Mpenzi atishia kujiua Kisa sms ya Ex akiomba msamaha!-Ushauri

"Kwanza pole na hongera kwa kazi unayofanya ya kutoa ushauri kwa jamii. Mimi ni msichana mwenye miaka 23, nina mpenzi ambaye siku hizi ni kama kafichua makucha vile. Tumekuwa pamoja kwa muda wa mwaka mmoja.

Kilichonifanya niandike leo Dinah, ni huyu mpenzi wangu! mwanzo tulikuwa tunapendana sana na ahadi tele tele, yaani mikwaruzano haikuwepo na muda wote huo hatukuwahi kukosana. Basi siku moja tulikuwa tumekaa sehemu akaniomba nimuhamishie wimbo kutoka kwenye simu yangu kwenda kwenye simu yake.

Kwa utani tu nikamwambia nimeiacha simu nyumbani, jamaa akaja juu kwamba nimemdharau nikamuomba msamaha lakini wapi! akanipokonya simu huku akiuliza "unaficha nini?" Nikamwambia samahani lakini hakukubali na hivyo akachukua simu na akaenda nayo kwake.
Ile simu alikuwa kaninunulia yeye, kwenye simu hiyo kulikuwana sms za x- boyfriend akiniomba msamaha ili turudiane.

Mpenzi wangu akazidi kukasirika na kupandisha sana na akampigia huyo kaka nilieachana nae nakumpandishia aache kunifatilia. Kinachomuuma hasa ni bada ya kugundua kwenye zile sms kuwa Ex wangu anamzidi Elimu kwani kamaliza Chuo Kikuu na pia anamzidi kifedha. Lakini mimi sinampango nae huyo jamaa wala elimu yake wala fedha zake kwani niliisha achana nae na analijua hilo.


Sasa tatizo kubwa hapa ni kuwa mpenzi wangu huyu ananitishia kuwa atajiua na hatanii kweli, ni Mchaga alafu pia nimemzidi kielimu kwani hivi sasa niko Chuo Kikuu mwaka wa pili yeye aliishia Kidato cha 4 na kuanzisha Biashara zake zinazomuingizia hela.

Mimi kuwa Chuo Kikuu ndio limekuwa tusi tukiongea kidogo tyu utasikua "au kwa vile sijasoma najiua ili nikuache huru" Mpenzi wangu anamiaka 25 aliniambia hajawahi kuwa na mwanamke na mimi ni wake wa kwanza.

Dinah najieleza na kuomba kila kukicha na sasa ni miezi 3 imepita lakini msimamo wake ni ule ule wa kujiua, nikamwambia nirudishie simu lakini kila tukipanga kuonana anasema yuko busy. Nikimuomba ninunue simu nyingine hataki, ikabidi nijinunulie mwenyewe simu nyingine kama ile ile ili kuendeleza mawasiliano.

Sasa jamani huyu mwanaume niendelee nae? kama nikiendelea nae na nikajamkosea tena si atajiua!! na nisipoendelea nae na yeye akajiua mimi sinitakuwa matatizoni na Degree yangu ikaishie Segere?
Naomba ushauri kutoka kwa wachangiaji wote".

