ajili yako…you know, Kubeba mimba na kukupa Watoto. Kurudi nyumbani kwa wakati kila siku au kusema “ahsante mke wangu kwa chakula” sometimes haitoshi(sio kila mwanamke anahisi kutakwa sexually kwa kupewa shukrani au kushikwa tako, wengine wanapenda kushawishiwa/tongozwa.

 

Je unaujua Mzunguuko wa Mkeo wa Hedhi na unakabiliana nao vipi mwanzo mpaka mwishoni? Au na wewe unaamua kukaa Kazini/Bar mpaka usiku wa manane halafu unakutana nae mlangoni na Panga? (Natania).

 

 Huo mzunguuko ndio sababu kuu Wanawake na Uongozi is a Scam, we cannot make Big maamuzi bila kuweka Mahisia mbele, kama sio hasira bin visirani au furaha kupitiliza basi  huruma kupitiliza. Wanaume homono zake zipo vilevile, hazibadiliki mara 4 kwa Mwezi kama sisi. Nimetoka kwenye topic, sorry.

 

Takuona wiki ijayo.

Bbai. 

Comments