Ufupi wangu unaudhi ndugu zake-Ushauri

Dinah habari yako nina swali nataka kujua. Mimi ni msichana nina bf tunapendana ,ila shida yangu ni hii bf wangu ni mrefu kuliko mimi. Siku moja mama yake akamwambia "unataka kuoa mbilikimo" halafu nilisikia, nilijsikia viabaya sana mpaka leo nikikumbuka ile sentensi huwa nakuwa na hasira sana.

Je niendelee kuwa naye na nivumilie "unyanyapaaji" wa ndugu zake hasa dada zake wanavyosema mimi ni mfupi au nianze zangu nikatafute mtu ambaye atanipenda na familia yake haitaniona tofauti hasa kimaumbile? Maana hata bf hapendi tuongozane maana anasema naonekana kama mtoto wake. ???

Comments

Anonymous said…
Mh kama mpenzi wako angekuwa anakusupport ningesema endelea nae na usijali watu wengine kwani hawahusiki kwenye mapenzi yenu lakini kama mpenzi wako hanasupport kwako anadiliki hadi kukataa kutoka na wewe kwa vile mfupi hakufai huyo. Kwanza hakukuona kama ulikuwa mfupi alipokutokea mwanzo? Na kama alikutaka kimapenzi ni dhahuli kuna kutoka na kuambatana pamoja sasa iweje sasa akuone wewe kama mtoto wake? Tafuta ustaarabu mwingine kwani wewe hukuomba kuwa mfupi na yeye hakuchagua kuwa mrefu yote ni mapenzi ya mungu, anakutumia tu huyo.
Anonymous said…
Wanawake wafupi ni watamu hivyo jamaa atakuwa na wewe kwa ajiliz a kimwili zaidi na sio lingine, toka nduki dada.
Anonymous said…
dada pole sana,kwanza Hivyo ulivyo ni Mungu ndio amekuumba,hawo wanaokunyanyapa sio sawa kabisa,dada yangu,hapo jiondoe kabisa,huo ni mwanzo tu wameanza hivyo,hata kama ukivumilia bado wataendelea tu kukusema,na inavyoonyesha huyo mwanaume anataka akutumie tu,chunguza mwenyewe kuna jambo unamsaidia ndio maana,or kuna vitu na yeye anamatatizo nayo,wewe anza maisha upya utapata mtu atakayekupenda na familia yake,na umushirikishe Mungu sana.
BRAYAN said…
Pole sana dada yangu i can fill jinsi unavyoumia kwa ajili ya maumbile yako ambayo hayana kasoro yoyote bali ni mtazamo tuu wa watu unatofautiana,
Kwanza kabisa ushauri wangu wangu ninao kupa si lazima uufwate kwani ni mtazamo wangu mimi binafsi kama brayan.
Jinsi inavyoonekana toka mwanzo wa mapenzi yenu jamaa alikutamani na hakukupenda kwani mtu ukipenda kasoro za mtu zote huzioni na utajiskia furaha kuwa nae na kumwonyesha kwa kila mtu,sasa kama jamaa hata kutembea na wewe hataki basi ni kwamba yuko na wewe kwa sasa kama mazoea tuu labda anaogopa kukwambia ukweli kuwa hakufill tena kwani utajiskia vibaya na kuumia sana,kwakua naamini hakuna mtu anae mpenda girl friend wake halafu hawezi kutembea nae?there is no true love there???
Sasa itakuwaje kama ndio akiwa mumeo je hamtapata muda wa kutoka pamoja au itakuwaje hiyo??
Pili natumaini uhusiano wenu ulikuwa unalenga pazuri kama vile kuwa mume na mke sasa kama hilo ndio lengo na umesema upande wa familia mama hakupendi anakudharau si jambo jema kabisa kwenda huko kwani utakuwa umejiongezea matatizo katika maisha yako ya kuishi bila raha wala amani while naamini wewe ni mrembo tuu unaweza kupata mwanaume atakaye kuthamini na familia yake pia kukuheshimu kama mtoto wao pia.
Sijajua umri wako ila ushauri wangu kwako ni kwamba wewe take you time najua utaumia sana mwanzoni kwakuwa ulikuwa unampenda ila take it easy kwani maisha yana challenge nyingi kubwa hata zaidi ya hizo so mysister mwache huyo hakufai thanks.

