What to do when umevamba(married into these families )....

 Soma sehemu ya kwanza (Usiolewe kwenye familia hizi) kwa kubofya hapa

1-Washirikina, wana Imani ya Dini kupilitiliza(makanisa ya kisasa) na wanachukiana(wanaoneana wivu)-Hawa huwa ni hatari wenyewe kwa wenyewe, na kujaribu kuumizana kwa kulipizana visasi au kuonyeshana nani ni nani. Ukichunguza utajua tu how they move na pengine your spouse have already told you.


Cha kufanya: Kama Imani yako ya Dini ni vuguvugu au huna kabisa, dada/kaka anza kuamini na ongeza majeshi ya Mungu, kumbuka unahitaji maombi ya nguvu na mara kadhaa kwa siku(kila siku) hivyo hakikisha una muda mwingi wa ziada vinginevyo husimami au hautoishi kwa furaha wala amani kwenye hiyo ndoa. Nakuambia hivyo kama Mama wa nyumbani mwenyewe watoto 3 na Baba yao ambae sina muda wa kuongeza nguvu kwenye maombi dhidi ya maadui wangu (maCCM). 


Sasa Kama wewe ni mama wa kazini niamini mimi nakuambia hutokuwa na muda wa kufanya maombi makuu daily  kuilinda familia yako Dhidi ya familia ya Mume/Mkeo na maadui wengine huko mtaani na pengine Maccm au Machedema. Utakufa kwa stress(Stress husababisha maradhi ya Moyo). 


Hebu picture this, you as a wife(sijui ratiba ya husbands) get home from work, watoto wanakusubiri na Mumeo yupo njiani anakuhitaji, hapo hapo kuna selfcare, , lone time to relax, skincare halafu unatakiwa utoke uende Kanisani kufanya maombi makuu kwa masaa mawili,  unatakiwa kuamka saa Kumi na Moja kuwahi job.....8hrs sleep where? Usitake nianze kuzungumzia Homono zinabadilika mara 4 ndani ya siku 28, hongera kama  kwako ni 35days. Hapa mwenzangu, omba Talaka au mshawishi mumeo mhame Nchi halafu mnawachunia wote shenzi type.


2-Wapenda Mikutano, kila jambo lazima kuwe  na kikao na jambo hilo  likuzwe na liwe la Ukoo mzima. Hii utaoina mapema tu mnapoanza mahusiano, kuna siku mlipishana na mwenzio akakimbilia kwa Mama/kaka/dada nae akaitisha kikao kujadili suala hilo ambalo kiukweli halikuwa kubwa kiasi cha kuwafikia ndugu/wanafamilia.


What to do; Hameni, iwe Wilaya, Mkoa yaani live far away na ukiweza another country, pia hakikisha na kujitahidi kuweka mipaka kati yako na mkeo/mumeo, hakuna haja ya ku-share kila jambo na familia nzima. Enzi nakumbuka kwenye sherehe za kufunga ndoa, wanandoa walikuwa wanaambiwa matatizo madogo malizeni wenyewe, yale makubwa tuleteeni. Kumbuka unapolekeka jambo negative kwa wazazi/ndugu zako, wanalitunza na kumuona Mumeo/mkeo kwa namna hivyo hiyo negative no matter what, itamuondolea respect kwa ndugu zako.


3-Karibu kila mmoja wao  wa kiume alizaa nje ili kupata mtoto wa kiume au wanawake wanatoka na waume za watu au/na walizaa kabla ya Ndoa(na hawajaolewa)...hawa bana, wanaruhusu cheating, yaani hawana moral wala family values. Hawa aisee hata ikitokea  your spouse cheats. be sure his/her family know and they support them(wanamtunzia siri na wanatembeleana na Kimada wa mkeo/mumeo).


Nini cha kufanya: Hiyo familia niwazi hawapenzi wanawake,japokuwa wana mama na dada(wanawake pia huwa wanachukia wanawake na kuchukia uanamke wao so...). Jiweke mbali na watoto hao wa nje ya ndoa ya Mke mwenzio(mmeolewa familia moja) na Shemeji yako na waume za watu na watoto wao kama bado wanao. Mf; Wifi/Mpwa anatoka na mume wa mtu na wote kwa pamoja wanataka kuja kukutembelea, ingia mtini(kuwa busy). Kwamba hupatikani, akitaka aje peke yake bila mume wa mtu na watoto wao kama anao, wakwepe wote. Yaani kaa mbali na mikosi ya Wifi zako.


4-Ambao hawajaondoa mavumbi(wengi wao ni wa la saba la Mkoloni, Nyerere, Mwinyi na Mkapa). 

Cha kufanya; Hawa, dah, wasamehe tu ila kumbuka kuweka mipaka na hakikisha hawaivuki ili kutozeana sana, vinginevyo hawa ni wale wanakuja kwako na kukuambia "this is my brother/sister's house i can do what i want"....hiyo ni nyumba yako,  hapo ni kwako, wakija waheshimu sheria na mipaka uliyoiweka hapo nyumbani kwako.


