Mume wangu anatereza nje na "dada" zake na kuzaa ovyo, nifanye nini?


"Dada Dinah,Salaams.

Naona nianze moja kwa moja matatizo yangu. Mimi ni mwanamke umri miaka 38, nimeolewa miaka mitatu iliyopita, sina mtoto. Ninaishi na mume wangu pamoja na binti wa mume wangu ambaye anasoma boarding.


Tatizo kubwa ni kuwa nimeshindwa kumzalia mtoto mume wangu na hivyo ume wangu kazaa na housegirl wetu. Kabla hajampa ujauzito, aliomba nimfukuze akidai hana adabu. Baadaye nikaambiwa na majirani kuwa housegirl wetu ana mimba. Sikujua ni ya nani hadi hapo baadaye.


Baada ya muda nikagundua kuwa mume wangu anatembea na msichana jirani aliyekuwa akimuita dada kwa vile wanatoka sehemu moja. Dada huyo alikuwa akija kututembelea na wakati mwingine akitusaidia kazi wakati mimi nikisafiri. Kazi yangu ni ya kusafiri na baadaye nikahamishiwa Wilayani kabisa.


Kurudi kwangu nyumbani ni siku za weekend tu.Kumbe yule dada akawa anakuja kulala na mume wangu usiku. Nikaambiwa na majirani. Nilipomuuliza kama kawaida alikataa. Yule mwanamke baada ya kuona nimegundua amehama mkoa na kuhamia Dar.


Hivi karibuni nimetumiwa sms na msichana akiniambia kuwa ana mimba ya mume wangu na kuwa kaipatia nyumbani kwangu kwenye kitanda changu na kuwa eti nisubiri kuletewa watoto. Nilipofuatilia nikagundua kuwa huyo msichana ni mwanafunzi wa Sekondari na wanatokea sehemu moja pia na mume wangu.


Nilipomuuliza mume wangu alikanusha kama kawaida. Lakini baadaye nikapata taarifa kuwa mume wangu kampiga sana yule msichana hadi kulazwa Hospitali kwa kuwa eti kanitumia sms. Nilipomuuliza alikubali, halafu baadaye alikanusha akidai kuwa ingekuwa ni stori ya kweli basi angeshitakiwa police.


Kweli mambo ni mengi, mojawapo likiwa la mume wangu kutopenda kabisa mimi kugusa simu yake. Nilishakuta sms za wanawake wawili kwenye simu yake, mmoja ninayemfahamu. Hata nikiamka kujisaidia usiku, yeye anashituka akihofia simu zake zisiguswe. Mume wangu anao marafiki wengi wa kike yeye akiwaita ni dada zake na wengi wa kabila lake la Wapare, ambao wengine ndio hao anaotembea nao.


Sasa mimi sielewi hili kabila, nimegundua kuwa ni Malaya sana, hadi najuta. Mimi nafanya kazi na kipato changu ni kikubwa kuzidi cha mume wangu. Namnunulia nguo nzuri anapendeza, nimemsaidia kumjengea nyumba mama yake na sasa tunajenga ya kwetu. Nampenda sana mume wangu na yeye anadai kunipenda.


Kutokana na hali hiyo afya yangu Kisaikolojia imeharibika, naombaeni ushauri wenu. mngekuwa ni nyie mngefanya nini"?

Comments

Anonymous said…
mmmmmmhhhhh dada yangu kwanza, nakupa pole sana kwa jinamizi hilo linalokukosesha amani kwenye ndoa yako.

Maelezo yako yamenifanya nitamani kukuona ili tukae tuongee kwa undani zaidi na yamkini nikupe ushauri ambao unaweza kukufaa zaidi maana vitu vya kusimuliwa vinakosa maelezo mengine mengi ambayo yanaweza kuleta nuru zaidi katika tatizo.

Mimi nikiwa mwanaume kwa kweli nimesikitishwa na kitendo cha mumeo kama ulioyasimulia ni kweli yote. La kukushauri kwa kweli linakuwa gumu,ila nakuomba sana jaribu kuvumilia kwa kiasi kikubwa kwa sababu hujamkamata na yeyote na wala hujapata kithibitisho chochote mkononi mwako zaidi ya masimulizi na sms unazopata kutoka kwa watu wa nje.

