Dinah habari yako nina swali nataka kujua. Mimi ni msichana nina bf tunapendana ,ila shida yangu ni hii bf wangu ni mrefu kuliko mimi. Siku moja mama yake akamwambia "unataka kuoa mbilikimo" halafu nilisikia, nilijsikia viabaya sana mpaka leo nikikumbuka ile sentensi huwa nakuwa na hasira sana.
Je niendelee kuwa naye na nivumilie "unyanyapaaji" wa ndugu zake hasa dada zake wanavyosema mimi ni mfupi au nianze zangu nikatafute mtu ambaye atanipenda na familia yake haitaniona tofauti hasa kimaumbile? Maana hata bf hapendi tuongozane maana anasema naonekana kama mtoto wake. ???
Je niendelee kuwa naye na nivumilie "unyanyapaaji" wa ndugu zake hasa dada zake wanavyosema mimi ni mfupi au nianze zangu nikatafute mtu ambaye atanipenda na familia yake haitaniona tofauti hasa kimaumbile? Maana hata bf hapendi tuongozane maana anasema naonekana kama mtoto wake. ???
Comments
Kwanza kabisa ushauri wangu wangu ninao kupa si lazima uufwate kwani ni mtazamo wangu mimi binafsi kama brayan.
Jinsi inavyoonekana toka mwanzo wa mapenzi yenu jamaa alikutamani na hakukupenda kwani mtu ukipenda kasoro za mtu zote huzioni na utajiskia furaha kuwa nae na kumwonyesha kwa kila mtu,sasa kama jamaa hata kutembea na wewe hataki basi ni kwamba yuko na wewe kwa sasa kama mazoea tuu labda anaogopa kukwambia ukweli kuwa hakufill tena kwani utajiskia vibaya na kuumia sana,kwakua naamini hakuna mtu anae mpenda girl friend wake halafu hawezi kutembea nae?there is no true love there???
Sasa itakuwaje kama ndio akiwa mumeo je hamtapata muda wa kutoka pamoja au itakuwaje hiyo??
Pili natumaini uhusiano wenu ulikuwa unalenga pazuri kama vile kuwa mume na mke sasa kama hilo ndio lengo na umesema upande wa familia mama hakupendi anakudharau si jambo jema kabisa kwenda huko kwani utakuwa umejiongezea matatizo katika maisha yako ya kuishi bila raha wala amani while naamini wewe ni mrembo tuu unaweza kupata mwanaume atakaye kuthamini na familia yake pia kukuheshimu kama mtoto wao pia.
Sijajua umri wako ila ushauri wangu kwako ni kwamba wewe take you time najua utaumia sana mwanzoni kwakuwa ulikuwa unampenda ila take it easy kwani maisha yana challenge nyingi kubwa hata zaidi ya hizo so mysister mwache huyo hakufai thanks.
Everything happens for a reason nothing happens by chance or by good luck,
BRAYAN
me nakushuri dada kaa chini jifikirie unajisikiaje then fanya maamuzi kufuatana na da way u feel mkiwa nae
mapenzi ni kukupenda jinsi ulivyo sio kukutoa kasoro otherwise hii is not there for you
thanx
Mungu akutangulie kwenye maamuzi yako
So Sis kwa hali hiyo basi kama ningelikuwa mimi na kwa maamuzi ya haraka although yanaumiza kwa kuamua kumuacha huyo jamaa kwa maana mapenzi yenu hata mkiendelea hayana maisha malefu na hata kama yatakuwa na maisha malefu basi kwako wewe itakuwa ni mateso, itaonekana kuwa wewe unajipendekeza kwa familia yao na hata wakati mwingine jamaa akionesha kukupenda kwa dhati ukasemekana kuwa umemuendea kwa karumamnzira kumchanganya ndugu yao. Nikirudia maneno ya jay jay hapo juu kuwa madada zetu wafupi mmebalikiwa radha iliyo ya hali ya juu katika suala zima la mapenzi, basi hata huyo jamaa yako kwa kufuata hiyo radha itakayomchanganya na kuto banduka kwako.
