"Habari dada Dinah pole na majukumu ya kila siku,
mimi ni dada wa miaka 27 nina mchumba ana miaka 35 tumekuwa pamoja kwa muda
wa mwaka na miezi mitatu hivi. Nampenda sana mchumba wangu na yeye naamini ananipenda.
wa mwaka na miezi mitatu hivi. Nampenda sana mchumba wangu na yeye naamini ananipenda.
Tatizo limejitokeza hivi karibuni; ni kwamba kabla ya kuwa na mimi alikuwa na mwanamke ambaye alinishanitaarifu kuwa aliachana nae ndio maana mimi nikakubali na tukawa wapenzi. Sasa ananiambia kuwa huyo dada ana mtoto wake tena kamzaa this year, ina maana
hiyo mimba kapata wakati ndio tunaanza uhusiano wetu.
hiyo mimba kapata wakati ndio tunaanza uhusiano wetu.
Sijasikia kwa mtu mwingine zaidi yake amesema eti nikisikia kwa watu na yeye
hajaniambia nitamuacha, amesema yeye ananipenda mimi na anataka niwe mke wake. Hapa nilipo nimechanganyikiwa mbaya zaidi badonampenda sana huyu kaka na sijui nifanyaje!
hajaniambia nitamuacha, amesema yeye ananipenda mimi na anataka niwe mke wake. Hapa nilipo nimechanganyikiwa mbaya zaidi badonampenda sana huyu kaka na sijui nifanyaje!
Yaani mpaka sasa sijamuelewa ananidanganya au ananipenda kiukweli, mwenyewe ananiomba msamaha sana kuhusiana na tukio la kuzaa na ex wake.
NAOMBA USHAURI WENU, nifanye nini?
Comments
Nikiwa kama mwanaume na uzoefu kiasi nilionao ningependa umchunguze kwa umakini mkubwa sana huyo bwana wako bila kujali kuvunjika kwa uhusiano wenu.
Nasema hivyo kwa sababu huwezi kujua kilichomleta kwako ilikua ni tamaa pekee au na mapenzi ya dhati aliambatanisha. Pia jaribu kufuatilia maisha yake na ya x wake yalianzaje, yakaendeshwaje na yakavunjikaje na hapo ndipo utapata picha halisi ya jamaa yako kama ni muonjaji na kuacha au anakudanganya na kukupotezea muda. Kikubwa usioneshe hisia za kutomwamini ili ufanikishe uchunguzi wako kikamilifu.
Nakutakia maisha yenye amani dada. (jcaustical@yahoo.com)
Good luck!!!!
1.wewe bado unachunguza au kumchunguza sana mumeo..which is big mistake ambayo inapelekea kukufanya uishi kwa mashaka
2.bado unafuatilia data za x wake...utaumia
3.unasikiliza maneno ya watu..kwenye mapenzi mbaya sana
..anyways kwavile umeshasikia ..suala ni je ni kweli umehesabu umri wa mtoto+mimba= na umri wa ndani ya mahusiano yenu?..maana usije ukajipanikisha bure kumbe mtoto au mimba ilipatikana b4 wee hujatia timu...jaribu kutafuta proof b4 kujamuattack mumeo naogoppa usije ukakosa mume kwa data feki na wambea..mapenzi hayataki hayo..
...pia ushauri wangu kama utakuta sio kweli kuwa mtoto sio wa mumeo au ni wake ila alipatikana mimba yake kabla ya uhusiano wako nae..mi nashauri potezea na komaa na maisha yenu matamu na mumeo
Mwanaume kaishasema anakupenda na huenda akawa mumeo soon..hilo ni important sana..jaribu kuwa close na mumeo sio lazima mtembee pamoja no mawasiliano muhimu kula na kulala pamoja kama inawezekana mara kwa mara ..kuzungumzia maisha na kutoka kidogo ..utashangaa jamaa anakupa ukweli yeye mwenyewee tena bila huongo..
..jaribu kumuonesha wewe bado unampenda na kama hujali habari za mtoto wa nje utaona yeye mwenyewe atacalm down na kukupa issue...
Ila achana na mambo ya kuwachunguza x wa mchumba ako itakucost ..pia inawezekana kabisa mimba ni ya jamaa ako ila mazingira ya mimba huenda ndio zile mambo ya bahati mbaya kwani sio mwenye mimba basi kapendwa inawezekana mwanamke alitegea mimba ili apendwe na haiwezekani na unapendwa wewe..
Mwisho..tafuta uhakika...na jali mahusiano yenu kwani kama ni kweli yameisha tokea ..mpende be close open na stable muishi wote ili asitoke tena nje au kurudi kwa huyu x..
pole zote ni challenge za mahusiano..hakuna yaliyo smooth kabisa zaidi ya kuvumiliana..
Gluv...gluv100@yahoo.com