Je tangu umefunga Ndoa, ume-improve...

...Mchezo au upo vile vile? Kwamba ya nini ni-showcase  au ujiboreshe wakati  umeshampata, ni wako mpaka kifo? Sio sasa ni wangu wacha ni practise nae zaidi na time to time ni showcase niliyofuzu? nayo hapana? Ndoa ikibuma je utaanza kujifunza upya?  hehehehe hawa wa siku hizi hawajui kusubiri, yaani hata muda wa ku-show off maujuzi hupewi.....ukitoka na hujalipia  meal, umeachwa(wakati haukuwa na uhusiano nae)....hii kwa wote, wewe na mkeo/mmeo. 



Natambua kuna kubadilika au tuseme kukua(inategemea na umri mliofunga ndoa)....uboreshaji  wa tabia au mtindo wa maisha ni jambo muhimu, maana huwezi kuishi kama kijana/binti wa miaka 32 wakati sasa una miaka 47...Wataalamu wanasema kuwa Uhusiano haubadiliki bali wenza ndio hubadilika, mimi nabisha kwasababu ninyi mkibadilika/kua ni wazi kuwa mahitaji yenu yanabadilika na hivyo uhusiano mzima kubadilika. 



Mfano; Uhusiano wenu ulivyokuwa kabla ya kufunga ndoa ni tofauti na sasa mmefunga ndoa, na uhusiano huu baada ya ndoa hubadilika baada ya kupata watoto. Kitu pekee kati yenu ambacho  hakibadili ni Penzi mlionalo kwa kila mmoja wenu, Upendo uliokuwa nao mwanzo huwa ni ule ule, unaweza kuongezeka kutokana na "values" alizo-ongezea kutokana na uzoefu na changamoto mlizopitia kama wana ndoa ila haubadiliki no matter what!



Sio tu kwamba wewe ni mtu tofauti kwa kiasi fulani tofauti na yule wa miaka 32, mahitaji yako ya kimwili pia ni tofauti(kutegemeana na ulipo kiafya/career/umri wa watoto wenu,), unaweza kujikuta unahitaji zaidi ya kila siku(kwamba sasa ni mara 4 kwa siku) au umeshuka zaidi ya mara moja kwa Wiki(and you are married? why?).



Kwasababu tu Mkeo/Mumeo halalamiki na kila mara anafika umpelekago haina maana anafurahia mwanzo wa safari au safari yenyewe...hata kama ni "mvumilivu hula mbivu" jamani shulti safari iwe yenye manjonjo na vionjo. Ukute mwenzako anahamisha mawazo kwa mtu mwingine ambae humtamani ila hawezi kumpata au kamuona Twitter soft "corn" na ndie anamsidia kufika....usimuulize Mkeo/Mumeo kuhusu hili, mtagombana. Jua tu hii inawezekana usipo impruvu.



Ngoja nije kwa engo tofauti, ikitokea leo hii umekutana na Mpenzi wako wa kwanza kabisa na ukalazimika kukumbushana ili kuokoa maisha ya yenu kwa uzoefu mlio nao sasa, huoni kuwa itakuwa vema kama utatumia nafasi hiyo kuonyesha ujuzi wako ambao hukua nao enzi zile ulikuwa bongolala kwa kufanya mapenzi? No? 



Nachojaribu kusema ni hiviii, jitahidi kuboresha, kumbushia na kuongeza ujuzi, kama ambavyo unafanya kwenye maeneo mengine ya maisha yenu kama Mume na Mke. Sio kwasababu mmefunga ndoa basi ndio mmemaliza mwendo. Maisha ya ndoa kwenye kitengo cha tendo la ndoa yanaweza kuwa very boring, sasa kwa sababu mmezoeana mnachukulia poa na hakuna ari wala kujisukuma na kuweka effort kwenye kona hiyo.


                                                       Picha kwa hisani ya Google.


Ndoa ya muda mrefu (zaidi ya miaka 10) can become boring kirahisi sana kwenye sekta ya intimacy na Tendo, mtatoana mitoko kila wiki na kupoteza pesa kwenye expensive zawadi  wakati mnachohitaji ni kuwasiliana kwa uwazi na kupeana/jifunza mambo mapya au kurudisha yale mliyokuwa mkiyafanya miaka 3 ya kwanza kabla watoto hawajaingilia "maisha" yenu.



Kuna ule wakati unafikiria namna gani unataka kufanywa au unakumbuka siku ile(miezi 6 iliyopita) jinsi alivyokushughulikia, unapata mhamko...unaamua kum-text mumeo/mkeo, yeye anakujibu "hebu acha utoto"😆. Improve  kwa ku-practice na mwenza wako na siku moja moja show off  ulichofuzu, acha uzee.


Bila kujali urefu wa ndoa yako (sijui kwa uoande wa wanaume) ila dada, Mumeo akikupitia/kumbatia kwa nyuma bado unatakiwa kusisimka/nyegeka/mtaka mumeo kimwili....anyways.

Bbai.

Comments