Imekuwa kawaida kwa baadhi ya Blogger KUIBA kazi zangu na kufanya zao kwa kuongeza picha au kubadili kichwa cha habari.
Kwa miaka Saba blog yangu inamashabiki na wapenzi hivyo wanapoona kazi yangu imetumiwa kwingine huja kunitonya.
Nimekuwa nikidharau kwa muda wote huo na wakati mwingine kufurahi kuwa kazi yangu inapendwa mpaka wengine kuikopi na kuipesti au kuanzisha Blog ili kublog post zangu za miaka ya nyuma kama zao.
Mwaka huu sitaki ujinga tena. Nitafanya kila liwezekanalo kuhakilisha post zinazoibwa Mwaka huu zinaondolewa kwenye blog husika na Google.
Hii tabia ilinifanya nipungize kutoa Masomo mara kwa mara kwasababu mijitu haitoi Credit kwangu au hata kuweka link ya Blog yangu kama kielelezo cha wapi wametoa maelezo husika......ni lwasababu wanataka ionekane wao ndio wajuzi.
Niandikayo yanatokana na uzoefu wangu binafsi kama mwanamke wa Kabila fulani......hivyo sio kila mtu atakuwa na uzoefu uleule hata kama anayoka kabila moja na mimi.
Najaribu kufanya Mawasiliano na Google as well third parties ili wanisaidie kutatua issue hii.
Ahsante kwa uvumilivu na endelea kuniyonya kila unapoona maelezo ya Dinahicious kwenye blog.....forum....social media n.k.
Shukurani kwa ushirikiano na uvumilivu.
Comments