"My dear,
mimi ni msichana wa miaka 25, bado nipo chini ya himaya ya bi mkubwa, nimepata mimba na siku zote nasema sitatoa mimba. Sema bi mkubwa wangu nitamueleza vipi? Naombeni msaada jamani tafadhali dada dinah na wachangiaji wengine kwani nipo njia panda.
Boyfriend yeye yu tayari kuwa baba japo wote bado twamalizia masomo si fikirii sana juu ya yeye kwa sasa, yeye si ngumu kujadiliana naye isipokuwa mama yangu, sijui nianzie wapi kumwambia??? msaada tafadhali tafadhali...".
mimi ni msichana wa miaka 25, bado nipo chini ya himaya ya bi mkubwa, nimepata mimba na siku zote nasema sitatoa mimba. Sema bi mkubwa wangu nitamueleza vipi? Naombeni msaada jamani tafadhali dada dinah na wachangiaji wengine kwani nipo njia panda.
Boyfriend yeye yu tayari kuwa baba japo wote bado twamalizia masomo si fikirii sana juu ya yeye kwa sasa, yeye si ngumu kujadiliana naye isipokuwa mama yangu, sijui nianzie wapi kumwambia??? msaada tafadhali tafadhali...".
Comments
Sikushauri hata siku moja kupata ibilisi wa kutoa mimba hiyo kwa sababu nilizokwisha zielezea mwanzo, na siku zote tufanyapo mapenzi yasiyosalama tunajua mwisho wake ni huo, Hivyo sioni sababu ya wewe kuona ajabu. Muhimu kwako ni kuhitaji radhi ya mama ili katika kpindi chako cha kumalizia shule yako Mama ako ndio akawe msaada kwako ktk hali uliyonayo na baadae mtoto wako.
Pole kwa mzigo wa mawazo ulionao lakini naamini hata awe mkali kiasi gani mwisho wa siku ataikubali tu hiyo hali kwani imeshatokea. Nakutakia kila la kheri dada.
Je huyo mjamaa mlikubaliana nini katika kusakata hiyo gemu iliyokutia sokomoko?
Mliibiana tu au vipi?
Nimeuliza maswali hayo ili nijue cha kukushauri maana sioni kama ni bifu zito sana kumweleza mamayo bayana kilichokusibu hapo ulipo.Mama ndiye wa karibu na mtoto wa kike na ndiye mshauri wako mkuu.Usije ukaitoa bibie huyo kiumbe ndiyo rais mtarajiwa wa Tanzania katika mwongo wa tano ujao kuanzia sasa.
Mbili hakuna kosa kaa kuzaa na mwanafunzi mwenzako utamtunza vipi huyo mtoto au ndio unataka akakuzwe na bibi.
Na what the hurry?kama baba anataka kuwa baba siungesubiri umalize shule
Kama ilinavyoaminika siku moja utapata taarifa ya m2 uumpendaye kupoteza maisha basi ujue kila jambo linaweza kutokea hata kuwe na vipingamizi na litakubalika tu. Nasema hivyo kwa sababu bi mkubwa anategemea siku moja utamletea mjukuu lakini hajafikiria kivipi au lini kwa sababu anakuona bado ni mdogo. Ningependa kukushauri kama unashindwa kumweleza wewe kama wewe, basi umtafute ndugu ambaye atasikilizwa atakapomwelezea jambo kuhusu tatzo ulilo nalo. Naamini kwa umri uliofikia atajifikia na kugundua kuwa sasa ni wakati wako muafaka wa kupata mtoto tena mwanaume kakubali alichokifanya hakuna tatzo. Kiukweli haitamwingia akilini kwa siku ya kwanza au ya pili tu lkn siku zingne atakubali na yy ndiye atakae kua msaada mkubwa kwako. USIJIUMIZE KWA KUFIKIRIA SUALA DOGO DADA YANGU.
jcaustical@yahoo.com
cha msingi..ongea na mama mueleze kuwa umepata mimba usioipangia na muahidi kuendelea na kumaliza masomo yako..pia muombe msamaha ila mwambie utaendelea kuwa mtoto mzuri...vyovyote atakavyosema maneno hayaui..chukulia poa cha msingi wewe msg send..mzigo wa kukaa kimya ni mkubwa kuliko wa kusema na kuwa muwazi hasa kwa mzazi..pia mwambie jamaa kama nae anakupenda na anajiamini awaambie wazazi wake au mzazi wake mmoja ili iwe rahisi kama backup kwakko incase of anything pia is good for the coming innocent mtoto
Gluv
gluv100@yahoo.com