"Dada Dinah,Salaams.
Naona nianze moja kwa moja matatizo yangu. Mimi ni mwanamke umri miaka 38, nimeolewa miaka mitatu iliyopita, sina mtoto. Ninaishi na mume wangu pamoja na binti wa mume wangu ambaye anasoma boarding.
Tatizo kubwa ni kuwa nimeshindwa kumzalia mtoto mume wangu na hivyo ume wangu kazaa na housegirl wetu. Kabla hajampa ujauzito, aliomba nimfukuze akidai hana adabu. Baadaye nikaambiwa na majirani kuwa housegirl wetu ana mimba. Sikujua ni ya nani hadi hapo baadaye.
Baada ya muda nikagundua kuwa mume wangu anatembea na msichana jirani aliyekuwa akimuita dada kwa vile wanatoka sehemu moja. Dada huyo alikuwa akija kututembelea na wakati mwingine akitusaidia kazi wakati mimi nikisafiri. Kazi yangu ni ya kusafiri na baadaye nikahamishiwa Wilayani kabisa.
Kurudi kwangu nyumbani ni siku za weekend tu.Kumbe yule dada akawa anakuja kulala na mume wangu usiku. Nikaambiwa na majirani. Nilipomuuliza kama kawaida alikataa. Yule mwanamke baada ya kuona nimegundua amehama mkoa na kuhamia Dar.
Hivi karibuni nimetumiwa sms na msichana akiniambia kuwa ana mimba ya mume wangu na kuwa kaipatia nyumbani kwangu kwenye kitanda changu na kuwa eti nisubiri kuletewa watoto. Nilipofuatilia nikagundua kuwa huyo msichana ni mwanafunzi wa Sekondari na wanatokea sehemu moja pia na mume wangu.
Nilipomuuliza mume wangu alikanusha kama kawaida. Lakini baadaye nikapata taarifa kuwa mume wangu kampiga sana yule msichana hadi kulazwa Hospitali kwa kuwa eti kanitumia sms. Nilipomuuliza alikubali, halafu baadaye alikanusha akidai kuwa ingekuwa ni stori ya kweli basi angeshitakiwa police.
Kweli mambo ni mengi, mojawapo likiwa la mume wangu kutopenda kabisa mimi kugusa simu yake. Nilishakuta sms za wanawake wawili kwenye simu yake, mmoja ninayemfahamu. Hata nikiamka kujisaidia usiku, yeye anashituka akihofia simu zake zisiguswe. Mume wangu anao marafiki wengi wa kike yeye akiwaita ni dada zake na wengi wa kabila lake la Wapare, ambao wengine ndio hao anaotembea nao.
Sasa mimi sielewi hili kabila, nimegundua kuwa ni Malaya sana, hadi najuta. Mimi nafanya kazi na kipato changu ni kikubwa kuzidi cha mume wangu. Namnunulia nguo nzuri anapendeza, nimemsaidia kumjengea nyumba mama yake na sasa tunajenga ya kwetu. Nampenda sana mume wangu na yeye anadai kunipenda.
Kutokana na hali hiyo afya yangu Kisaikolojia imeharibika, naombaeni ushauri wenu. mngekuwa ni nyie mngefanya nini"?
Comments
Maelezo yako yamenifanya nitamani kukuona ili tukae tuongee kwa undani zaidi na yamkini nikupe ushauri ambao unaweza kukufaa zaidi maana vitu vya kusimuliwa vinakosa maelezo mengine mengi ambayo yanaweza kuleta nuru zaidi katika tatizo.
Mimi nikiwa mwanaume kwa kweli nimesikitishwa na kitendo cha mumeo kama ulioyasimulia ni kweli yote. La kukushauri kwa kweli linakuwa gumu,ila nakuomba sana jaribu kuvumilia kwa kiasi kikubwa kwa sababu hujamkamata na yeyote na wala hujapata kithibitisho chochote mkononi mwako zaidi ya masimulizi na sms unazopata kutoka kwa watu wa nje.
Inawezekana kabisa mumeo ni mzinifu na kuwa na wanawake wengi kama ulivyosimulia,ila jaribu kuwa mtulivu ili ujue ukweli ulio halisi kuliko masimulizi.Na kwa sasa hivi jaribu kutumia kinga muwapo kwenye maliwazano yenu ya night food.
Weka mitego yako kisirisiri ili uweze kumnasa mwenyewe kwa ushahidi wa kutosha ndipo uwe na nguvu ya kuwa na maamuzi ya busara. Najua humu wamo wengi wenye hasira waliotendwa watakwambia mtupe chini au mkimbie,mwache hakufai nk.Naomba uwe makini sana ili uweze kupata maamuzi yaliyo sahihi na wala siyo yale ya kukupotosha.
Dada, nakuombea sana jinamizi hilo limtoke kabisa huyo mumeo na pia muombe Mungu na wewe kila kukicha ili aingilie kati ndoa yako isalimike.Mungu aendelee kukutia nguvu katika wakati huo mgumu maana naelewa jinsi inavyoumiza sana kama ulivyosema imeanza kukula kisaikolojia.Tulia dada na mpe Mungu nafasi akusahuri na kukurekebishia tabia ya mumeo.