Inawezekana kabisa mumeo ni mzinifu na kuwa na wanawake wengi kama ulivyosimulia,ila jaribu kuwa mtulivu ili ujue ukweli ulio halisi kuliko masimulizi.Na kwa sasa hivi jaribu kutumia kinga muwapo kwenye maliwazano yenu ya night food.

Weka mitego yako kisirisiri ili uweze kumnasa mwenyewe kwa ushahidi wa kutosha ndipo uwe na nguvu ya kuwa na maamuzi ya busara. Najua humu wamo wengi wenye hasira waliotendwa watakwambia mtupe chini au mkimbie,mwache hakufai nk.Naomba uwe makini sana ili uweze kupata maamuzi yaliyo sahihi na wala siyo yale ya kukupotosha.

Dada, nakuombea sana jinamizi hilo limtoke kabisa huyo mumeo na pia muombe Mungu na wewe kila kukicha ili aingilie kati ndoa yako isalimike.Mungu aendelee kukutia nguvu katika wakati huo mgumu maana naelewa jinsi inavyoumiza sana kama ulivyosema imeanza kukula kisaikolojia.Tulia dada na mpe Mungu nafasi akusahuri na kukurekebishia tabia ya mumeo.

Uwe na amani ya Bwana daima.
jeromy E said…
pole dada yangu kwa hali hiyo inayokusibu,,mimi nina maswali machache kwanza ambayo hujayaweka wazi labda kwa kuhofia mail yako kua ndefu sana...

1. umesema umeolewa ila hukutuambia kua mlifunga ndoa au lah au ni kuchukuana na kuwekana ndani tu

2. umesema ni miaka mitatu tu imepita tangu umeolewa je huyo mumeo mlianza mahusiano mda mrefu kabla ya kuoana au mlikutana gafla bila kufahamiana vyema na kuamua kuoana? kwani inaonesha huyo mumeo ni MALAYA TENA WA KUPINDUKIA hivyo kama mngepata mda wa kumchunguza vyema kabla ya kuoana ungeweza kumtambua vyema.

3. umesema kua umeshindwa kumzalia mtoto ila hiyo ndoa yenu ina umri wa miaka mitatu tu je labda umepima na kutambua kua huwezi kuzaa au ni kipi kilichokufanya useme umeshindwa kumzalia mtoto?? kwani kwenye ndoa mtoto anaweza patikana hata baada ya miaka mingi kupita.

4. nimefurahi kua wewe ni muajiriwa, na pia umeolewa lakini Je umefanya yapi katika kuijenga ndoa yako na kuiimarisha hasa kwa kuzingatia kua unafanya kazi mbali na mumeo na mda wa kuonana na mumeo ni finyu sana ( only wk ends)kwani sitetei umalaya hata kidogo ila ni muhim tuangalie ni kipi kinacho changia na kujitahidi kukabiliana nacho.

umesema uwezo unao wa kifedha ila pia uwezo wa kimapenzi unahitajika sana kwani katika ndoa mapenzi yanatakiwa yawe zaidi ya pesa.

suala la afya yako kwa sasa ni la muhimu zaidi hivyo ningependa kukushauri kwanza ikiwezekana uende ukacheki afya yako then kaa chini na huyo mumeo uongee nae kwa uwazi na kwa mapenzi ya dhati kuhusu hali halisi ilivyo then akili kichwani mwako kuchukua hatua zaidi kujinusuru kwa huyo haramia wa mapenzi especially kama hataonesha dalili yoyote ya kukusikiliza na kubadilika kabisa.

weka uvumilivu pigania ndoa yako ila sio kwa kuitoa roho yako wakati unaempigania yeye hana habari kabisaaaa

