"Hongera kwa kutupatia mavitu motomoto,me ni mdau wako mkubwa,da dinah naomba unisaidie kwa hili; nimeolewa miaka 5 iliyopita na sijapata mtoto mpaka sasa na tatizo langu kubwa ni hedhi yaani kupata kwangu hedhi si kila mwezi.
Naweza pata mwezi huu na unaofuata nisipate hata miezi 2 au 3. Nilikosa hedhi kwa muda wa miezi 5 nyuma na nimepata mwezi huu nimeanza period tarehe 13/8/2008 hadi tarehe 8/10/2008 ndio nimemaliza na hitaji nibebe mimba hasa kwa mwezi huu.
Nimkumbushe vizuri tarehe za upevushaji ili ni-do na niweze kupata ujauzito.Yaani nina hamu kweli na mtoto mwenzio!
Asante. Mdau!"
Jawabu: Asante, Sasa Mdau umenichanganya kidogo hapa, inamaana umekuwa hedhini kwa takribani mwezi na nusu? Alafu unapokaribia hedhi huwa unahisi dalili zozote kuwa sasa unakaribia au inaibuka tu bila taarifa?....nisaidie nili nikusaidie kiuhakika zaidi.
Kabla sijakujibu (nasubiri ufafanuzi wako) ni vema basi ukaelewa suala zima la mzunguuko wako wa hedhi kwani kwa baadhi ya wanawake huwa wanachanganya mzunguuko huu wakidhani kuwa kila mwezi lazima apate hedhi ktk tarehe zile zile lakini ukweli ni kuwa tarehe kuwa hazijirudii kila unapokuwa hedhini inaweza ikawa siku nne kabla ya tarehe ya mwezi uliopita au siku saba mbele ya tarehe uliyopata hedhi mwezi uliopita.(inategemea zaidi na urefu wa mzunguuko wako wa hedhi).
Mzunguuko wa kawaida unachukua siku 24 mpaka 35, kwa maana kuwa mzunguuko mrefu ni siku 35 na mfupi ni siku 24 japokuwa wengi wanakwenda mzunguuko wa siku 28 tu bila kubadilika.
Mzunguuko huu unaweza ukaanzia tarehe 10th na kuendelea kuzunguuka na siku moja utajikuta unapata hedhi yako tarehe 31st Sept ambayo ni sawa na mwenzi mpya (yaani October) si ndio alafu usipoata hedhi mwezi mwezi wa kumi labda tarehe 28th kwako wewe unaweza kudhani kuwa umepata hedhi mara mbili ktk mwezi mmoja.......lakini katika hali halisi ya mzunguuko wako ni kwamba umepata hedhi miezi miwili tofauti kwani kinachohesabiwa ni ile siku ya kwanza ya kuona damu ambayo ni 31st na sio tarehe 1st ya mwezi uliofuata......sijui umenielewa hapo?
Kwa baadhi ya wanawake hasa wale ambao wanatumia madawa ya kuzuia mimba kuruka hedhi inaweza ikawa kawaida, pia wale ambao ndio kwanza wamevunja ungo pia inaweza kuwa ni kawaida bila kusahau kwa wale wenye matatizo fulani ya kiafya (kama kisukari, matatizo ya figo,au wapenzi wa ku "Diet" inayokunyima virutubisho muhimu unaweza kuruka hedhi.
Kuruka hedhi inaweza isiwe tatizo unapotaka kushika mimba/kumibika kama utajua dalili za yai lako kupevuka (kuwa tayari kurutubishwa) ila utahitaji kujega tabia ya kuhesabu siku zako na vilevile kusoma na kutambua mabadikiko ya mwili wako hasa maeneo nyeti nikiwa na maana uke.
Kuruka hedhi sio tatizo kubwa sana kama wewe unaafya njema na mara kwa mara yai linashuka kwa maana unapata hedhi hivyo uwezekano wa kukamata/shika/mimbika upo, ila utakachopaswa kukifanya ni kuwa mwepesi kugundua mabadiliko ya mwili wako ili uweze kujua kama yai limepevuka na linahitaji kurutubishwa na hapo ndio ufanye mapenzi na mumeo....nitakueleza mabadiliko gani ya mwili wako uyafuatilie jinsi ninavyoendelea.....
Pamoja na kusema hivyo kuruka hedhi huko kunaweza kuwa tatizo ikiwa tu umri wako ni mkubwa, kwani jinsi unavyokua uwezo wako na upevukaji wa mayai yako hupungua, uwezo wako kunyevuka(nyegeka) wakati wa kufanya mapenzi ili kurahisisha "usafiri" wa mbegu za kiume kwenda kuungana na yai lako lililopevuka, vilevile kama huna matatizo ya mirija ya "felopian".
Unaweza kutumia njia asilia (nitakuelekeza ukinipa ufafanuzi) ili kushika mimba au unaweza kwenda kumuona Daktari kwa ushauri zaidi na matibabu, mara nyingi wanakufanyia uchunguzi alafu kama huna matatizo mengine basi wanakupatia vidonge ambavyo vitasaidia na kuongeza muda wa upevukaji wa mayai yako kila hedhi inapokaribia.Nikija nitakupa maelezo ya mabadiliko ya mwili wako ambayo yatakusaidia wewe kujua kama uko tayari kumimbwa.
.......mida mida basi.

Comments
mama Taty
Mungu yupo na ndio anawawezesha madaktari kuweza kuperform wonders.
Hivyo fuata ushauri hapo juu,nenda kwa matatibu fuata ushauri wao mwisho wa siku utakubali Mungu ni mkubwa na aweza yote.
Dinah ..kazi nzuri..siku njema
Serikali, naomba umpigie sema nimepewa namba yako na mtu aliyepata matibabu toka kwako, maelezo mengine atakupa yy ila sharti la kwanza lazima uende na mumeo au mpenzi wako ili awaangalie wote kwa pamoja, tiba yake ni ya kizungu sio kienyeji. wapo watu wengi wamepata watoto nawajua kupitia yy na wengine wanatoka hadi nje ya tanzania wamekwenda kwake wakafanikiwa, hii ni kwa wanawake wote ambao wanatatizo km lako nawaomba mtafutini huyu mama