"Dada Dinah ur a great hero in all about sex education and health in general, Kwa kweli mimi nataka kukuuliza hili kuhusiana na huyu girlfriend wangu niliye naye. Ni kweli nampenda na nilianza naye akiwa bikira kiasi nimeamua kama mungu akipenda tuoane naye na nimeanza kumtambulisha kwa baadhi ya ndugu zangu.
Dada dinah nisaidie mwenzio cz huyu girlfriend wangu ana tatizo la kuruka hedhi zake ila ya mwisho imeniacha na mawazo mengi mpaka sasa maana siku ya mwisho amepata period ni mwezi wa saba mwaka huu mpaka sasa tumesubiria lakini hatujaona dalili zozote naogapa mpaka nikampeleka mwenyewe kupima mimba lakini hamna maana nilihofu ana mimba lakini wapi.
Sasa nikamshauri aende kwa Daktari anasema amemuulizia rafiki yake amemwambia huwa inatokea kutokana na mabadiliko ya hali ya hewa stress na n.k lakini naona imezidi na ananipa wakati mgumu kwani sijui ni kwa nini iwe ivyo maana nataka kumuoa ila kama ndo ivi tutaweza kupata mtoto kama mungu atatusaidia kuoana naye? Naomba msaada wako wa kina dada pls tusaidie wana jamii.
Mdau, Kahama. "
Jawabu: Kukosa hedhi kunaweza kusababishwa na vitu mbalimbali pamoja na hali ya hewa ambayo inaweza kuhoroganya/kanganya Homono, mahangaiko ya akili yanayosababishwa na maisha(stress) pia inaweza kusababisha mwanamke kukosa hedhi.
Ni kweli kabisa kuwa "stress" na hali ya hewa inaweza kuwa sababu. Kama mpenzi wako amehamia huko mliko hivi sasa for the past 12months basi mmpe muda ili mwili wake uzoee.
Ikiwa mpenzi wako anatumia madawa ya kuzuia mimba hakika anaweza kuwa anaruka sana siku zake, kuna baadhi hupata Hedhi mara tatu kwa mwaka, wengine mara nne nakadhalika inategemea aina gani ya kinga ya mimba unatumia.
Kwa vile mpenzi wako anapata damu yake mara fulani fulani sio kwamba anakosa kabisa ana kwa mwaka anakwenda mara tatu basi sidhani kama anaweza kupata matatizo ya kushikamimba ya hatimae kujifungua.
Suala muhimu kwake na kwako wewe ni kufuatilia terehe zake kila mwenzi hasa miezi ile ambayo anaona damu yake(hedhi). Mtakapo funga ndoa na mkaamua kuwa ni wakati muafaka wa kujaribu kwa ajili ya mtoto (kushika mimba) basi mfanye hivyo kwenye zile siku ambazo yai liko tayari kurutubishwa yaani limepevuka na linasubiri kushuka.
Ili kujua siku hizo mpenzi wako anaweza akatumia kalenda(tarehe) na vilevile anaweza kutumia njia za kiasili kama vile kuangalia na kufuatilia mabadiliko ya mwili wake.
Nitakueleza mabadiliko hayo ya mwili mara baada ya masaa machache.....
Bofya hapa kusoma maelezo ambayo ni majibu ya swali kuhusu kuruka hedhi

Comments
gynae=daktari bingwa wa magonjwa ya kina mama. asante sana
ni mimi mdau namba moja wa dada dina,
shaister!
Ni kawaida kwa mwanamke kupita hedhi sometimes, ingawa kuna wakati inaweza kuwa mayai hayapevuki vema, isikutishe, ni kweli stress na hali ya hewa inaweza kumfanya mwanamke kutooana siku zake,
Mshauri akamuone Dr wa kina mama atmpa dawa zitamsaidia.Pia anaweza kupata mimba akiwa hapati siku kwani hata mie imenitokea mara mbili.Ondoa shaka
Mama Perlyn
inavyoonekana Girlfriend wako anatumia pills or contacentive.
au inawezekana alitumia,hizo zinasababisha kabisa kuruka period,either sindano,etc..
jingine ,kuhusu kuzaa hilo haina tatizo,antaweza kuzaa,ila itabidi aache hizo contraceptive,mm nilikaa mwaka mzima bila period,next nilianza morning sickness,na result ikawa positve -preg.
wala usiwe na wasiwasi,mpeleke kwa gyno.mzuri,atamwanzishia dawa na pperiod itarudi kama kawaida,unless kama ana matatizo makubwa ,or kwao kuna matatizo kama hayo.
thanks.
Ushauri wangu tu ni kwamba usimwaache kabisa kwa sababu ana afya ya kutosha kukuzalia mtoto.Kuchelewa au kuruka si hoja.ila ungesema haingii kabisa mwezini,hilo lingekuwa jambo lingine, lakini hilo it is not major case, it can be solved and something can be worked out. So please commit yourself to help your partner in side down.Got it?
Kwanza umesema wewe ndiye ulimbikiri, halafu una wasiwasi na kuruka hedhi!!! Acha ufisadi huo!!!Jengana na mwenzio mfikie hatua ya mwisho ya kuoana.
Hata mimi nakushauri usiwe na wasiwasi huyo bikira wako ni buheri wa afya kabisaa na atakuzalia malkia wako vizuri ila fuata ushauri uliopewa na wadau hapo juu.
Nikaja kuolewa na hedhi yangu ikaondoka kwa mwaka mmoja, nilikuwa nakwenda kuona doctor tofauti hakuna aliye weza kunisaidia. Na nipo hapa America toka mwaka 2000 na kilicho nisaidia ni dawa za miti shamba ambazo nilipewa na kijana mmoja kutoka Nigeria. Baada ya kuinywa ile dawa kwa mwezi mmoja tu, na mimba nikapata na sasa nina watoto 3.
Ninacho taka nikuambie ni kwamba, atajapa hedhi yake tu, kwani haijapita hata mwaka, ni vijimiezi tu. Na kuzaa, atazaa tu, hilo tumuachie Mola mwenyewe. Kupata watoto ni majaaliwa ya Mw/mungu.
Kumbuka siku hizi kuna magonjwa mengi duniani. Nakushauri kaa naye msichana wako, na pia mkafunga ndoa paoja itakuwa jambo la Kheri na mkajaaliwa kuwapata watoto machapa. Nakuomba msitumie dawa kwa sasa. Na kama mtajaribu dawa bora dawa za miti shamba, na wamasai ndiyo waokozi wakubwa tu.
Nakutakia kila la kheri na dua zangu zitawafikia, na muyapangayo Mola atayafungulia njia. Inshaallah.
thanx so much wanajamii wenzangu,If God wish all our dreams come true.
Mwanajamii, kahama.