Habari za siku nyingi mpenzi msomaji, mchangiaji, mtembeleaji na wewe ulieendelea kunitumia maswali japokuwa sikuwa na muda wa kuyajibu kutokana na sababu nilizozieleza kwa kifupi (kulia hapo kwa juu).
Kwa kawaida blog hii huwa haihusishi masuala yangu binafsi isipokuwa yanayohusu maisha halisi ya kimapenzi ya mtu yeyote, lakini kutokana na nitakachogusia hapo chini, nimeshindwa kujizuia bali kukushirikisha ili utambue kuwa Blog haikunishinda bali nilikuwa nakabiliana na mabadiliko ya Kimwili, Kisaikolojia na kihisia kutoka Dinah kuwa mama kwa mara ya kwanza.
Baada ya safari ndefu ya Ujauzito na mkanganyiko wa Homono zilizonifanya nichukie mambo yote yanayohusisha Teknolojia (ndio maana sikuweza kufanya kazi yangu hapa) yote kwa yote namshukuru Mungu nimejifungua salama mtoto wa Kiume siku chache zilizopita.
Mungu awabariki na awape moyo huo huo wa ushirikiano katika kujaribu kusaidiana ili kuendesha maisha ya amani, furaha na upendo kwenye mahusiano na ndoa.
Asanteni.
Comments
funzadume
Mola ambariki mtoto wenu na watoto wote wa Tanzania. We love you!
Mola ambariki mtoto wenu na watoto wote wa Tanzania. We love you!
Hey FunzaDume kitamboo, Mimi shukrani.
Anony @2:11:00 PM ni kweli kabisa, kuwa mama sio kazi rahisi ila baada ya kumuona mtoto unasahau yote. Mungu awabariki kina mama wote Duniani.
Anony @3:25:00 PM ni Mama Doug (Douglas~Barrack)hehehehe
Anony @2:23:00 PM asante na tubarikiwe sote.
Anony @4:01:00 PM kama umepitia Profile yangu nimehabarisha kuwa mimi ni mke wa mtu, ninakwenda kuongezea kuwa nina mtoto sasa....
'Just kiss him for me...'