Everything happens for a reason nothing happens by chance or by good luck,
BRAYAN
Anonymous said…
me naona huyo anataka akutumie tu kwani hata me na bf wangu tunatofautiana sana kwani yeye ana urefu wa183cm name nina 153cm ila jinsi anavyonijali kiasi kwamba ile tofauti ya ufupi siioni na hata nikitaka kuvaa viatu virefu sometimes huwa ananidiscourage na kusema no i want to see you in your natural way and not in an artificial way so najisikia name ni mrefu coz of him
me nakushuri dada kaa chini jifikirie unajisikiaje then fanya maamuzi kufuatana na da way u feel mkiwa nae
mapenzi ni kukupenda jinsi ulivyo sio kukutoa kasoro otherwise hii is not there for you
thanx
Mungu akutangulie kwenye maamuzi yako
Anonymous said…
hello baby girl pole sana kwa kwa yaliyokukuta, unajua mapenzi huwa hayachagui namna ya mtu alivyoumbwa na mungu na kitu ambacho watu wengi wanakosea kwenye mahusiano ni kumropokea mpenzi wako kuhusu mapungufu yake au kasoro ambazo ni za kuzaliwa nazo watu wa namna hii huwa wanaleta misuko suko sana kwenye mahusiano, na kama huyo bf wako mwenyewe haoneshi ushirikiano inamaana hana mpango wowote na wewe ndio maana hajali kukuumiza moyo wako kwa kukuambia kasoro ambayo mungu amekupa wakati huenda na yeye anazo kasoro zake pia, nakushauri mdogo wangu endelea na maisha yako hamna future hapo mungu atakupa atakae kupenda kwa hali yoyote kaza buti fanya mambo yako mengine ya maana ok.
Anonymous said…
POle kwa Unyanyaapaliwa, Sis mapenzi ni wawili wapendanao. Sasa basi kama ni kama unaamini unampenda huyo jamaa yako na huku alisha kuambia hawezi kutembea na wewe, kama ni mimi ndio wewe kwanza ningemuuliza ana mpango gani na mimi (wewe) kuchezeana tu au kuwa mama wa watoto wake maishani!!! If kuwa maishani nami anauchukuliaje usemi wa mama yake ambao wewe uliusikia mwenyewe jinsi anavyo kunyanyapaa na hata dada zake wakusemavyo!! Then wewe hapo ndio utajua lakufanya kwani asikudanganye mtu Sis kuwa mwaweza pendana wenyewe wawili na mkaanza maisha yenu vema lakini kwa chuki na unyanyapaa ulijijenga baina yako na upande wa familia ya jamaa wako mkashindwa kuendelea kuishi pamoja na hata kama mtaishi pamoja lakini si kwa amani kama kukiwa hakuna unyanyapaa baina yenu kwa upande mwingine wowote wa familia zenu.

So Sis kwa hali hiyo basi kama ningelikuwa mimi na kwa maamuzi ya haraka although yanaumiza kwa kuamua kumuacha huyo jamaa kwa maana mapenzi yenu hata mkiendelea hayana maisha malefu na hata kama yatakuwa na maisha malefu basi kwako wewe itakuwa ni mateso, itaonekana kuwa wewe unajipendekeza kwa familia yao na hata wakati mwingine jamaa akionesha kukupenda kwa dhati ukasemekana kuwa umemuendea kwa karumamnzira kumchanganya ndugu yao. Nikirudia maneno ya jay jay hapo juu kuwa madada zetu wafupi mmebalikiwa radha iliyo ya hali ya juu katika suala zima la mapenzi, basi hata huyo jamaa yako kwa kufuata hiyo radha itakayomchanganya na kuto banduka kwako.

But all in all kwa heshima, raha na furaha ya maisha yako ni vema ukaangalia yule (wale) watakao kujali kama mwanadamu na sio wanyanyapaaji. Kuwamakini katika maamuzi yako!!!
Kapongola said…
Mapenzi yanapaswa kua baina yenu nyie wawil pasi kuangalia watu wa pembeni wanasemaje. Kaa na mpenzi wako muulize kwanini hapendi kuongozana nawe. Kama atakuambia hapendi kuongozana nawe kwa ajili ya ufupi wako, unahitaji kufikiri mara mbili, kwani hakuliona hilo tangu mwanzo?

Mapenzi hayakupaswa kua machungu....
Anonymous said…
Dada achana na huyu msanii. Huyo hana mapenzi na wewe maana jicho la mapenzi haliwezi kuona kimo kuwa ni tatizo. Hivi alikuona lini?!! Ni hivi sasa tu?!!!! Huyo ni muwongo, laghai, dhaifu na hakustahili hata kidogo. Achana naye na mwambie sababu ni ile ile anayoiona yeye, kwako. Nayo ni kwamba na wewe hupendi kutembea na mtu anayeonekana kama Unju-bin-Unuki!!!!

