"Kwanza pole na hongera kwa kazi unayofanya ya kutoa ushauri kwa jamii. Mimi ni msichana mwenye miaka 23, nina mpenzi ambaye siku hizi ni kama kafichua makucha vile. Tumekuwa pamoja kwa muda wa mwaka mmoja.
Kilichonifanya niandike leo Dinah, ni huyu mpenzi wangu! mwanzo tulikuwa tunapendana sana na ahadi tele tele, yaani mikwaruzano haikuwepo na muda wote huo hatukuwahi kukosana. Basi siku moja tulikuwa tumekaa sehemu akaniomba nimuhamishie wimbo kutoka kwenye simu yangu kwenda kwenye simu yake.
Kwa utani tu nikamwambia nimeiacha simu nyumbani, jamaa akaja juu kwamba nimemdharau nikamuomba msamaha lakini wapi! akanipokonya simu huku akiuliza "unaficha nini?" Nikamwambia samahani lakini hakukubali na hivyo akachukua simu na akaenda nayo kwake.
Ile simu alikuwa kaninunulia yeye, kwenye simu hiyo kulikuwana sms za x- boyfriend akiniomba msamaha ili turudiane.
Mpenzi wangu akazidi kukasirika na kupandisha sana na akampigia huyo kaka nilieachana nae nakumpandishia aache kunifatilia. Kinachomuuma hasa ni bada ya kugundua kwenye zile sms kuwa Ex wangu anamzidi Elimu kwani kamaliza Chuo Kikuu na pia anamzidi kifedha. Lakini mimi sinampango nae huyo jamaa wala elimu yake wala fedha zake kwani niliisha achana nae na analijua hilo.
Sasa tatizo kubwa hapa ni kuwa mpenzi wangu huyu ananitishia kuwa atajiua na hatanii kweli, ni Mchaga alafu pia nimemzidi kielimu kwani hivi sasa niko Chuo Kikuu mwaka wa pili yeye aliishia Kidato cha 4 na kuanzisha Biashara zake zinazomuingizia hela.
Mimi kuwa Chuo Kikuu ndio limekuwa tusi tukiongea kidogo tyu utasikua "au kwa vile sijasoma najiua ili nikuache huru" Mpenzi wangu anamiaka 25 aliniambia hajawahi kuwa na mwanamke na mimi ni wake wa kwanza.
Dinah najieleza na kuomba kila kukicha na sasa ni miezi 3 imepita lakini msimamo wake ni ule ule wa kujiua, nikamwambia nirudishie simu lakini kila tukipanga kuonana anasema yuko busy. Nikimuomba ninunue simu nyingine hataki, ikabidi nijinunulie mwenyewe simu nyingine kama ile ile ili kuendeleza mawasiliano.
Sasa jamani huyu mwanaume niendelee nae? kama nikiendelea nae na nikajamkosea tena si atajiua!! na nisipoendelea nae na yeye akajiua mimi sinitakuwa matatizoni na Degree yangu ikaishie Segere?
Naomba ushauri kutoka kwa wachangiaji wote".

Comments
yakitokea uwe huru usije ukapata matatizo, na mara nyingi ulimi unaumba unachosema ndicho kinachokuwa, kuna rafiki yangu mmoja uk hapa alikuwa na mchumba wake kila siku alikuwa anamwambia nitajiuwa, msichana haikriki, iko siku mwanamme kaenda kujitosa temsmid, baada ya wiki mbili ndiyo mwili umeokotwa umeharibika vibaya, police kuja kwa yule kijana wamekuta kaacha meseji na fist of kin ni mchumba wake kamuandika, ilibidi police wamhoji yule msichana na baada ya kueleza akaambiwa siku nyingine ukiona mtu anasema maneno kama hayo toa ripoti, kwa usalama wako na wake, Kwa hiyo toa ripoti kwa usalama wako na wake. kutosoma yeye sio sababu wanaume wengi wasiosoma ambao hawako understanding wako hivyo kama mtu mnapendana hajalishi elimu,
Tafuta mbinu ya kumthibitishia kuwa unampenda sana yeye na huyo jamaa huna mpango naye,kunua simu tena inayofanana na ile aliyokununulia inaonesha kama umemjibu kwani akijua atajisikia vibaya zaidi...
