Kazaa na kuolewa kisa Umbali.....nipo radhi kurudiana.

Nimatumaini yangu humzima dada dinah  pole na kazi unayoifanya ya kutuelimisha.
Mm nikijana ninae ishi Mbeya.


Nimekuwa kwenye mahusiano kwa muda kidogo. Nilikuwa ninampenzi wangu  ambaye nimekuwa nae zaidi ya miaka 2  huyu  mpenzi wangu alikuwaga rafiki yangu toka utotoni na ukweli tulikuwa tunapendana sana.



Na tulikuwa tunamipango mizuri kama wapenzi na nilikuwa kwenye mipango ya kumtambulisha nyumbani kwetu kwa wazazi wangu japo nyumbani wazazi walikuwa wakimfahamu.



Sasa huyu mwenzangu alihitaji kujiendeleza kimasomo na kweli alipata Chuo, kwenda kusoma kwa mwaka mmoja kwahiyo Morogoro ambapo alikuwa anaishi na nduguzake.


Mahusiano yetu yaliendelea vizuri huku tukiwa tunawasiliana na tulikaa mwaka mzima bila yakuonana. Tulijitahidi kuonana lakini fedha ilikuwa kikwazo kwasababu ya  umbali hivyo tukakubaliana amalize masomo yake atakapo rudi tutaonana.




Kama  unavyojua  mkisha kuwa mbali na hasa wapenzi kukorofishana kupo. Kuna kipindi tulipishana na hatukuwasiliana ndani ya mwezi mmoja ila tulikuja kupatana tukaendelea kama kawaida.



Kumbe ktk kipindi ambacho tulipishana na mwenzangu yeye alipata mwanaume mwingine ambaye alimpa Mimba na kipindi tunasameehana alikuwa tayari ana Mimba na ukweli alinieleza



Sasa huyo jamaa aliye mpa Mimba alikuja akamuoa huyo binti na mpaka sasa amejifungua mtoto. Lakini tatizo lililopo  kwangu huyu mwanamke muda wote amekuwa akiwasiliana na mimi na amekuwa akiniambia bado ananipenda na hata mimi moyo wangu bado unamuhitaji.



Alikubali kuolewa kwasababu ya ile Mimba maana kuna kipindi alitaka kuitoa ili aendelee  kuwa na mimi ila mimi nilimsihi asifanye hivyo.

Naomba ushauri wako dada dinah mimi bado na mpenda huyu mwanamke hata yeye ananipenda na yupo tayari kumuacha huyo mumewe.

************

Dinah anasema: Mungu anabariki na ahsante kwa ushirikiano.

Kwanza napenda ufahamu kuwa mwanamke hapewi Mimba bali anashiriki kwa hiari yake tendo ambalo matokeo yake ni mimba.


Sio kama mwanamke alimfuata na Mimba kisha akambebesha bali mbegu za jamaa na yai lake ndio Mimba so hakupewa Mimba na bali kashika Mimba. Hilo moja.



Pili....kuna uwezekano mkubwa kuwa aliahidiwa kwenda huko ili akasomeshwe na huyo mkibaba.....kumbuka umesema hukuwa na pesa hata za kufanya mawasiliano.



Kutokana na mahesabu yangu ya ghafla hapa sio rahisi kwa mtu kwenda mahali kusoma na ndani ya mwaka mmoja kushika mimba na kuolewa....ni wazi kulikuwa na kauhusiano kasiko rasmi lakini serious na huyo mjamaa hata kama ulikuwa ule wa Internet sijui whasaap bin facebook na walipokutana ikawa kama wamejuana kwa miaka kadhaa.....uaicheze na Power of mawasiliano ya Kimtandao.



Huyo mwanamke hakuolewa kwa sababu ya Mimba.....alishika mimba kwa vile hakutumia Kinga na ameolewa kwasababu alitaka hiyo Ndoa.