But all in all kwa heshima, raha na furaha ya maisha yako ni vema ukaangalia yule (wale) watakao kujali kama mwanadamu na sio wanyanyapaaji. Kuwamakini katika maamuzi yako!!!
Mapenzi hayakupaswa kua machungu....
Unju-bin-Unuki ni jitu la kale linaelezewa lilikuwa refu kupindukia kiasi na kutokana na urefu wake alionekana kuwa hana akili! Nadhani Unju-bin-Unuki wa hadithini ndiye huyo anayejidai kuwa eti ni mpenzi wako lakini hawezi kutembea na wewe eti kwa vile wewe ni mfupi!! Ni Unju-bin-Unuki tu huyo!
Hakuna aliyeweza kutoa hoja, kwasababu mapenzi kwa ujumla hayajali rika, umbile au rangi. Mapenzi ni hisia inayojijenga toka ndani, na nje ni kama vipambizo tu.
Sasa ndugu yanguee, watu wanakunyanyapaa kwasababu ya umbile lako, hawajui huyu akisema napenda hiki yule anasema anapenda kile ndivyo mapenzi yalivyo.
Sisemi moja kwa moja kuwa jamaa yako hakupendi, huenda anakupenda ila `hajiamini' na kutojiamini katika jambo lolote ni kasoro.
Na kumbuka mapenzi ni kati yako wewe na yeye, wengine ni washabiki tu, kwahiyo huo mpira unatakiwa uucheze wewe na mwenzako. Wanandugu , wazazi watanyamaza kama nyie mtafunga magoli. Na goli ninalolizungumzia mimi ni nyie kuwa wapenzi wa kikwelikweli kama mumeshajiandaa(mume na mke).
Kwa ushauri wangu, mpe mwezako muda huku ukumuonyesha mapenzi ya nzati(sio ngono, kwani wengine wataniuliza m3 ulishasema ngono ifanyike ndani ya ndoa mbona unamshauri mwenzako vinginevyo. Jenga tabia njema kwa hao nduguzako bila kujali wasemavyo nk. Baada ya muda fulani muulize nini hatima yenu. Swali kubwa ni je wewe unanipendea nini? unanipenda mimi au unapenda kitu gani kwangu? Na la mwisho ambalo linatakiwa liwe la mwisho ni je upo tayari kuishi na mimi kama mke na mume?
Najua majibu ya wanaume ni ya `kisiasa zaidi' atakuambia anakupenda vyovyote ulivyo. Sasa akikujibu hivyo kama ingelikuwa mimi ningemuambia atangaze ndoa. Wengi ambao ni `wanasiasa wa mapenzi' wakifika hapa hushikwa na kigugumizi, `unajua ngoja kwanza kieleweke...' Hapo kama kweli unampenda weka msimamo, kuwa hakieleweki kitu mpaka angalao `uchumba uwepo'.
Hayo ndiyo yangu
emu-three
Nilikuwa busy malishoni na kupika pika..aaa aaa
Nikija kwenye mada ya leo.
Kwanza pole sana kwa wewe dada yalikusibu.
Familia ya mpenzi yako inaweza kuwa na sehemu kwenye mahusiano yenu ila sio ndani kiasi hicho.
Na kama mwenza wako angesimama upande wako ningekwambia kanyaga twende.Ila kwa hali ilivyo...
Wao WAMEMWAGA "ugali" wewe MWAGA "mboga" yaani tangaza njaa.
Namaanisha wewe sepa tu Mungu atakusaidia utakutana na atakaye kupenda na kimo chako.Huyo sio wako.Najua mwanzo itakuumiza lakini amini ni kifo tu ambacho hakizoeleki mengine yote yatanazoelekea baada ya muda.
Dinah tupo pamoja kila siku ..sema muda wa kuachia vijineno wakati mwingine unagomba...aaa aaa
siku njema