Masikilizano/Maelewano(Nguzo tano za Ndoa Bora).

 Masikilizano/elewano huja wakati/baada ya mawasiliano japo ni Nguzo inayoweza kusimama peke yake kutegemea na tukio....mf:- wakati wa manunuzi makubwa(gari, nyumba), familia yenu iwe na watu wangapi?, Shule/Malezi ya watoto na pengine “career”.



Unapowakilisha jambo/kero kwa mwenza wako ni vema kuwa katika hali ya utulivu(sio mara zote hufanya kazi hasa kama mwenzio sio msikilizaji mzuri). Utulivu wako husaidia kutoongea kwa sauti ya kushambulia na hivyo kuepeuka yeye kujitetea(bila shambulio hakuna pa kurudisha shambulio).



Unapoibua suala ili lizungumzwe/jadiliwe nia ni kufikisha Ujumbe/kero na kupata muafaka(maelewano) na sio kung'aka na kuanza kugombana....hii hupoteza muda(kusumbua watoto kihisia/akili) na tatizo kuzimishwa badala ya kumalizwa.



Kuzima/acha tatizo bila muafaka/maelwano kwa muda mrefu hupelekea mwanzilishi wa “mazungumzo" kuhisi kuwa hasikilizwi na hisia zake hazithaminiwi na mwenza wake. Hisia hizo hupelekea hasira(jitahidi kujizuia ili usifanye jambo mbaya) na pengine kupunguza Heshima kwa mwenza wake. Kutoelewana/sikilizana pia hupelekea “issues" kurundikana kitu ambacho sio afya kwenye Uhusiano wenu.




Suala muhimu hapo ni Msikilizaji ambae hakusikiliza na badala yake kuanza kujitetea kwa kung'aka(na kutimia maneno  makali ya kuudhi) au kupuuzia na kuzima(kaa kimya) kuomba radhi.



Siku nyingine, jaribu kuomba mzungumze na kumwambia mwenza wako kuwa “naomba tuongee kuhusu bla-bla-bla, usikilize kwanza mpaka mwisho bila kufoka, kujibu wala kunikatisha. Heshima ikikosekana kwa pande zote mbili, Uhusiano unaweza kuyumba na pengine kufa. Heshima ni Moja ya Nguzo muhimu sana pande zote mbili. 


Njoo tena ukipata muda, tuiangalie Heshima kwa “engo” tofauti na ile ya 2015.....Muda wako unathani kubwa kwangu, ahsante.
Bai.Ma

Comments