J. E
Anonymous said…
Pole sana dada mzuri, naomba ufanye kila uwezalo uilinde ndoa yako maana inakaribia kuvunjika, hakuna watu wabaya kama wapare, usimwamini mpare wa kike ata siku moja kwaiyo ata ukiambiwa huyu ni dada yangu kuwa makini sana, nimevunja ndoa sababu ya rafiki yangu mpare kutembea na mme wangu 2 yrs bila mimi kujua, at the end ye mwenyewe mpare akaja kuniambia kuwa mme wangu maraya sana anamtongoza kumbe kiukweli anatembeanae! mme wangu alikuwa mwema some how aliamua kusema ukweli kabisa kuwa huyu rafiki yako ni mnafiki maana natembeanae 2 yrs ss na sijui kwannn ameamua kukwambia leo, upo hapo dada? mie niliamua kuvunja ndoa kabisa maana niliumia sana, so take cr sana na WAPARE
Anonymous said…
inasikitisha sana,w.ke kwa kutokujiamini.sasa hapo raha ya ndoa iko wapi?kwa nini unashindwa kuachana nae wakati unaweza kujikimu kimaisha?au unaogopa kusemwa na ulimwengu kwa nini mmeachana?najua ni ngumu anza maisha kivyoko,before is too late.huyo bwana hata condom hatumii kwa hao w.ke.inavyoonyesha hata tukikushauri kwa kuwa unampenda utaendelea kukaa nae tu.kwa kweli nakuonea huruma,bora upate ukimwi kwa zinaa yako mwenyewe,kuliko kuletewa ukimwi wakati wewe umejituliza,maana mateso ni mara 2 yake,wake up dada,jijali mwenyewe,usijali maneno ya wote,unampendezesha,anakula raha na wengine.achana nae as faster as you can,najua ni ngumu utaweza tu,na utakuwa happy
Anonymous said…
Mpenzi angalia mbele mimi wakwangu ananisumbua hivyo hivyo lakini mtoto ndio anayenizuia na kipata changu pia kidogo ningekuwa na uwezo ningehama hata mkoa ili nisimwone roho inauma nikimwona mtoto wangu na jinsi ninavyowaza kumtenga na baba yake kwa sababu ya tabia yake.
Anonymous said…
Mmh, pole dada yangu, kama mlifunga ndoa jaribu kuwaomba washenga wenu waweze kuwaweka chini ili mmalize hilo tatizo. matatizo yapo mengi zaidi ya hayo ktkt ndoa na usifikirie suala la kuachana kwasababu unaweza kuachana na huyo leo kesho ukampata mwenye matatizo zaidi ya huyo. cha muhimu pigania kusolve hilo tatizo ipo siku atatulia tu, najua inaumiza sana but jaribu katika maombi yako ya kila siku kumuombea mumeo aweze kubadilika. na inabidi uchunguze kwa umakini kuhusu hao wanaodai wanamahusiano na mumeo kwasababu wengine wapo tu kwa ajili ya kuharibu ndoa za watu. M/mungu akutangulie.

precious
Anonymous said…
Hao ndio Wapalestina mnatakiwa muwe waangalifu mnapofikia suala la ndoa.
Anonymous said…
mhh jamani pole sana mdogo wangu,wanaume wote ni wahuni ila Wapare funga kazi,sasa hapo ni kujikinga na Ukimwi,sikwambii ondoka ila wewe mwenyewe mdogo wangu uishi kimachale,PENDA NDUGU ZAKO,SADIA NDUGU ZAKO,JIPE RAHA ,USIJIACHIE UTAPATA MAPRESSURE MENGI,MI wakwangu alitembea na mwanamke eti kasema ni ndugu yake ,ila sijawi kumuona toka nimjue ,ila amekuja mpaka nyumbani ,na kwenye harusi ya huyo ndugu yake amekwenda,mhh yaani we acha tu..
Anonymous said…
Mpendwa, mimi nakwambia sentense moja tu....KIMBIA.

