Uhusiano una Mwaka, Ex wa Mpenzi amejifungua mtoto wake mwaka huu! Nifanyaje?

"Habari dada Dinah pole na majukumu ya kila siku,
mimi ni dada wa miaka 27 nina mchumba ana miaka 35 tumekuwa pamoja kwa muda
wa mwaka na miezi mitatu hivi. Nampenda sana mchumba wangu na yeye naamini ananipenda.

Tatizo limejitokeza hivi karibuni; ni kwamba kabla ya kuwa na mimi alikuwa na mwanamke ambaye alinishanitaarifu kuwa aliachana nae ndio maana mimi nikakubali na tukawa wapenzi. Sasa ananiambia kuwa huyo dada ana mtoto wake tena kamzaa this year, ina maana
hiyo mimba kapata wakati ndio tunaanza uhusiano wetu.

Sijasikia kwa mtu mwingine zaidi yake amesema eti nikisikia kwa watu na yeye
hajaniambia nitamuacha, amesema yeye ananipenda mimi na anataka niwe mke wake. Hapa nilipo nimechanganyikiwa mbaya zaidi badonampenda sana huyu kaka na sijui nifanyaje!

Yaani mpaka sasa sijamuelewa ananidanganya au ananipenda kiukweli, mwenyewe ananiomba msamaha sana kuhusiana na tukio la kuzaa na ex wake.

NAOMBA USHAURI WENU, nifanye nini?

Comments

Anonymous said…
Pole sana dada yangu mpendwa kwa matatizo yaliyokukumba.
Nikiwa kama mwanaume na uzoefu kiasi nilionao ningependa umchunguze kwa umakini mkubwa sana huyo bwana wako bila kujali kuvunjika kwa uhusiano wenu.
Nasema hivyo kwa sababu huwezi kujua kilichomleta kwako ilikua ni tamaa pekee au na mapenzi ya dhati aliambatanisha. Pia jaribu kufuatilia maisha yake na ya x wake yalianzaje, yakaendeshwaje na yakavunjikaje na hapo ndipo utapata picha halisi ya jamaa yako kama ni muonjaji na kuacha au anakudanganya na kukupotezea muda. Kikubwa usioneshe hisia za kutomwamini ili ufanikishe uchunguzi wako kikamilifu.
Nakutakia maisha yenye amani dada. (jcaustical@yahoo.com)
Anonymous said…
....'Unampenda na unaamini naye anakupenda', Huu ni uogo! ....'Ukimpenda utamlinda au atakulinda'. Kama amepata mimba, maana yake anatembea nje ya mahusiono yenu, tena peku peku - usalama wa afya zenu upo kweli hapo. Chekecha mwenye, then make a good decision!

Good luck!!!!
Anonymous said…
Huna lako hapo bibie kimbia tafuta njenge nyingine maana hilo litakuumiza daima hasa ukijua mtoto amepatikana mkiwa katika mahusiano na wewe.Hiyo ina maana jamaa anakula kuwili pasipo kujijua ninyi.Akitwanga hapo kwako anakimbia kutwanga kwa yule mwenzio ambaye kwa mtazamo wangu ndiye mpenzi wake wa kweli na wewe spea taili pale inapopata pancha moja hilo la kubadilishia.Hadi mtoto kazaliwa unafikiri mchezo dada.Utakula mwande
Anonymous said…
nyooo kkmko mwanae ni bora kuliko wewe malaya mkubwa,nyie ndio mnauaga watoto kisa mapenzi,una roho mbaya sana wewe,sasa unachukia mtoto kuzaliwa kwa sababu ya kutombana wewe na huyo mwenye mtoto? ngono yenu unaiona ya maana?kwa taarifa yako huyo jama hawezi akakuona wa maana kuliko damu yake mnaacha roho chafu wewe mwanamke mwehu kabisa
Anonymous said…
Pole sana..Ninachokiona hapa ni kuwa:
1.wewe bado unachunguza au kumchunguza sana mumeo..which is big mistake ambayo inapelekea kukufanya uishi kwa mashaka
2.bado unafuatilia data za x wake...utaumia
3.unasikiliza maneno ya watu..kwenye mapenzi mbaya sana

..anyways kwavile umeshasikia ..suala ni je ni kweli umehesabu umri wa mtoto+mimba= na umri wa ndani ya mahusiano yenu?..maana usije ukajipanikisha bure kumbe mtoto au mimba ilipatikana b4 wee hujatia timu...jaribu kutafuta proof b4 kujamuattack mumeo naogoppa usije ukakosa mume kwa data feki na wambea..mapenzi hayataki hayo..