Unju-bin-Unuki ni jitu la kale linaelezewa lilikuwa refu kupindukia kiasi na kutokana na urefu wake alionekana kuwa hana akili! Nadhani Unju-bin-Unuki wa hadithini ndiye huyo anayejidai kuwa eti ni mpenzi wako lakini hawezi kutembea na wewe eti kwa vile wewe ni mfupi!! Ni Unju-bin-Unuki tu huyo!
Anonymous said…
Hii hoja ya maumbile na mapenzi niliidodosa-dodosa kipindi fulani kuwa maumbile ya mtu yana athari gani katika `ngono' au mapenzi kwa ujumla. Kwa mfano kwanini `warembo wanatajishwa kwa umbile fulani?'

Hakuna aliyeweza kutoa hoja, kwasababu mapenzi kwa ujumla hayajali rika, umbile au rangi. Mapenzi ni hisia inayojijenga toka ndani, na nje ni kama vipambizo tu.

Sasa ndugu yanguee, watu wanakunyanyapaa kwasababu ya umbile lako, hawajui huyu akisema napenda hiki yule anasema anapenda kile ndivyo mapenzi yalivyo.
Sisemi moja kwa moja kuwa jamaa yako hakupendi, huenda anakupenda ila `hajiamini' na kutojiamini katika jambo lolote ni kasoro.
Na kumbuka mapenzi ni kati yako wewe na yeye, wengine ni washabiki tu, kwahiyo huo mpira unatakiwa uucheze wewe na mwenzako. Wanandugu , wazazi watanyamaza kama nyie mtafunga magoli. Na goli ninalolizungumzia mimi ni nyie kuwa wapenzi wa kikwelikweli kama mumeshajiandaa(mume na mke).

Kwa ushauri wangu, mpe mwezako muda huku ukumuonyesha mapenzi ya nzati(sio ngono, kwani wengine wataniuliza m3 ulishasema ngono ifanyike ndani ya ndoa mbona unamshauri mwenzako vinginevyo. Jenga tabia njema kwa hao nduguzako bila kujali wasemavyo nk. Baada ya muda fulani muulize nini hatima yenu. Swali kubwa ni je wewe unanipendea nini? unanipenda mimi au unapenda kitu gani kwangu? Na la mwisho ambalo linatakiwa liwe la mwisho ni je upo tayari kuishi na mimi kama mke na mume?

Najua majibu ya wanaume ni ya `kisiasa zaidi' atakuambia anakupenda vyovyote ulivyo. Sasa akikujibu hivyo kama ingelikuwa mimi ningemuambia atangaze ndoa. Wengi ambao ni `wanasiasa wa mapenzi' wakifika hapa hushikwa na kigugumizi, `unajua ngoja kwanza kieleweke...' Hapo kama kweli unampenda weka msimamo, kuwa hakieleweki kitu mpaka angalao `uchumba uwepo'.
Hayo ndiyo yangu
emu-three
Anonymous said…
Asanteni sana ndugu zangu kwa maoni yenu.Nipo kwenye kipindi sasa cha kuachana naye, nashukuru sana kaka na dada zangu.nimefarijika sana sana baada ya kusoma maoni yenu.nawashukuru sana.
D habari za masiku wangu.

Nilikuwa busy malishoni na kupika pika..aaa aaa

Nikija kwenye mada ya leo.
Kwanza pole sana kwa wewe dada yalikusibu.

Familia ya mpenzi yako inaweza kuwa na sehemu kwenye mahusiano yenu ila sio ndani kiasi hicho.

Na kama mwenza wako angesimama upande wako ningekwambia kanyaga twende.Ila kwa hali ilivyo...

Wao WAMEMWAGA "ugali" wewe MWAGA "mboga" yaani tangaza njaa.

Namaanisha wewe sepa tu Mungu atakusaidia utakutana na atakaye kupenda na kimo chako.Huyo sio wako.Najua mwanzo itakuumiza lakini amini ni kifo tu ambacho hakizoeleki mengine yote yatanazoelekea baada ya muda.

Dinah tupo pamoja kila siku ..sema muda wa kuachia vijineno wakati mwingine unagomba...aaa aaa

siku njema