Uwe na amani ya Bwana daima.
1. umesema umeolewa ila hukutuambia kua mlifunga ndoa au lah au ni kuchukuana na kuwekana ndani tu
2. umesema ni miaka mitatu tu imepita tangu umeolewa je huyo mumeo mlianza mahusiano mda mrefu kabla ya kuoana au mlikutana gafla bila kufahamiana vyema na kuamua kuoana? kwani inaonesha huyo mumeo ni MALAYA TENA WA KUPINDUKIA hivyo kama mngepata mda wa kumchunguza vyema kabla ya kuoana ungeweza kumtambua vyema.
3. umesema kua umeshindwa kumzalia mtoto ila hiyo ndoa yenu ina umri wa miaka mitatu tu je labda umepima na kutambua kua huwezi kuzaa au ni kipi kilichokufanya useme umeshindwa kumzalia mtoto?? kwani kwenye ndoa mtoto anaweza patikana hata baada ya miaka mingi kupita.
4. nimefurahi kua wewe ni muajiriwa, na pia umeolewa lakini Je umefanya yapi katika kuijenga ndoa yako na kuiimarisha hasa kwa kuzingatia kua unafanya kazi mbali na mumeo na mda wa kuonana na mumeo ni finyu sana ( only wk ends)kwani sitetei umalaya hata kidogo ila ni muhim tuangalie ni kipi kinacho changia na kujitahidi kukabiliana nacho.
umesema uwezo unao wa kifedha ila pia uwezo wa kimapenzi unahitajika sana kwani katika ndoa mapenzi yanatakiwa yawe zaidi ya pesa.
suala la afya yako kwa sasa ni la muhimu zaidi hivyo ningependa kukushauri kwanza ikiwezekana uende ukacheki afya yako then kaa chini na huyo mumeo uongee nae kwa uwazi na kwa mapenzi ya dhati kuhusu hali halisi ilivyo then akili kichwani mwako kuchukua hatua zaidi kujinusuru kwa huyo haramia wa mapenzi especially kama hataonesha dalili yoyote ya kukusikiliza na kubadilika kabisa.
weka uvumilivu pigania ndoa yako ila sio kwa kuitoa roho yako wakati unaempigania yeye hana habari kabisaaaa
J. E
precious
Huyo mmeo hakuheshiku kabisa na wala hana hata soni, yaani anatembea na mahousegirls na wengine jirani na kwenu. Halafu anangonoka bila hata kutumia kondomu. Inamaana hakujali na wala YEYE MWENYEWE HAJALI AFYA YAKE. Ilimradi Mola amekujalia kazi nzuri, concentrate kwenye kazi dadangu, sikuhizi usione kina dada wengi wako wenyewe wenyewe tu, wanaogopa kuishia na kilo mbili mwenzangu.
UAMUZI NI WAKO...KWAKE KUBADILIKA NI KAMA USIKU NA MCHANA.
Jiulize mwenyewe ni
1. hatari ngapi zinazokukabili kwa kuishi na mwanaume wa tabia hii
2. Je ungependa kuishi na mwanaume wa tabia gani
3. Je mwanaume uliyenaye anakidhi vigezo vyako wewe mwenyewe?
4. Mapenzi uliyonayo kwake unaweza kustahimili kuishi naye licha ya vituko hivyo?
5. Kwa wewe mwenyewe mwanaume anathamani gani?
6. wewe mwenyewe kama mwanamke unahisi una mapungufu gani ya wazi na yale ya siri?
Katika maisha tumejionea wapo wanawake wameendelea kuishi na wanaume wa namna hii bila ya tatizo. Tena wengine wanaume zao wametembea mpaka na watoto zao wenyewe!!!!!! Na utashangaa mwanamke bado yupo tu, kesi siku mbili tatu mara mambo kimyaa lijibaba linaendelea kula kwa mtoto na mama.
Halafu tena tumeona wanawake malaya wanatembea mpaka na house boy, au mpaka na marafiki wa mume. But utashangaa mwanaume wala hachukui hatua zozote na akiambiwa anakuwa mkali kwa aliye mwambia.
Kwa hiyo mpendwa naomba yatafakari maisha yenu, then chukua maamuzi mazito, yaani au kuendelea kuishi naye bila ya malalamiko au kuachana nae kabisa.
Halafu naomba nikutahadharishe jambo moja wanaume wa namna hii ni nadra sana kuacha tabia hii, kinachotokea mara nyingi pale wanaposema wameecha tabia hii, ukweli kinachotokea ni kuanza kutongoza wanawake wa mbali ambapo wewe huwezi kufahamu kwa urahisi.
Kuhusu kabila sidhani kama ni tatizo hiyo ni tabia tu ya mtu haina uhusiano wowote na kabila lake.
La mwisho naomba usikate tamaa ya kuzaa, umri wa miaka 38 bado kuna matumaini labda kama ulipata matatizo na kizazi kikaondolewa ndio unaweza ukate tamaa.
JIPI MOYO UTAPATA UFUMBUZI.