Heshima kwa mkeo(Nguzo tano za health marriage).

 Kwa kawaida huwezi kutana na Wanawake(Mkeo) akidai kuheshimiwa mpaka labda Mume utoke nje ya Ndoa ambapo uwezekano wa yeye kubaki Ndoani huwa ni  0.01%(that's me)....Hiyo haina maana kuwa Mkeo haitaji Heshima. Jaribu yafautayo kudhihilisha kuwa unaheshimu mkeo vile anavyo/utakavyo akueshimu wewe.


Usimuudhi/Umize: Msome Mkeo ili ujue nini anapenda/hapendi Uwanjani na nje ya Uwanja na ujitahidi kutekeleza/kuacha vitu hivyo.



Usimfokee/Karipia: Mkeo sio Mwanao/Mdogo wako bali ni mtu mzima mwenzio hata kama umemzidi miaka kadhaa, ongea nae kwa adabu kama Mwenza wako na sio mtu alie chini yako.


Msikilize: Pamoja na kua wewe ni Kichwa na Kiongozi wa Familia haina maana kuwa Mkeo hana Sauti humo ndani. 


Mkeo ni Mwanadamu na m-treat kama mwanadamu mwenzio ila  sio kwa Usawa (kama Mwanaume mwenzio) na sio kwa kiwango cha chini kama vile hana thamani ya Utu.




Usilazimishe Itikadi(mf Ushirikina, Imani, Siasa n.k):  Usijione kuwa wewe  ndio mwenye kutoa Neno la mwisho bila kukubaliana Mkeo. Ndoa ni ya wawili hivyo ni Muhimu kuweka Mada mezani ijadiliwe na kukubaliana/kutokubaliana.


Uwazi bin Ukweli: Ndoa haina siri...siri za familia yako baki nazo, ila wewe na Mkeo hampaswi kuwa na Siri miongoni mwenu. Achana na "mambo ya kiume hutakiwi kujua", Mkeo anatakiwa kujua Kila kitu kuhusu wewe na uyafanyayo.


Usimzungumzie vibaya; kwa watu baki (online)hata kama ni rafiki ndugu au jamaa. Haijalishi amekuudhi kiasi gani na unahasira vipi!  Usitumie jina baya kumuwakilisha Mkeo. Jitahidi kutumia "Mke wangu" zaidi kuliko Mama watoto hasa kama ulizaa(ga) kabla yake(Mama mtoto/watoto linaondoa Heshima ya Ndoa kwa Mkeo).


Usitoke nje ya uhusiano wenu Kiakili  Kihisia au Kimwili:  "Social media" imefanya watu kudhani kumsaliti Mwenza ni pale tu unapofanya Tendo Kimwili(busy, shika, jigijika n.k)


Ukaribu unaokua nao na watu/mtu online with pic bin video na sauti ni sawa na kuwa nae/o Kimwili ila inaenda ndani zaidi Kisaikolojia na kubaki na wewe kwa muda mrefu kuliko tendo la dk 45. Kwenye  Jinsi ya kumheshimu Mume  ongezea hili.


Epuka taarifa baada ya maamuzi: Zungumza nae kuhusu jambo ambalo unataka kwenda kufanya kabla ya maamuzi(isipokuwa kama ni "sapuraizi").


Usimshushe mbele ya Watoto/Adharani: Kama amekosea na kuna hitaji la kumkosoa/rekebisha, ni vema kusubiri muda ambao mtakua peke yenu na kuwakilisha Hoja yako. 


Ahsante kwa ushirikiano.

Comments