Enzi nafundwa, hakuwa kuhusu kufanya tendo la mikao/mitindo
yake tu bali pia ilikuwa kuhusu Maisha ya ndoa kwa ujumla (Uzazi,malezi ya Watoto,Vifo
na jinsi ya kukabiliana na maombolezo). Unaambiwa wazi kabisa kuna wakati Mumeo
atakosa pesa, mtafiwa na unatakiwa kufanya
nini wewe kama mke ikiwa hayo yatatokea.
Kulingana na urefu wa Ndoa yetu nimekabiliana nayo yote
hayo, hivyo nikalazimika kufanyia kazi kwa vitendo yale ambayo nilifunzwa awali,
kwasababu sikuolewa mara tu baada ya mafunzo, kuna makosa mengi nimefanya.
Baadhi ya mafunzo niliyokuwa nayakumbuka niliyaandika na kuyatunza ki-eletronic
(Unaikumbuka Dinahicious ya 2007/8?) hivyo ilikuwa rahisi kurudi kwenye files nakujikumbusha.
Turudi kwenye Topic ambayo ni Mwanaume na Pesa; Kwa kawaida Mwanamke
anaekupenda kiukweli huwa haonyeshi kujali wala kutaka pesa zako (kama unazo).
Mara zote anakuwa amekwishaona kuwa una potential ya kuwa na kipato cha uhakika
kwa sababu wewe ni ambitious (inategemea na unavyojibeba/jieleza). Anajua kabisa
bila kipato itakuwa ngumu kwake kuvutiwa nawe kwa muda mrefu(maisha ya ndoa), inakuwa kana vile
huna “UANAUME” kwamba hujakamilika kusimamia na kuilinda familia ikitokea
mmeamua kufunga Ndoa.
Ukianza uhusiano na Mwanamke huyu atakusukuma ili kujiboresha na hivyo kukua kiuchumi kwa kupendekeza mf uangalie uwezekano wa kubadilisha kazi, kujiendeleza kielimu ili kuongeza uwezekano wa kufanikiwa na anapofanya hayo anakua very loving, hakusukumi na harudii mara kwa mara…unaweza hata kusahau. Mtakapofunga ndoa nakuanza kuishi pamoja kama Mke na Mume na sasa mna watoto.
Gharama
zimeongezeka lakini anaona unachelewa kufanya mabadiliko, anaweza kujiweka yeye
mbele na kukuambia kuwa anataka kurudi Shule ile kuboresha/ongeza kipato(anakukumbusha
kwa kinyume)….hapo kwa kawaida kama mwanaume utachukua uamuzi wa kufanya
hivyo kwasababu yeye ana majukumu mengine
na muhimu kwa Watoto wenu. Utajitahidi kumpunguzia Mzigo, vinginevyo si atakuwa
single mother with a husband? No...yes.
Kwa kawaida(asilia) mwanamke havutiwi kabisa na mwanaume
ambae hana pesa/kipato….huitaji kuwa Milionea isipokuwa uwe na uwezo wa
kurekebisha mambo na kusimama ikiwa yeye hana Kipato au Ikitokea kaamua kuwa
Mama wa nyumbani uweze kusimamia Majukumu yako kama Mume vema wakati yeye ana-focus kwenye malezi ya Watoto
wenu na kutunza nyumba yenu. Kiasilia Mkeo anahitaji uhakika na ulinzi wa
kipato kama vile wewe unavyohitaji “umiliki”, Tendo la ndoa kwa uhakika,
Heshima na Amani kutoka kwake.
Unatakiwa kufanya nini ikiwa Mumeo kapoteza Kazi?
Unatakiwa kumpoza na kumpa Moyo/matumaini na kumhakikishia
kuwa unaamini anaweza na kuongezea
mengine ya kiimani kulingana na mnachoamini kama familia. Kamwe
usimshushe kwa kumwambia “usijali nitaenda kuongea na Fulani atusaidie” au “usijali
naenda kutafuta kazi” na wala usi-panic
na usimpe presha ya kutafuta kipato. Jukumu lako ni kusimama nae, kumpa support
na kumpa muda(kaa kimya kuhusu issue hii nzima), kama mwanaume anajua nini cha kufanya.
Atajipa siku kadhaa au Wiki then atatoka humo ndani na akifanikisha atakujuza.
Hivi, mnapokwenda nje for dinner na mumeo ndiye alieandaa na kulipia, unahisi nyenyere za ajabu hata kama circle yako ipo ukavuni(baada ya kupevusha pale njia panda ya kuelekea siku Salama na Hedhini)mkifika home huwa mnakuwa na a very hot tendo tofauti na wewe ukiandaa/lipia dinner date? Ukute ni mimi tu.
Haya bwana, takuona wiki ijayo.
Bai.
Comments