Comments

Anonymous said…
Nenda karipoti police mapema ili
yakitokea uwe huru usije ukapata matatizo, na mara nyingi ulimi unaumba unachosema ndicho kinachokuwa, kuna rafiki yangu mmoja uk hapa alikuwa na mchumba wake kila siku alikuwa anamwambia nitajiuwa, msichana haikriki, iko siku mwanamme kaenda kujitosa temsmid, baada ya wiki mbili ndiyo mwili umeokotwa umeharibika vibaya, police kuja kwa yule kijana wamekuta kaacha meseji na fist of kin ni mchumba wake kamuandika, ilibidi police wamhoji yule msichana na baada ya kueleza akaambiwa siku nyingine ukiona mtu anasema maneno kama hayo toa ripoti, kwa usalama wako na wake, Kwa hiyo toa ripoti kwa usalama wako na wake. kutosoma yeye sio sababu wanaume wengi wasiosoma ambao hawako understanding wako hivyo kama mtu mnapendana hajalishi elimu,
Anonymous said…
pole sana wandugu, inabidi mjiweke wazi kama uhusiano unawashinda ili kila mtu achukue ustaarabu wake, kujiua mwambie sio issue, zaidi aeleze msimamo wake kwako msipotezeane muda.
gudchaz said…
Pole sana mdogo wangu,kweli huo ni mtihani ....huyo kijana anakupenda kwa dhati sana na suluhisho si kuachana nae kwani tayari ana mapango wa kujidhuru c unajua tena penzi jipya,kiukweli hata mimi mkongwe ningejihisi vibaya kwamba mpenzi wangu amenizidi kielimu haafu nakuta sms za mapenzi na mshikaji wake wa zamani ambaye naye ni msomi kweli inauma....
Tafuta mbinu ya kumthibitishia kuwa unampenda sana yeye na huyo jamaa huna mpango naye,kunua simu tena inayofanana na ile aliyokununulia inaonesha kama umemjibu kwani akijua atajisikia vibaya zaidi...
Jaribu kumfanya ili yeye aonekane ni bora zaidi ya mwengine na pia yeye ni wa thamani zaidi............ila yeye ni mtu mzima haoni kwamba kujiua c suluhisho ni kinyume na sheria yetu ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania
Anonymous said…
loooh,pole sana mdogo wangu,inaonesha hata wewe bado hujakuwa kabisaa. Yaani uolewe na form 4? kisa nini? for what so special;wala usijaribu kuoana na mtu kama huyu,kwanza ni kuwa hawezi kujiua. Mimi ni kati ya walee wa Iringa,kama tukitakaga kujiua hatusemi utakuta mtu kafa tu huyu anapiga mkwara hakuna kitu kama hicho.
Achana nae taaaratiiiiibu,yaani punguza fon calls,sms,even regular meetings ili kuweza kupunguza ile frequent comm then utajichomoa na kutafuta mtu wa caliber yako. Au nikuulize swali,ok mmeoana then one day ikatokea mikwaruzo so atajiua maa ngapi? so make god decision early as possible. Mtu kashaanza kujistukia mapema kuwa unajidai na usomi wako,so how about 20 yrs in merriage?
Regards,
mdau from Pasiansi- MZA
Anonymous said…
Pole sana dada kwa maswahibu yaliyokufika.

Kwa kweli mdogo wangu mwogope sana mtu anayetishia kujiua mara kwa mara, iko siku ataja-jiua kweli. Hata hivyo mdogo wangu msg za Ex wako za nini kuzihifadhi katika simu? Mimi binafsi huwa msg za hivyo hata kusoma huwa sizisomi kabisa, ikiingia tu naidelete mara moja.

Pamoja na hayo huyo jamaa hakufai, kaa chini mweleweshe kwa upendo na mkanye kuhusu kauli yake ya kutaka kujiua kuwa siyo nzuri na huipendi. Kama akiendelea, nakushauri anza kumwacha pole pole kwani utajaitwa mjane kabla hata hujafikisha miaka 30.

Julie
Anonymous said…
Wala hawezi kujiua! Angekuwa wakujiua si hata msiba ungekuwa umeshapita? Miezi 3 yote anaimba kujiua tuu! Nakushauri uachane nae mapema iwezekanavyo. Hamtakuwa na amani katika maisha yenu kwa sababu an inferiority complex kubwa sana! Ataendelea kukutukania elimu yako kila siku. Wala hutaweza ku reason nae huyo. Kila utakachofanya atakihusisha na masuala ya elimu. Mwache mwache mwache haraka iwezekanavyo!
Anonymous said…
Waw! nimeguswa na hii story. pole mdogo wangu wee.... u know wat? me too ni muhanga km ww.

mm nasema jamani hakuna m2 anaesumbua km mpumbavu, ujue hata vitabu vitakatifu vinasema "ghadhabu ya mpumbavu inalemea kuliko gunia la misumari"

1. huyu mkaka hajiamini kabisa, anajifeel infirior coz uko juu kielimu na hivi alivyogundua huyo ex BF nae yuko juu. yani ameathirika kisaikolojia thats y kila anachoongea oooh.. kwa vile umesoma nk.