Jaribu kumfanya ili yeye aonekane ni bora zaidi ya mwengine na pia yeye ni wa thamani zaidi............ila yeye ni mtu mzima haoni kwamba kujiua c suluhisho ni kinyume na sheria yetu ya Jamuhuri ya muungano wa Tanzania
Achana nae taaaratiiiiibu,yaani punguza fon calls,sms,even regular meetings ili kuweza kupunguza ile frequent comm then utajichomoa na kutafuta mtu wa caliber yako. Au nikuulize swali,ok mmeoana then one day ikatokea mikwaruzo so atajiua maa ngapi? so make god decision early as possible. Mtu kashaanza kujistukia mapema kuwa unajidai na usomi wako,so how about 20 yrs in merriage?
Regards,
mdau from Pasiansi- MZA
Kwa kweli mdogo wangu mwogope sana mtu anayetishia kujiua mara kwa mara, iko siku ataja-jiua kweli. Hata hivyo mdogo wangu msg za Ex wako za nini kuzihifadhi katika simu? Mimi binafsi huwa msg za hivyo hata kusoma huwa sizisomi kabisa, ikiingia tu naidelete mara moja.
Pamoja na hayo huyo jamaa hakufai, kaa chini mweleweshe kwa upendo na mkanye kuhusu kauli yake ya kutaka kujiua kuwa siyo nzuri na huipendi. Kama akiendelea, nakushauri anza kumwacha pole pole kwani utajaitwa mjane kabla hata hujafikisha miaka 30.
Julie
mm nasema jamani hakuna m2 anaesumbua km mpumbavu, ujue hata vitabu vitakatifu vinasema "ghadhabu ya mpumbavu inalemea kuliko gunia la misumari"
1. huyu mkaka hajiamini kabisa, anajifeel infirior coz uko juu kielimu na hivi alivyogundua huyo ex BF nae yuko juu. yani ameathirika kisaikolojia thats y kila anachoongea oooh.. kwa vile umesoma nk.
2. mm siamini km anaweza kujiua, coz anaejiua hasemagi. anakutishia tu. sasa km akiamua kujiua ww utafanyeje? ukweli uko moyoni mwako kama unampenda ama unamcheat.
3. may b utafute mtu mzima amfanyie canseling kdg itamweka sawa.
USHAURI KWA WANAUME KM HUYU
naona km una tatizo na mpenzio ni bora ukafind out how to solve. na siyo kuanza kutishia kujitoa uhai jamani, hiyo cyo solution ila unacriate anaza problem tu.
Its me,
Gg
Umefanya makosa Dada yangu hakuna mtu yeyote ambaye angeridhika na situation aliyoiona HATA WEWE ingetokea kukuta sms za ex wa B4friend wako katika Simu yake ungefurahi? kikubwa cha kufanya kaa nae chini na jaribu kuondoa kasoro zilizopo ikiwemo MKUMWAMBIA UKWELI WOTE KUHUSU EX WAKO kuwa huna mpango nae zaidi ya YEYE KUOMBA MRUDIANE.
Mi naamini MAPENZI YA WAWILI WALIOPENDANA KAMWE HAYAFI hata KAMA YEYE AKIOA NA WEWE KUOLEWA HAPO BAADAYE mara moja, nini cha kufanya:
Ex wako anaonekana kuwa bado ana Mapenzi na wewe na BINAFSI MWANAMKE AMEUMBWA KUWA NA MOYO MWEPESI WA KUSAMEHE hivyo kitendo cha wewe kumkaribisha EX wako na Yeye kuanza kukulilia ni DHAHIRI MOYO WAKO TARATIBU utaanza kuitikia msamaha wae na hatimaye MKARUDIANA KAMA ZAMANI, HIVYO KATIKA HILI CHUNGA SANA KAMA KWELI UNAMPENDA BOYFRIEND WAKO WA SASA NI LAZIMA UKAE MBALI NA HUYO EX LA SIVYO BOYFRIEND WAKO ULIYE NAYE ATAJIUA KIUKWELI (INGAWA INAONEKANA NI KAMA MZAHA FULANI).
Kuhusu tishio la Boyfriend wako kutaka kujiua ni vyema ukeenda kwa ndugu, jamaa na marafiki zake na wazazi kama unatambulika kwao ili ueleze kisa kizima INGAWA UGOMVI WA MAPENZI WASULUHISHI NI NYINYI WENYEWE, lakini mi nathani sauti, maonyo na busara za wazee zinaweza zikamwogopesha.
