Kama mke umejitosheleza?

 Kila Mwanamke ni Imara hiyo inajilikana na wala huitaji kujitanganza(kuwa chini ya Kundi fulani kuthibitisha hilo), pamoja nakusema hivyo  wewe kama Mke bado ni Dhaifu/laini(Kimwili) na hakuna kosa mkimama kuwa mlaini(jivunie  udhaifu wako).


Kazi yako kubwa Duniani ni kuwa msaidizi wa Mumeo, kuleta uhai(kubeba Mimba na Kuzaa), kulea, kufundisha na kutunza Familia.



Ili uweze kufanya hayo(niliyoyatajabhapo juu) unatakiwa kuwa  umejitolesha kwenye nyanja nyingine ili kurahisisha Maisha yako kama Wewe, Mama na Mke. Unapaswa kuwa na uwezo  wa kufanya baadhi ya vitu haraka na kwa ukamilifu bila uwepo wa mtu wa pili iwe Mumeo au Muuza Huduma.




Je ni nyanja gani hizo?

Dharura; Unaweza kujituliza, kutafakari kwa haraka na kufanya uamuzi kwa faida yako na familia badala ya kusubiri mpaka Mumeo apokee Simu/arudi.


Uchumi; kuwa na Akiba ya Senti kwa mahitaji madogo madogo(ya ghafla) nje ya Bajeti ya Familia(kutoka kwenye zile anazokupa Mumeo), sio kila akikupa Pesa unatumia zote kwa wakati mmoja. 


Elimu; Uwezo wa kuwafunza watoto wako na kuwasaidia wanapokwama Kimasomo, ili kukuza uelewa wao wa Somo husika wanapokwenda Shule.


Nyumba; Usafi wa Mazingira...kuibadili Nyumba na kuwa Nyumbani kwa kila mtu sio familia yako tu. Uwezo/juzi wa kurekebisha mf; bulb imeungua au "fuse" imekata  sio mpaka uite Fundi Umeme/usubiri Mumeo akuje.


Tendo; Unahamu, badala ya kulianzisha, unasubiri mpaka Mumeo akusogelee? Acha hizo.


Labda leo mwendo ni mrefu, badala ya kulalamika, kuonyesha haupo "interested" na kubaki umelala kama gogo...kuwa na mbinu (sio kukata kiuno)za kumfanya awahi "kucheka" na wakati huo huo wewe kufurahia safari.


Kujijali/Jipamba; Jifunze kutengeneza Nywele, Kucha, kujiremba n.k ikitokea Salon zimefungwa *cough* Covid19  Lockdown *cough*. Na mwisho kabisa, Jifunze aina tofauti za Mapishi, aina 3 za kushona/repair nguo(hasa kama una watoto). 

Je, wewe ni Mke uliejitosheleza? Ongeza zako basi na mie niongezee kwangu.

Muda wako unathamani kubwa kwangu, ahsante. 
Bai.

Comments