2. mm siamini km anaweza kujiua, coz anaejiua hasemagi. anakutishia tu. sasa km akiamua kujiua ww utafanyeje? ukweli uko moyoni mwako kama unampenda ama unamcheat.
3. may b utafute mtu mzima amfanyie canseling kdg itamweka sawa.

USHAURI KWA WANAUME KM HUYU

naona km una tatizo na mpenzio ni bora ukafind out how to solve. na siyo kuanza kutishia kujitoa uhai jamani, hiyo cyo solution ila unacriate anaza problem tu.

Its me,

Gg
JIBABA said…
Pole Dada kwa misukosuko iliyokupata.

Umefanya makosa Dada yangu hakuna mtu yeyote ambaye angeridhika na situation aliyoiona HATA WEWE ingetokea kukuta sms za ex wa B4friend wako katika Simu yake ungefurahi? kikubwa cha kufanya kaa nae chini na jaribu kuondoa kasoro zilizopo ikiwemo MKUMWAMBIA UKWELI WOTE KUHUSU EX WAKO kuwa huna mpango nae zaidi ya YEYE KUOMBA MRUDIANE.

Mi naamini MAPENZI YA WAWILI WALIOPENDANA KAMWE HAYAFI hata KAMA YEYE AKIOA NA WEWE KUOLEWA HAPO BAADAYE mara moja, nini cha kufanya:

Ex wako anaonekana kuwa bado ana Mapenzi na wewe na BINAFSI MWANAMKE AMEUMBWA KUWA NA MOYO MWEPESI WA KUSAMEHE hivyo kitendo cha wewe kumkaribisha EX wako na Yeye kuanza kukulilia ni DHAHIRI MOYO WAKO TARATIBU utaanza kuitikia msamaha wae na hatimaye MKARUDIANA KAMA ZAMANI, HIVYO KATIKA HILI CHUNGA SANA KAMA KWELI UNAMPENDA BOYFRIEND WAKO WA SASA NI LAZIMA UKAE MBALI NA HUYO EX LA SIVYO BOYFRIEND WAKO ULIYE NAYE ATAJIUA KIUKWELI (INGAWA INAONEKANA NI KAMA MZAHA FULANI).

Kuhusu tishio la Boyfriend wako kutaka kujiua ni vyema ukeenda kwa ndugu, jamaa na marafiki zake na wazazi kama unatambulika kwao ili ueleze kisa kizima INGAWA UGOMVI WA MAPENZI WASULUHISHI NI NYINYI WENYEWE, lakini mi nathani sauti, maonyo na busara za wazee zinaweza zikamwogopesha.

Ikishindana kote nenda POLISI na utoe taarifa juu ya tishio hilo na hatimaye taratibu za kisheria ziweze kuchukua mkondo wake kwani iwapo BOIFRIEND wako atajiua na kuandika ujumbe kuwa wewe ndiye MHUSIKA KUU, fahamu Ndugu yangu kuwa SHUZI LITAKUNUKA WEWE.

Poa chao!!!!!!!!!!!!!!
JIBABA said…
Pole Dada kwa misukosuko iliyokupata.

Umefanya makosa Dada yangu hakuna mtu yeyote ambaye angeridhika na situation aliyoiona HATA WEWE ingetokea kukuta sms za ex wa B4friend wako katika Simu yake ungefurahi? kikubwa cha kufanya kaa nae chini na jaribu kuondoa kasoro zilizopo ikiwemo MKUMWAMBIA UKWELI WOTE KUHUSU EX WAKO kuwa huna mpango nae zaidi ya YEYE KUOMBA MRUDIANE.