                                                      picha kutoka google


5-Wale wanao amini Mali au mafanikio ya ndugu kuwa ni Mali/mafanikio yao pia na vizazi vyao. Hii hata mumeo/mkeo atakuwa nayo sababu kalelewa kwenye familia hiyo, hapa dada/kaka unahitaji kumuelimisha kuwa kila mmoja wenu kaja Duniani kivyake japo wote chanzo na njia ni moja, hiyo haina maana upatacho wewe ni chao na wapatacho wao ni chako. Sisi ni Mwili mmoja mbele ya Mungu na Serikali hivyo the two of us will work hard for  our little family we created. If some people in your family need help and we are able, we will try our best to help them, but what is ours, is for us and our children. Okay!! Do that.


6-Ile familia bwana'ko ndio mwanaume pekee halafu ni wa kwanza/mwisho kuzaliwa. Mwambie mumeo aache u-mama na a grow some strong balls na ndevu, ajitegemee kiakili na kimawazo na kuweka mipaka, Aache kudeka na kuachia ndugu zake wam-treat kama vile anamika 12., huyu wa mwisho. 


Ikiwa mumeo ni kwanza kuzaliwa , da-daaaaa jiandae kupokea wifi/shemeji zako mara kwa mara na matatizo yao, watamuona mumeo kama Baba yao....hapa nenda nae taratibu, huyu yupo damaged na hajui what he is supposed to do. Muelimishe kuwa ndugu zake sio jukumu lake bali jukumu la wazazi wake, anaweza kuwasaidia pale anapoweza ila sio kuegemea kwao tu na kujisahau yeye kama mwanadamu, mume na baba kwa watoto wake,,,aweke nguvu hapo kwa watoto wake. Itachukua  muda, ila with your love, respect, great sex and support atabadilika na atapona.


7-Wasujudu mwanafamilia mmoja sababu tu anapesa au kaolewa na mwenye pesa kuwazidi wengine familiani

Unafanyaje; Waache waendelee, maana hii doesn't concern you, unless otherwise mumeo nae yupo hivyo, hapo sasa inabidi umshushue aache ujinga/ushamba, akue na atafute pesa zake. Muonyeshe namna ya kutobabaikia watu kwasababu  wanapesa ambazo hata yeye akitaka kushindana nao anaweza kuwa nazo.


8-Mpenzi kasomeshwa kama "uwekezaji" kwamba afanye ajualo ili kurudisha faida. Tangu kaanza hajamaliza tu deni? hebu mkalishe chini na kisha pigeni mahesabu kwa thamani ya pesa ya wakti ule, kama bado kuna mabaki pay back and get done. Mwambie mkeo/mumeo huwezi kuishi maisha yako yote kulipa madeni ya wazazi wako, wazazi walitakiwa kutokuzaa watoto wengi hivyo. Ulitakiwa kuzaliwa peke yako na kusomeshwa bila baggage ya ndugu zako for life(hii haina uzungu, ni common sense).


9-Mama/Baba anakupa kipaumbele wakati kuna wakwe zake wengine kabla yako. Unafanyaje, unaweza ku-enjoy but kumbuka kuwa wewe ni mgeni na unaweza kuwa chambo, nenda taratibu na kwa uangalifu, usijisahau na usiamini mtu(sikiliza. uliza maswali ila usiongezee neno)...utalibeba.


10-Hawakutaka ndugu yao afunge ndoa na wewe

Cha kufanya? Hapa unaweza ku manage if your husband is a very strong and have strong mind who can stand up for himself(na wewe), hii haitofanya wakupende bali wanaweza kukuheshimu, again kama mumeo yupo as nimesema hapo awali mtaishi mbali nao na will limit communication with them.  Kama yeye ni mkeo, hakikisha mnaishi mbaaali na familia nzima na unamtunza binti yake vema, hakikisha hapati mashtaka kuhusu wewe kutoka sehemu ya tatu(majirani,rafiki,ndugu wanaowatembelea), maana kwa uhakika mkeo hawezi kupeleka malalamiko huko, hasa kama anakupenda.


11-Wana maradhi ya kurithi Saratani(ya Damu, Matiti, Mifupa, Mapafu, Ngozi, Tezi Dume), Kisukari, Moyo, Ukoma, Ukichaa/Akili, Upofu, Maradhi ya ngozi n.k,

Unafanyaje hapa? Unaishi kwa tahadhari, jitahidi kula vema na kujali/pima afya kwa familia nzima mara kwa mara, hakikisha  Bima ya Afya in-cover maradhi hayo(usisubiri mpaka mtu augue) na kumuomba Mungu awaepushie mabalaa.


Bbai.

Comments