Kwanini kila mtu anazungumzia Mahusiano, Mapenzi na Tendo la ndoa?

Jibu rahisi ni kwasababu kila mwanadamu anahitaji mapenzi, mahusiano na Ngono, ukiachilia mbali kuwa hitaji hilo ni sehemu ya haki yako kama mwanadamu pia ni sehemu ya afya ikiwa yote hayo matatu yatafanyika kwa kufuata utaratibu mzuri ili kujilinda na maradhi na unyanyasaji. Kwa vile tu ni haki ya kila mwanadamu kupendwa/penda, kuwa kwenye mahusiano na kufanya tendo la ndoa haina maana ujilazimishe kwenye mambo hayo wakati uhitajiki, unateswa na Maisha yako yapo hatarini aukuhatarisha Maisha yaw engine.

 

Watu wengi wanaamini kuwa wanawake ndio tunaongoza kuzungumzia masuala hayo mitandani, kwamba hatuna la maana la kuongelea ambalo linajenga Zaidi ya hayo mambo 3 ambayo yakifanyiwa kazi kwa Pamoja (na ukapatia kuchagua) unapata matokeo mazuri na hivyo kuongeza furaha na Maisha yako. Wiki iliyopita niliandika kuhusu wanaume kuandika masuala hayo kwenye magazeti na ndio ikawa sababu ya mimi kuanzisha Blog hii.

 

Mimi na wewe tupo hapa kutokana na mambo hayo matatu, inawezekana labda hukuzaliwa katika mazingira ya mahusiano na mapenzi bali ngono(kubakwa au ulevi au mazizi wako mmoja alikosea…pole) au una uzoefu mbaya na watu wa jinsia ambayo sio yako na hivyo imetokea tu unachukia/unaogopa au huoni umuhimu wake.

 

Sio kila mwanamke anataka kuwa kiongozi au boss lady na sio kila mwanamke anataka kuwa Feminist wave 3(hawa awa sasa ambao wengi wao ni millenials), baadhi yetu sisi ambao tulizaliwa mwisho mwa mwaka 1970-1989 tume-relax na kufurahia “options” tulizonazo ambazo zilipigwaniwa na Mama zetu (wa Ulaya) kuanzia miaka ya 1950s, kwamba kama wanawake tunaenda shule nakupata Elimu ya juu badala ya kubalehe na kuolewa.

 

Tunatumia Elimu kupata kazi na kuingiza kipato ili kujitegemea wakati tunasubiri kukutana na Mr right. Baada ya hapo  bado una options kibao nje ya nyumbani  kama Mke  kwa mumeo….mkijaaliwa/kubaliana kuanzisha familia options bado zipo kwako wewe kama mwanamke….je ubaki uwe mama wa nyumbani na nakuitumia kuwafundisha Watoto wenu au urudi kazini nakuacha mtoto alelewe na mtu/watu baki au uwalee kwa muda Fulani(miaka 5 ya kwanza) halafu urudie/badilishe career yako au uendelee kuwepo nyumbani nusu na kuwepo kazini nusu?

 

Kwa nchi za Magharibu(hasa Ulaya) wanawake wana haki nyingi kuliko wanaume, mimi kama mama wa Watoto wawili wa kiume na mmoja wa kike, naliona hilo kwa ukaribu Zaidi na imefikia mahali nahisi kuwa sio sawa. Naona kabisa baadhi ya sheria za kumlinda mwanamke ni unyanyasaji kwa wanaume. Kabla ya kuwa mama kwa wavulana wangu, sikujali.

 

Nikijibu swali kuzungumzia masuala ya mapenzi, mahusino na tendo ni rahisi na huitaji kutumia akili kwa kiasi  kikubwa isipokuwa pale unapotaka kujiswali la mtu kulingana na “situation” yake bila kujua upande wa pili. Sasa kama wewe ni mfanya kazi, mwanasiasa, mtumishi wa Serikali, mke/Mume au mwanafunzi….shughuli unazozifanya kutimiza majukumu yako zinachosha akili. Huwezi kutoka Job akili imechoka halafu uanze ku-blog kuhusu Kazi zako. Ukiweza basi blog yako haitofika mbali kwasababu utaishiwa topics, hutokuwa na muda siku ambazo umechoka kiakili na vilevile utakosa msukumo wa kuendelea kwasababu ya kukosa wasomaji.

 

Maelezo kuhusu mapenzi, mahusino na tendo la ndoa mengi ni yale yale(ndio maana slogan yangu ni “tukumbusha” sio “nikufunde”, hakuna jipya lakini kumbuka kuwa sisi kama binadamu tupo tofauti sana sio tu kimazingira bali pia kielimu, kiupeo(siolazima uwe na elimu), kiuzoefu, kisaikolojia kimalezi/tabia. Unapoingia kwenye mahusiano mara zote unakuwa hujui “how to” kwenye mambo mengi.

 

 Ukiingia kwenye ndoa pia utakuwa hujuo “how to” kwenye masuala kibao, mkijaaliwa Watoto napo kuna ma-how to kibao kama wazazi wapya, mume na mke halafu mama na baba. Hivyo Pamoja na kuwa mambo ni yale yale bado ni tofauti na unahitaji kujipa nafasi ya kujifunza mawili matatu kutoka kwa watu wengine ambao wana uzoefu Zaidi au uziefu tofauti na wako lakini walipitia issue inayokutatiza sasa hivi.

 

Hitimisho: Siasa, Upiganaji, Uongozi au Utumishi wa Umma sio kwa kila mtu kama ilivyo kuwa Mama/mke wa nyumbani au mjasilia mali, lakini kila mtu anahitaji Mapenzi, Uhusiano na Tendo la ndoa at some stage of their lives.

 

Niakuache kwa sasa, yep ni mimi yule yule  Dada Di wa enzi, nimerudi. Ahsnte kwa ushirikiano.

Comments