Mi naamini MAPENZI YA WAWILI WALIOPENDANA KAMWE HAYAFI hata KAMA YEYE AKIOA NA WEWE KUOLEWA HAPO BAADAYE mara moja, nini cha kufanya:

Ex wako anaonekana kuwa bado ana Mapenzi na wewe na BINAFSI MWANAMKE AMEUMBWA KUWA NA MOYO MWEPESI WA KUSAMEHE hivyo kitendo cha wewe kumkaribisha EX wako na Yeye kuanza kukulilia ni DHAHIRI MOYO WAKO TARATIBU utaanza kuitikia msamaha wae na hatimaye MKARUDIANA KAMA ZAMANI, HIVYO KATIKA HILI CHUNGA SANA KAMA KWELI UNAMPENDA BOYFRIEND WAKO WA SASA NI LAZIMA UKAE MBALI NA HUYO EX LA SIVYO BOYFRIEND WAKO ULIYE NAYE ATAJIUA KIUKWELI (INGAWA INAONEKANA NI KAMA MZAHA FULANI).

Kuhusu tishio la Boyfriend wako kutaka kujiua ni vyema ukeenda kwa ndugu, jamaa na marafiki zake na wazazi kama unatambulika kwao ili ueleze kisa kizima INGAWA UGOMVI WA MAPENZI WASULUHISHI NI NYINYI WENYEWE, lakini mi nathani sauti, maonyo na busara za wazee zinaweza zikamwogopesha.

Ikishindana kote nenda POLISI na utoe taarifa juu ya tishio hilo na hatimaye taratibu za kisheria ziweze kuchukua mkondo wake kwani iwapo BOIFRIEND wako atajiua na kuandika ujumbe kuwa wewe ndiye MHUSIKA KUU, fahamu Ndugu yangu kuwa SHUZI LITAKUNUKA WEWE.

Poa chao!!!!!!!!!!!!!!
Anonymous said…
hahahah..huyo jamaa kweli zobaa,wee muache tu ana kutisha hawezi kujiuwa.na wewe umetokana wapi na huyo mchanga mshambaa anae taka kujiuwaa.ukiowana nae mdogo wangu ndo itakuwa balaa cse atakuumiza kichwa sanaa
Anonymous said…
Pole sana dada yangu kwa kuwa inaelekea ndio umeingia kwenye sanaa hii ya mapenzi.Hakuna mwanaume hata mmoja katika dunia hii mwenye mipango ya kuoana na mwanamke anayempenda halafu akakubali kushea mapenzi na mwanaume mwingine.Kwa kuwa unampenda mbembeleze asitishe uamuzi wake wa kujiua.Na wewe uwe makini kwa kuwa unaonekana kama huyo wa kwanza hujamuacha kabisa kwa kuwa kama uliingia kwenye mtego mdogo wa kuombwa wimbo ndivyo utakavyoingia kwenye mtego wa kutoa penzi kirahisi ukizingatia kuwa huyo wa kwanza huna cha zaidi cha kumnyima kwa kuwa ulishampa.Acha ajiue kwa kuwa huo ni uamuzi wake ila utafutie ushahidi usije ukahusika kwa njia yoyote ile.
Anonymous said…
Dent wa chuo kikuu,

kwanza pole na kashikashi ya huyo mpenzi wako.

Pili unaelekea ulianza mapenzi mapema mno kiasi kwamba yamekutia upofu kiasi.Kama ungekuwa umekomaa kabisa, hizo sms za huyo X-B/F wako usingezitunza kwenye simu yako kwa sababu ulishaachana naye zinakusaidia nini ukizihifadhi humo? matokeo yake ni hayo sasa hadi mlimbwende wako kazifuma humo.