...pia ushauri wangu kama utakuta sio kweli kuwa mtoto sio wa mumeo au ni wake ila alipatikana mimba yake kabla ya uhusiano wako nae..mi nashauri potezea na komaa na maisha yenu matamu na mumeo

Mwanaume kaishasema anakupenda na huenda akawa mumeo soon..hilo ni important sana..jaribu kuwa close na mumeo sio lazima mtembee pamoja no mawasiliano muhimu kula na kulala pamoja kama inawezekana mara kwa mara ..kuzungumzia maisha na kutoka kidogo ..utashangaa jamaa anakupa ukweli yeye mwenyewee tena bila huongo..
..jaribu kumuonesha wewe bado unampenda na kama hujali habari za mtoto wa nje utaona yeye mwenyewe atacalm down na kukupa issue...

Ila achana na mambo ya kuwachunguza x wa mchumba ako itakucost ..pia inawezekana kabisa mimba ni ya jamaa ako ila mazingira ya mimba huenda ndio zile mambo ya bahati mbaya kwani sio mwenye mimba basi kapendwa inawezekana mwanamke alitegea mimba ili apendwe na haiwezekani na unapendwa wewe..

Mwisho..tafuta uhakika...na jali mahusiano yenu kwani kama ni kweli yameisha tokea ..mpende be close open na stable muishi wote ili asitoke tena nje au kurudi kwa huyu x..

pole zote ni challenge za mahusiano..hakuna yaliyo smooth kabisa zaidi ya kuvumiliana..

Gluv...gluv100@yahoo.com
Anonymous said…
me nadhani endele na huyo kaka kwa sababu wanaume weng siku hiz wanazaa nje bila kutoa taarifa kwahyo mshukuru mungu hata huyo kakuambia ukweli, wanaume wamekuwa wababaishaji sana unaweza kukimbia hapo ukidhani ni tatizo then unakoenda ukakutana na tatizo kubwa zaid
Anonymous said…
mh dada kama hajakuoa yet mie naona u av the chance to make your life muache yeye akalee mtoto, kashakudanganya na atakudanganya tena, na atakuwa akitumia kigezo cha huyo huyo mtoto mara ataongeza mtoto wa pili na wa tatu na huyo huyo anayemuita ex wake, open up ur eyes dia friend
Anonymous said…
Aisee pole sana dear. Ningekushauri umwache huyo jamaa lakini nadhani ntakuwa nimekukwaza, ila watoto wa nje ya ndoa wanaweza leta ugomvi siku za usoni kwenye ndoa yenu. Kwa kuwa unampenda sana jamaa, nakushauri usikubali hata kidogo kuolewa nae kwa sasa. Endelea kuwa nae huku ukimsoma vizuri kwa sababu kwa sasa nina imani kutokana na tukio hilo, moyoni nawe unahisi umfahamuu vizuri huyo mchumba wako. Give two years to study him na kwa muda huo utajua ni mtu wa aina gani. Najua anaweza kukimbilia kukwambia tuoane kwa kuwa anajua waweza kumtema muda wowote tokana na hilo tukio. Please please take time to study him, time will tell.
Anonymous said…
huyo atakuwa ni mke wake acha kudanganywa na yawezekana wana ndoa nae je uko karibu na familia yao au mtu anayeweza kumfahamu vizuri embu chunguza coz men are like that, atadanganya anakupenda sasa huyo mtoto katoka wapi if he really loves you. TAKE CARE
Anonymous said…
pole sana mamii,fanya maamuzi kwa kutumia kichwa na sio moyo ambao siku zote uko dhaifu.