Huyo mmeo hakuheshiku kabisa na wala hana hata soni, yaani anatembea na mahousegirls na wengine jirani na kwenu. Halafu anangonoka bila hata kutumia kondomu. Inamaana hakujali na wala YEYE MWENYEWE HAJALI AFYA YAKE. Ilimradi Mola amekujalia kazi nzuri, concentrate kwenye kazi dadangu, sikuhizi usione kina dada wengi wako wenyewe wenyewe tu, wanaogopa kuishia na kilo mbili mwenzangu.
UAMUZI NI WAKO...KWAKE KUBADILIKA NI KAMA USIKU NA MCHANA.
Anonymous said…
Du hapo nimechoka, tatizo si kabila kama wengine mnavyofikiri tatizo ni tabia ya mtu Wapare wangapi tuko nao tunaishi nao lakini hawana tabia kama hizo please jaribuni kufikiria kwanza eti vile umetendwa na Mpare unafikiri Wapare wote wako hivyo, La hilo sikubaliani na nyie ina maana wanawake wote wanaonyanyasika kwa mapenzi wameolewa na wapare hebu jaribuni kuwa na Fikra za kikubwa msiwe kama watoto wadogo kwa fikra zenu finyu.
Anonymous said…
Kama hali ndio hiyo nakuomba fikia maamuzi mazito.

Jiulize mwenyewe ni
1. hatari ngapi zinazokukabili kwa kuishi na mwanaume wa tabia hii
2. Je ungependa kuishi na mwanaume wa tabia gani
3. Je mwanaume uliyenaye anakidhi vigezo vyako wewe mwenyewe?
4. Mapenzi uliyonayo kwake unaweza kustahimili kuishi naye licha ya vituko hivyo?
5. Kwa wewe mwenyewe mwanaume anathamani gani?
6. wewe mwenyewe kama mwanamke unahisi una mapungufu gani ya wazi na yale ya siri?

Katika maisha tumejionea wapo wanawake wameendelea kuishi na wanaume wa namna hii bila ya tatizo. Tena wengine wanaume zao wametembea mpaka na watoto zao wenyewe!!!!!! Na utashangaa mwanamke bado yupo tu, kesi siku mbili tatu mara mambo kimyaa lijibaba linaendelea kula kwa mtoto na mama.

Halafu tena tumeona wanawake malaya wanatembea mpaka na house boy, au mpaka na marafiki wa mume. But utashangaa mwanaume wala hachukui hatua zozote na akiambiwa anakuwa mkali kwa aliye mwambia.

Kwa hiyo mpendwa naomba yatafakari maisha yenu, then chukua maamuzi mazito, yaani au kuendelea kuishi naye bila ya malalamiko au kuachana nae kabisa.

Halafu naomba nikutahadharishe jambo moja wanaume wa namna hii ni nadra sana kuacha tabia hii, kinachotokea mara nyingi pale wanaposema wameecha tabia hii, ukweli kinachotokea ni kuanza kutongoza wanawake wa mbali ambapo wewe huwezi kufahamu kwa urahisi.

Kuhusu kabila sidhani kama ni tatizo hiyo ni tabia tu ya mtu haina uhusiano wowote na kabila lake.

La mwisho naomba usikate tamaa ya kuzaa, umri wa miaka 38 bado kuna matumaini labda kama ulipata matatizo na kizazi kikaondolewa ndio unaweza ukate tamaa.

JIPI MOYO UTAPATA UFUMBUZI.
Anonymous said…
By experience, wapare wengi ni nyoka japo si wote. Mi kama mwanamume, kama mke wangu hazai nitakuwa wa mwanzo kumfariji kuliko kumuumiza. Sitegemei kuoa mke mwingine au kutoka nje kwaajili tu eti wife hazai. My wife is my heart, siwezi kuumiza moyo wangu mwenyewe
Anonymous said…
Pole dada mpenzi. Langu kuu ni kuhusu wewe mwenyewe, embu jiangalie upya na hiyo kazi yako ya akukaa mbali na mumeo? Ni ngumu wakati mwingine ukizingatia wanaume ni wadhaifu mno, so akipata nafasi kama hiyo anajustify, ingawa simsupport kwa tabia zake. Linda ndoa yako mpenzi.
Anonymous said…
all in all leave hi alone, ujazaa unakaa nae wa nini atakupa ukimwi huyo uharibu future yako huyo sio mpango wa Mungu, Unajua watanzania wengi tunaogopa kuachika kisa watu na ndugu jali maisha yako sio wapare tu wanaume mafilauni wengi sana, mpenzi take care mchumba wako aliyekupangia Mungu yuko njiani anakuja wewe unamchelewesha kufika kwako kwa sababu ya huyo kiruka njia, fumbua macho natamani kupata namba yako ya cm nikushauri nikupe na mifano mbona utaachika haraka.