Kiutaratibu, kama uliachana na mtu si vema kutunza vitu vyake kwa sababu hivyo vitu vitageuka kuwa kishawishi cha kuwa katika mawasiliano naye.Ni dhahiri kwamba wewe uliona fahari unapotumiwa sms na huyo xBF wako pasipo kuangalia shilingi upande wa pili.Ya nini kuayrudia matapishi?

Tatu, kama unasoma chuo kikuu na umeanza kujikita kihivyo katika mapenzi hayo kiasi cha kuanza kukuchanganya hivyo, ni hatari mno, na umri wako bado wamo sana yaani mdogo.

Nne, mimi nipende kukushauri kuwa ni afadhali uachane naye kama atajingonga ni juu yake wala si wewe unayemnyonga.Ila itakuwa mbaya zaidi ukiwa umeolewa naye akajinyonga mkiwa pamoja, na kama hawezi kusamehe kwa jambo dogo hilo, basi sahau kuwa ukiolewa naye atakusamehe.

Mapenzi hayawezi kuwa ya mtelemko siku zote, kuna kupanda milima na kushuka mabonde, yaani vikwazo haviwezi kukosekana, muhimu watu tunadumisha mapenzi kwa sababu tunasameheana. Na hasa jambo dogo kama hilo haliwezi kuwa sababu mtu anatamani hata kujinyonga??? huyo ni hatari hakufai.

Ningekuwa ni mimi hata hizo sms wala nisingejali kwani mtu kuomba msamaha kwa mtu alnayempenda huwezi kumzuia, kasoro yako ni pale umezitunza za nini humo?

Kama pia elimu anaiona kikwazo kwake basi hamuishi mkaishiana kwani hilo litamtesa kila wakati maana ameishajenga inferiority complex tayari.Mkimbie mapema kabla hajatawala milki yako yote potelea mbali amekumega siku zote lakini itoshe hapo.Elimu yako ikukomboe kutafakari aina ya mtu na mapenzi unayotaka kuyafakamamia.
Anonymous said…
Mbwage takusumbua sana huko mbele na hakuna kitu kibaya kuishi na mwanaume mwenye inferiority complex atakutesa kuprove uanaume wake na hivi umesoma utajijutia nafsi yako. Ni bora ukatoe maelezo ya kutishia kujiua kwake Polisi ili siku akiamua kujiua basi uwe una ushahidi na yeye atangulie salama
Anonymous said…
Uyo sio mpenzi nilimbukeni wa mapenzi...achana nae ,kama kujiua kakaa miez yote mi3 anatishia ..angekua wakujiua angesha kufa..na ni mchoyo hana lolote kukunyang'anya hiyo cimu co kwamba nn wala nn kaona nakunulia cmu we unawacliana na wa2 wengine...sasa ckia hakufai na wala ucshughulike nae huyo..maana utamaliza chuo atakunyima kutafuta kazi na atakusimanga na hiyo elimu yako bure mtoto wa wa2 wakati wamekulipia ada wazazi wako...SHOSTIII ACHANA NA LIMBUKENI HUYO
Anonymous said…
oyaaaaaaaa...acheni kuzinguana, kama vipi kila mtu aseme msimamo wake, coz naona mnapotezeana muda, kujiua sio issue mwambie ajikaze atoe msimamo wake.
Anonymous said…
HV JAMANI MIEZI 3 BADO TU UNAHANGAIKA NA MTU? MI KWA MTAZAMAO WANGU NAOAN HUYO MWANAUME HAKUPENDI WALA NINI COZ WHAT I KNOW MAPENZI NI PANDE ZOTE MBILI KILA MTU AMPENDE MWENZAKE, SASA WEWE INAONEKANA WEWE UNAMPENDA ILA YE HAKUPENDI KAMA WEWE,NA MTU AKIKUPENDA KWELI KWELI HUWA NI MUELEWA HARAKA IWAPO MWENZIO KAKUOMBA MSAMAHA UNAKUWA MWEPESI KUSAMEHE NA KUSAHAU THEN MNASONGA MBELE SASA YE KAMA KAKOSA KADOGO KAMA HAKO HAWEZI KUKUSAMEHE JE SIKU UKIKOSEA KABISA ATAKUELEWA? WE KAMA UNA MAISHA YAKO AUA HAYO MASOMO YAKO ENDELEA TU TEMANA NAE UTAPATA TU MWINGINE MA DIA MAPENZI UKIYAELEWA HAYAKUPI SHIDA KABISA, POLE SANA TRY TO TAKE HEART ILA KAMA HAWEZI KUKUELEWA MI NAOAN HAKUFAI
Unknown said…
Jamani Dinah mbona nimetuma comments zangu lakini hazijawa published?
Julie
Anonymous said…
Mh pole sana dada ila ndio maisha yalivyo hawezi kujiua kama mlishakosana ss ni miezi mitatu imeshapita sidhani kama anaweza kufanya kitu kama hicho na je ni binadamu gani huyo asiejua neno msamaha hali hiyo urafiki je ukiingia kwenye ndoa si itakuwa tafrani?jaribu kuwatafuta rafiki zake or km unafahamiana na ndugu zake ili uwaambie na waongee nae.Kwenye mapenzi siku zote hakuna elimu na ingekuwa hivyo basi wale ambao hawajasoma hata nursery wasingeoa wala kuolewa ktk ulimwengu huu wa ss.

