Kujali...Nguzo tano za ndoa bora.

 Huwezi kuwa Mke bora kama hufanyi mambo Milioni moja na nusu ikiwa ni pamoja na Kujali. Kujali kwenye Ndoa  sio kitu kinachotakiwa kufanywa na Mke, bali Mume pia. Japokuwa  kwenye jamii yetu Mke ndio hutegemewa kuonyesha kujali zaidi kuliko mwenza wake wa kiume.


Mke atahakikisha Mume analala mahali safi na comfortable, nyumba safi na inapendeza, Nguo na hata Chakula kimeandaliwa vema na kwa wakati. Mke hatoishia hapo, atajiswafi na kujiremba/pendezesha/nukia vizuri kwa ajili ya Macho na Heshima kwa Mume(watu watakao kuona nje).


Mke ataendelea kutoa ushari, kumtuliza, kumpa moyo/matumaini, kum-support, kuhakikisha ana Afya njema na kumkumbusha suala zima la kuilinda Afya yake. Ikiwa mnaishi mbali na Wazazi wa Mume, Mke atakumbusha kuwajulia hali na pengine kwenda kama Familia ili wasipoteze ukaribu kwako na Wajukuu zao.


Mwisho kabisa, Mke atahakikisha watoto wanakubuka siku Muhimu kwa Baba yao na kukupatia vijizawadi kwa niaba yao(Watoto).
 

Uliza Mumeo anakujali kwa 
kufanya nini? Kwa 99% atasema “naenda Kazini kila siku ili kulinda na kulisha familia yangu”. Hutofurahia hilo jibu kwasababu huko sio kukujali bali kutimiza Wajibu wake kama Mume....maana na wewe(pengine Dada wa Kazi) unalinda, tunza, lea, fundisha watoto wenu.




Unajua kwanini Mumeo hajali kama unavyojali wewe?

Ni kwasababu  Mwanaume haandaliwi  kuwa Mume bali Mhudumia familia iwe Wazazi wake ama wadogo zake, ndugu na jamaa(which sio sahihi, na usije hapa na "hii ni kacha yetu". Watoto hawatakiwi kubeba majukumu ya wazazi na watu wengine wakati wahusika wapo hai na wana afya). 


Sasa ili mumeo aonyeshe kukujali inabidi uwe wazi na kumwambia ni nini hasa unataka akufanyie nini? Mf; kama kujuliwa hali mara kadhaa kwa siku, iweke hiyo wazi kwa mumeo. Kama ni kununuliwa zawadi kwenye siku maalumu au bila sababu hakikisha mumeo anajua kama ni kukumbatiwa au kusaidia shughuli za ndani mwambie n.k.

Ahsante kwa kuichagua blog hii.

Comments