Chanzo cha Nyumba ndogo.

Dada habari za Kazi? kwa muda nimekuwa na maswali mengi, juu ya chanzo cha michepuko katika jamii. Mimi ni kijana wa umri wa miaka 35, ni baba mwenye mke mmoja na watoto wawili wa kiume.


Nimebahatika kujenga nyumba kwa ajili ya kupangisha, Lakini nimegundua sehemu kubwa ya wapangishiwaji ni wadada ambao ni nyumba ndogo. Inakuwa kama sehemu ya kuja kuwaficha, wengine hata kazi hawana wanawategemea wanaume wao. Nimegundua wakati wa kwenda kudai kodi yangu, nikaambiwa na majirani kuwa mwenyewe haishi hapo anakuja mchana na kuondoka.


Kwenye appartment sita, wapangaji 4 nimekuta wanaishi style ya kihivyo. Kwa kweli nimejiuliza nini chanzo cha nyumba ndogo hasa? Naomba usitoe jina langu.

*************


Dinah anasema: Njema tu mkibaba. Ahsante kwa ushirikiano.
Nakumbuka niliwahi kulizungumzia hili miaka 7 iliyopita wakati naanza kublog. Kuna sababu nyingi za watu kuwa na nyumba ndogo na moja kuu ni kutokuwa na mapenzi ya dhati na ukosefu wa nidhamu kwa mke au mume wako na kutojali hisia za watoto.


Sababu nyingine ni ndoa za kulazimishwa/ lazimika kwamba unaoa au kuolewa kwasababu Imani yako ya Dini inakulazimu kufanya hivyo au unahisi umri umekwenda na hutaki kuzeeka bila mtoto au mke/mume. Ndoa za kutaka Makaratasi(Uraia kwa wanaoishi nchi za watu), kutaka mali so mtu anafunga ndoa bila mapenzi bali circumstances. Huwezi ishi maisha yako yote kwenye ndoa bila mapenzi au furaha.



Ipo siku utamdondokea mtu kimapenzi lakini hutotaka kutoka kwenye ndoa kwasababu ukitoka unaharibu mambo mengine yaliyosababisha ufunge ndoa in first place. Hivyo mtu anakaa kwenye ndoa kama status lakini mapenzi yanakuwa kwingine. Baadhi ni kuingia kwenye ndoa wakiwa bado hawajamaliza "ujana"  yaani hawapo tayari ku-commite kwa mtu mmoja au ni umalaya wa mtu tu(hataki kuzishinda taama sababu zinamfanya ajisikie ana nguvu).


Wengine ni kutoridhika/tamaa, ego kwa baadhi ya wanaume, ulimbukeni na kujaribu ku-fit in. Kukata tamaa kwa baadhi ya wanawake na kukubali ku-share mwanaume na mwanamke anaemjua hivyo kudhani mwanaume alioko kwenye ndoa ndio mtulivu kuliko vijana, kwamba akiwa na mume wa mtu anajua akitoka kwake anakwenda kwa mkewe na sio kwingine.....which is sad.


Sababu nyingine ni walioko kwenye ndoa kung'ang'ania ndoa mbaya au za mateso wakiamini kuwa ndoa zao zimepangwa na Mungu na hivyo ipo siku Mungu atambadilisha mwenza wake na atarudi kwake. Mara zote nasisitiza kuwa usikimbilie kufunga ndoa kwa sababu nyingine bali mapenzi ya dhati. Na kwa mkimama angalau olewa na mtu mwingine sio yule aliyekutoa Bikira kwasababu ukiingia kwenye ndoa ukiamini bikira yako kwake ndio italinda ndoa unajidanganganya.


Pia kunamfumuko wa Wanawake ambao hawataki/hawapenzi wanaume lakini wanataka watoto, hawa wanawake wapiganaji Malkia wa nguvu hukubali kuwa Vimada bila shida sababu wanataka kuwa in-control na maisha yao ya kipiganaji bila kuwa na majukumu ya Mke, kwasababu wh



Mapenzi ya kweli hayaishi wala hayachushi wala kuchosha bali hukua kama siku zinavyokwenda so long mnafanyia kazi uhusiano wenu kwani mapenzi pekee haya simamishi ndoa au uhusiano bali kile unachokipokea na kukitoa kwenye ndoa hiyo. Ndoa ni zaidi ya Bikira, Ngono, kupikiwa futari na kuzaa. Ndoa ina mambo mengi na  inahitaji kufanyiwa mambo mengi mno na baadhi nimekwisha yagusia kwenye blog hii.


Nadhani kwa leo niishie hapa.

Comments

Anonymous said…
kwa mtizamo wangu hizi nyumba ndogo/vidumu vinaletwa na kutoridhishwa na mapenzi ya mwenzi wako. hasa kwenye sekta ya sex, kama kila mnapokutana mmoja wenu anatoka hajaridhika, na amejaribu kuongea na wewe lakni bado mambo yanakua vile vile, tena kibaya zaidi anafikia kuona kama unamfanyia makusudi, bai anaona hakuna haja ya kulumbana wakati ipo namna ya kutatua tatizo kimya kimya, ndio hapo anapotafuta mtu wa nje ili kukidhi haja yake