Frm Doble HH
Anonymous said…
ACHANA NAYE ENDELEA NA SHULE LA SIVYO HATA WEWE ATAKUUA USIPOKUWA MWANGALIFU!!!!!

YA NINI KUHANGAIKA NA MAPENZI KATIKA GIZA TOTORO NAMNA HIYO?

SMS TU INAMKASIRISHA HATA HAKUBALI KUKUSAMEHE, JE YAKITOKEA MAKUBWA ZAIDI YA HAYO MTAISHIA WAPI?

JIHADHARI KABLA YA HATARI LA SIVYO UTAUMIZWA KWA UPUMBAVU WA MAPENZI YASIYO NA KICHWA WALA MIGUU.

INAELEKEA WEWE BINTI UNAMTEGEMEA SANA HUYO JAMA KUKUPA PESA MAANA UMESEMA LIPOKUNYANG'ANYA SIMU ULIMTAKA AKUNUNULIE TENA NA WAKATI HIYO ALIKUNUNULIA.UNASOMA CHUO KIKUU LAKINI HUELIMIKI BIBIE??
Anonymous said…
Umefika wakati wa wewe kuwa na msimamo,kama uliamua kuachana na huyo x wako,mawasiliano kwenye simu yanatoka wapi tena?na kwanini uendelee kutunza sms zake ilihali ukijua unamtu mwingine unaempenda?
Nachoweza kukushauri dear,tofauti za kielim ni tatzo kubwa ktk mapenz kwa sisi watanzania!hasa mwanaume anapokua chini kuliko mwanamke,anakua hajiamini muda wote!na itakusumbua maisha yako yote!cha kufanya take action,achana nae,tafta mtu atakayekuelewa.Kuhusu hivyo vitisho vya kujiua hana lolote huyo,anakutisha tu!hata akifanya hiyo we huna kosa!
Anonymous said…
Mdogo wangu miezi mitatu yote hajajiua tu? huyo anakutisha tu na mapenzi hayajengwi kwa vitisho achana nae huyo na hata akijiua wewe unahusika vipi? sheria haitakuhusisha mkimbie mapema sipendi watu wanaokagua simu za wapenzi wao.
EDAMO said…
Inaelekea huyo mwanaume amekupenda kwa dhati lakini wewe unamzuga na inawezekana ulipretend kumpenda kwa sababu ya fedha zake ama kutuliza machungu uliyoyapata baada ya kuachana na huyo Ex wako.Kama kweli wewe huna mpango wa kurudiana na huyo Ex kuna sababu gani ya kuendelea kuwasiliana nae hadi kutunza sms zake za kukuomba mrudiane kwa nini usifute sms zake kama kweli huna mpango nae,halafu mpezi wako anakuomba cmu unamnyima alipochukua kwa nguvu ndo anakutana na sms za huyo unayemwita Ex hata ungekuwa wewe ungejua sababu ya kunyimwa cmu ni hiyo sms haikutakiwa uione.Kwa ujumla wewe dada si mwaminifu kwanza ungetueleza sababu ya kuachana na huyo Ex.Halafu unaonekana kumfagilia kuwa amemzidi wa sasa kwa elimu na pesa na wewe vilevile umemzidi.Kwa ujumla wewe unaonekana huna mapenzi ya dhati kwa huyo mwanaume maana usingemnyima simu halafu unatuzuga ulikuwa unamtania,tungekuelewa hivyo sms za huyo ex zisingekutwa kwenye simu yako ni dhahiri kuwa ulikuwa unaogopa kumpa kwa sababu ya hizo sms.Cha msingi muache kijana wa watu ampate mwenye mapenzi ya dhati maana wewe huna msimamo upo kifedha zaidi lakini angalia mwisho wake utakuwa mbaya na utabki kujuta.
Anonymous said…
RUDIANA NAYE WA ZAMANI ACHANENI NA HUYO MLEGEVU ATAKUMALIZA HUYO!!!MAANA UNAONELKANA BADO UNA UTAMU WA XBF WAKO UMEMSIFIA ANA ELIMU NA KIPATO KULIKO WA SASA.KAMA NI HIVYO YA NINI KUGANDA NAYE NA HATIMAYE UKAMSABABISHIA KIFO BILA SABABU YA MSINGI??