Ikishindana kote nenda POLISI na utoe taarifa juu ya tishio hilo na hatimaye taratibu za kisheria ziweze kuchukua mkondo wake kwani iwapo BOIFRIEND wako atajiua na kuandika ujumbe kuwa wewe ndiye MHUSIKA KUU, fahamu Ndugu yangu kuwa SHUZI LITAKUNUKA WEWE.
Poa chao!!!!!!!!!!!!!!

kwanza pole na kashikashi ya huyo mpenzi wako.
Pili unaelekea ulianza mapenzi mapema mno kiasi kwamba yamekutia upofu kiasi.Kama ungekuwa umekomaa kabisa, hizo sms za huyo X-B/F wako usingezitunza kwenye simu yako kwa sababu ulishaachana naye zinakusaidia nini ukizihifadhi humo? matokeo yake ni hayo sasa hadi mlimbwende wako kazifuma humo.
Kiutaratibu, kama uliachana na mtu si vema kutunza vitu vyake kwa sababu hivyo vitu vitageuka kuwa kishawishi cha kuwa katika mawasiliano naye.Ni dhahiri kwamba wewe uliona fahari unapotumiwa sms na huyo xBF wako pasipo kuangalia shilingi upande wa pili.Ya nini kuayrudia matapishi?
Tatu, kama unasoma chuo kikuu na umeanza kujikita kihivyo katika mapenzi hayo kiasi cha kuanza kukuchanganya hivyo, ni hatari mno, na umri wako bado wamo sana yaani mdogo.
Nne, mimi nipende kukushauri kuwa ni afadhali uachane naye kama atajingonga ni juu yake wala si wewe unayemnyonga.Ila itakuwa mbaya zaidi ukiwa umeolewa naye akajinyonga mkiwa pamoja, na kama hawezi kusamehe kwa jambo dogo hilo, basi sahau kuwa ukiolewa naye atakusamehe.
Mapenzi hayawezi kuwa ya mtelemko siku zote, kuna kupanda milima na kushuka mabonde, yaani vikwazo haviwezi kukosekana, muhimu watu tunadumisha mapenzi kwa sababu tunasameheana. Na hasa jambo dogo kama hilo haliwezi kuwa sababu mtu anatamani hata kujinyonga??? huyo ni hatari hakufai.
Ningekuwa ni mimi hata hizo sms wala nisingejali kwani mtu kuomba msamaha kwa mtu alnayempenda huwezi kumzuia, kasoro yako ni pale umezitunza za nini humo?
Kama pia elimu anaiona kikwazo kwake basi hamuishi mkaishiana kwani hilo litamtesa kila wakati maana ameishajenga inferiority complex tayari.Mkimbie mapema kabla hajatawala milki yako yote potelea mbali amekumega siku zote lakini itoshe hapo.Elimu yako ikukomboe kutafakari aina ya mtu na mapenzi unayotaka kuyafakamamia.
Julie
Frm Doble HH
YA NINI KUHANGAIKA NA MAPENZI KATIKA GIZA TOTORO NAMNA HIYO?
SMS TU INAMKASIRISHA HATA HAKUBALI KUKUSAMEHE, JE YAKITOKEA MAKUBWA ZAIDI YA HAYO MTAISHIA WAPI?
JIHADHARI KABLA YA HATARI LA SIVYO UTAUMIZWA KWA UPUMBAVU WA MAPENZI YASIYO NA KICHWA WALA MIGUU.
INAELEKEA WEWE BINTI UNAMTEGEMEA SANA HUYO JAMA KUKUPA PESA MAANA UMESEMA LIPOKUNYANG'ANYA SIMU ULIMTAKA AKUNUNULIE TENA NA WAKATI HIYO ALIKUNUNULIA.UNASOMA CHUO KIKUU LAKINI HUELIMIKI BIBIE??
Nachoweza kukushauri dear,tofauti za kielim ni tatzo kubwa ktk mapenz kwa sisi watanzania!hasa mwanaume anapokua chini kuliko mwanamke,anakua hajiamini muda wote!na itakusumbua maisha yako yote!cha kufanya take action,achana nae,tafta mtu atakayekuelewa.Kuhusu hivyo vitisho vya kujiua hana lolote huyo,anakutisha tu!hata akifanya hiyo we huna kosa!
TENA UNAZITUNZA SMS ZAKE HIYO INAONYESHA KUWA UNAMINGUANA NAYE HASWA SO ACHA KUMPOTEZEA MUDA HUYO MWENYE BIASHARA ZA REJAREJA NENDA NA HUYO WA BIASHARA YA JUMLA MKATESE HUKO.