Yafuatayo yatakusaidia kurudisha furaha kwenye Ndoa yenu ikiwa mtashirikiana na kuyafanyia kazi. Yote haya mmeishawahi kuyaishi hivyo hakuna ugumu/jipya, sema tu mmezeoana so mnayachukulia kawaida, kwamba hayana "maana/umuhimu" kwa sasa.
-Wote; Acha yaliyopita huko huko yalikopita, kamwe usiayarudishe tena kwasabau tu unataka kushinda mabishano au unataka kumkumbusha mwenzio ni kiasi gani umemsamehe au namna gani alikuwa bwege hapo zamani za kale ili kumshusha na kumuumiza hisia zake(huo ni utoto).
-Wote; Unakumbuka enzi zile kabla hamjawa wazazi? Mlikuwa lovers, natambua hii inaweza kuwa ngumu hasa kwa sisi wanawake(wake)kwasababu katika haki halisi tumebadilika kiakili, kimwili na kiafya. Uzazi ni kujitolea mhanga, uzazi unakuja na trauma sio kimwili tu bali kiakili, Uzazi unabadilisha namna unamuona mumeo sio kwamba anapoteza umuhimu bali unahisi hakuhitaji tena kwasababu kuna kichanga.
Waume zetu mpo vile vile kimwili kwasababu hamkubeba mimba na hamkuzaa, hivyo inakuwa rahisi kwenu kama waume kusema “I want your old you” wakati yeye saa hii ni mama na “old her kwasababu hakuwahi kubeba mimba na hakuwa na Watoto”. Pia hiyo Old us huwa inazibwa zaidi na mapenzi yetu kwa watoto wetu na majukumu yake, by the time wamelala mama unakuwa hoi na unakosa Muda wa kutoa attention kwa baba ukidhani kuwa atakuelewa sababu umempa familia na kuilea 24/7, hyuuuu kumbe mume anadhani Watoto wake wamechukua nafasi yake.
-Mke; ikiwa Mumeo ni wale mpaka uombe kusaidiwa ndio unasaidiwa basi ni vema kukaongea nae nakuomba siku kadhaa ndani ya wiki (Mwisho wa Wiki au siku ambazo afanyi kazi) akusaidie na majukumu ya Watoto kwa kiasi Fulani hasa kama huna dada wa kazi, kama wewe una dada msaidizi huna sababu ya kushindwa kurudi kwenye “old you” na kuwa lover ndani ya miezi 3 tangu ujifungue. Wengine akina sisi tunaoishi mbali na familia tuliozaliwamo na hatuna dada wa kazi kutusaidia ni muhimu kuacha u-superwoman sijui u-kwini…huyo ni mumeo, mwambie ukizidiwa na omba akusaidie kila unapohitaji kupumzisha akili na mwili.
-Mume; msome mkeo, unaweza kupata “old her” lakini inawezekana kabisa kuna vitu siku hizi havifanyi kazi kwake kwasababu kabadilishwa na uzazi wa Watoto wako wapendwa hivyo kuna ulazima wa kumsoma tena na kubadilisha mbinu. Mf: Unakumbuka enzi ulikuwa ukishika kiuno tu kitu na box lakini sikuhizi kiuno kinashikwa na Watoto so mkeo hawezi kupata nyege tena kwenye eneo hilo, au kinyonya titi kama alivyokuwa akinyonya mtoto pia inam-put off so badilisha unyonyaji(muulize how).
Badala ya kuanza kulalamika kuwa mkeo havutiwi na wewe tana kimapenzi, kumbuka kuwa mwili wake sio ule uliomkuta nao ukiwa Bikira(hakuwahi kushika mimba wala kuzaa), baada ya uzazi kwa uzoefu wangu mambo mengi yanabadilika na kuwa better kuliko awali, lakini namna ya kufika huko inakuwa tofauti na iliyokuwa awali. Msome upya mkeo(explore mwili wake) na muulize wapi panamuamsha na namna gani anataka aamshwe.
-Wote; Acha kulalamika, kulaumu, kunug’unika na kuwa busy(marafiki, social media,Tv) unaweza usilalamike na kulaumu au kunung’unika kwasababu upo busy na social media, marafiki, kazi, Masomo n.k. Kuwa available kwa Mkeo/Mumeo wakati wote na hakikisha una-focus kwenye Ndoa yenu na sio watu wa nje ambao sio muhimu.
-Mke; Acha kumnyima mumeo tendo la ndoa bila sababu ya msingi(kuugua), kama umechoka sana mwache afanye amalize….ilakumbuka yeye kukufanya na kumaliza sio sababu kuu ya yeye kufanya tendo na wewe, tendo la ndoa linafanyika kwenye ndoa ili ku-connect naku-renew Ndoa yenu, na ili mume usinyimwe tendo hakikisha unapunguza maudhi(kumbuka triggers za mkeo na Mzunguuko wake wa Hedhi). Ikitokea amegoma usichukulie ki-personal mara zote kama alikuwa kachoka lazima katikati ya siku atakuja ili kufanya mapenzi na wewe kwasababu anajua ni muhimu kwenu nyote kama wanandoa.
-Wote; Acha kuangalia/sikiliza/fuatilia taarifa au Habari za watu wengine na badala yake kuwa-informed kuhusu Mkeo/Mumeo na siku yake ilivyokua, news mtatazama/sikiliza pamoja. Jitahidi kujua siku na mwenza wako nak ama kuna jambolinamsumbua au kama ana hofu yeyote(wake huwa na hofu kibao hasa linapokuja suala la Watoto na future zao)….hii sio kila siku, inaweza kuwa mara mbili kwa mwaka, ni muhimu sana hii kwetu wanawake.
-Wote; Tambua ni jinsi gani akili yako inafanya kazi na ujitahidi uiweke furaha, ifunze akili yako kutoku-react/overreact, kuwaza/fikiria sana kuhusu tukio unalohisi Mkeo/mumeo kalifanya/maanisha na epuka kujitetea, jitahidi kujieleza ili ueleweke badala ya kujitetea kila wakati na kuhusu kila jambo uulizwalo au ufanyalo. Kujishuku/stukia ndio kunasababisha tabia ya kuweka ngao kujilinda kitu ambayo inaweza kumfanya mwenza wako akuhisi vibaya.
-Wote; Fungua Moyo wako, achia mapenzi yako kwa mumeo/mkeo yatawale nakuzalisha furaha, amani na comfort. Mshike, msifie, mbusu bila kuishia kufanya mapenzi na fanya yote yale ambayo unadhani ungependa mkeo/mumeo akufanyie ili ufurahi(zawadi hazihusiki kwenye hili).
Kumbuka Ndoa ni ya wawili, na wote mnanguvu ya kurudisha furaha humo ndoani, weka utayari, nia na ari na nina kuhakikishia mtaifurahi ndoa yetu tena.
Kila la kheri. Bai
Comments