TENA UNAZITUNZA SMS ZAKE HIYO INAONYESHA KUWA UNAMINGUANA NAYE HASWA SO ACHA KUMPOTEZEA MUDA HUYO MWENYE BIASHARA ZA REJAREJA NENDA NA HUYO WA BIASHARA YA JUMLA MKATESE HUKO.
Anonymous said…
mhhh achana naye mapemaaaa mtu wa kutishia kujiua atakutesa mapa uzeeni tafuta mbinu hata mkoa hama looo hafai kabsia maana anawivu mbaya sana mtu hajui samahani ni nini? nna wewe chuo usiache soma mwanamke umalize kuna leo na kesho sawa ?
Anonymous said…
Hili ni onyo special kwako dada, wewe upo chuo kikuu unang'ang'ana na wa form four ili iweje? asikusumbue na simu yake apeleke hukooooo anakojua yeye, wewe hapo bado uko kwenye safari ya kuisaka elimu mama na bado hujajua utaishia kwenye masters au Phd sasa ikitokea ukifika huko bado utakuwa na huyo form four yako? nakuuliza! usilogwe, mimi yalinipata makubwa hata zaidi ya haya ya kwako, elimu yangu ya juu nikaolewa na form four yaliyonipata sitasahau, ni Mungu tu. Sitaki na wewe yakupate haya, kwanza anaonekana ni dhaifu na hajiamini, anakutishia atajiua ili usiangalie pembeni kuona mtu wa kukufaaa, akafilie mabali, mchaga mhcaga kitu gani tumeona wazungu na wahindi wakijiua sembuse yeye. tena kaz mwendo kwenye masomo yako achana na huyo chalii ati atajiua, kwa hiyo, akijiua wewe inahu! sana sana msiba utakuwa huko kwao na pengo litabaki huko huko kama ni rombo, kibosho, old moshi, uru, marangu au kirua. Tena nisikusikie tena ukisema ati atajiua, ama! pumbavu zake!
Anonymous said…
kwa kifupi mi nakushauri uachane nae sababu ya tofauti zenu kielimu japo anaonyesha kuwa anakupenda kwa dhati...inaonyesha hajiamini na baadae atakusumbua sana....elimu yako ndo itakua sababu ya kila ugomvi!tafuta mtu anayeendana na wewe kielimu na hata kipato mtaelewana zaidi kuliko huyo.