Dada D, nachukua nafasi hii kukupongeza kwa kuwa umekuwa una jibu maswali mbali mbali kwa ufasaha sana. Kuna mambo mawili napenda kukuuliza
i)nafasi ya bikira kwenye kuoa. Je Mwanamme akioa binti asiyekuwa na bikira anakuwa ameoa mke wa mwenzie?
Baba mmoja alikuwa anaugomvi na mkewe tatizo ilikuwa wivu, mwanamke alikuwa anataka kujua ameongea na nani? mbona anafuta msg kwenye simu yake ndo jamaa akamwamwambia mkewe kuwa kwani wakati nakuoa ulikuwa na Bikira? Mbona una kuwa na wivu wa kijinga? Je kuoa binti asiyekuwa na Bikira inaathari gani ndani ya ndoa.
***************
Dinah anasema: duh! Huyo mume mtu lazma atakuwa anatereza nje ya ndoa yake na kumkashifu mkewe ni sehemu ya kuzuia mkewe asiendelee kumfuatilia kwa kuogopa kukashifiwa tena.
Hapo Kisaikolojia mke ata back off akijiona mwenye "makosa" kwa kuolewa bila Bikira. Nafasi ya mwanamke kwenye ndoa ni ileile iwe aliolewa akiwa bikira au hakuwa nayo.
Hapana! Ikiwa hujafunga ndoa na bikira haina maana umeoa mke au mume wa mwenzio. Ili mtu awe mke au mume wa mtu ni lazima taratibu fulani zifuatwe na ubikira sio moja wapo (unless bado unaishi 1800s). Kisheria ukilaa na mkibaba au mkimama kwa miaka miwili inahesabiwa kama ndoa. Kungonoka ni muhimu, ni tendo la kuunganisha viungo vya uzazi....by doing so sio kugunga ndoa.
ii)Kuna haja gani kwenda honey moon wakati mmeshazaa mtoto na wengine watoto wawili. Au ni kwenda kuteketeza pesa, tafadhali nitoe ushamba ka sio uluga luga.
kazi njema.
***************
Dinah anasema: Unless bado tunaishi miaka ya 1800s ambapo Fungate ilimaanisha siku 7 za kuzoeshana endiketa.....kutoana Bikira na pengine kushika mimba. Siku hizi Fungate ni uamuzi wa mtu baada ya kufunga ndoa. Wengi wanachukilia kama mapumziko maana watu wamefanya maandalizi ya sherehe za ndoa kuwa complicated na kujaa mastress .....kwamba badala ya kurudi Kazini siku moja baada ya kufunga ndoa unataka ukapumzike.....thank God vikao vimeiaha badala ya halleluja nina mke/mume.
Wengine mpaka leo tumezaa watoto wawili bado hatujaenda Fungate......sasa kwani muda ulikuwepo? Tulikuwa busy na kazi na maisha matokeo yake tukaamua kuzaa na maisha yamekuwa busier kuliko so honeymoon is out of the window. Kama pesa ni zao wanandoa wacha waziteketeze kwani wamezifanyoa kazi lakini kama ni za michango aka za kuomba nadhani hata mimi sitopendezwa.
Natumaini nimekujibu kama ulivyotarajia.
Asante kwa ushirikiano.
Comments