Maana kama kweli Mimba ilimfanya aolewe ni wazi hakutaka kulea mtoto bila baba yake.....sasa jiulize kwanini leo akuambie kuwa yupo tayari kuiacha ndoa ili aje kuwa na wewe halafu na wewe uamini?



Najua unampenda au unahisi kuwa unampenda kwasababu katika umri wako niliouficha ni wazi kuwa unahitaji kusafisha macho a bit more kabla haujajua kama ulipenda huyo Binti au unadhani kuwa ulimpenda.


Umekwisha sema pesa ilikuwa kikwazo sasa je ukirudiana na huyo mwanamke na mzigo wake ambao ni mtoto utakuwa tayari kumsaidia kumlea mtoto huyo in terms of pesa?  Au utakuwa fine mwanaume mwenzio kukusaidia kumtunza mpenzio.....Maana watoto ni gharama.


Je? Unampango gani na huyo mwanamke.....unataka tu uhusiano wa nakupenda tangu enzi au unamalengo mengine huko mbele Ndoa ikiwa moja wapo.



Usijekubali aache ndoa aje kwako kisha siku yakimshinda kwako au usipomtimizia mahitaji ya mwanae akulaumu kwa kumharibia maisha yake na mwanae.



Nadhani ni vema kukubali tu kuwa hakuna future kati yako na huyo mkimama.

Poteza mawasiliano yale na wewe go out a bit more ukapate penzi la kweli kutoka kwa mtu mwenye kukuthamini jila kujali umbali au kipato.




Akiendelea kukufuatafuata mwambie ungependa kuanza fresh bila kuhofia mtoto wa mwanaume mwingine ulietereza nae nje ya uhusiano wetu.


Ka cheat.....kashika Mimba na kaolewa na huyo alieCheat nae bado unataka kurudiana nae?

Wacha kujishusha chini zaidi ya tumbo la Nyoka......jirudishie heshima na kujiamino kwa KUSONGA MBELE BILA YEYE.

Kila la kheri.

Comments

Anonymous said…
Kaka ili uishi kwa amani yakupasa ukubali ukweli japo unauma kwa vile unampenda.jipange achana na huyo mke wa mtu...mungu atakubariki na atakupa mke atakae kupenda na kukuvumilia hata pale ukiwa vibaya kiuchumi
Anonymous said…
Kaka yangu sikushauri umuoe tena huyo mwanamke. Kwana poteza nae mawasiliano haraka iwezekanavo ili kukwepa vishawishi japo ni ngumu kwa mtu unayempenda. maana kama yuko tayari kuiacha ndoa yake ina maana huyo mwanamke hajatulia na huenda huko ndani ya ndoa kuna shida au mumewe hamtimizii mahitaji yake yote hivyo huyo mwanamke ni kiruka njia. muombe Mungu atakuopa mwanamke wako atakayekupeda kwa hali uliyo nayo na mtaoana tu mwache huyo na ndoa yake. maana kama hajatulia iko siku atakukimbia tena wewe aende kwa mwanaume mwingine.
Unknown said…
Kaka, kwanza kabisa nikupe pole kwa yalio kupata. Wewe siowakwanza kukutana na hayo, yameshawakuta wengi maishani! Apo unatakiwa kutumia akili sana nasio kufwata hisia za moyo. Utampendaje mtu ambaye amekusaliti? Mapenzi kweli yananguvu kama mauti vile, ila wewe apo nikuangalia matokeo ya baadaye. Je unafikiri bado unaweza kumwamini tena kama zamani endapo akikwambia neno, hasa pale anapokwenda mbali nawe? Kama hukuumia naalioyafanya nakuimiza kumchukuwa ila kama umeumia basi naongopa usije ukaumia zaidi kupita kiasi! Kunadalili zinazo onyesha kwamba hakuwa na Mapezi ya dhati nawe! N.B: Uwamuzi ni wako kaka sisi niwashauri tu.
Anonymous said…
Achananae