umekua ukitusaidi kuhusiana na mahusiano ya kimahaba.
Nimekuandikia
ili unishauri juu ya tatizo langu kama ifuatavyo. Baada ya kumaliza masomo nilipata Kazi hivyo nikaona ni vyema nitafute mwenzangu.
Nilikumbuka enzi zile nikiwa shule kuna mdada nilimwacha kama madarasa mawili nyuma kwa sasa yupo Chuo, nilimkazia fikra zangu zote
nilikumbuka jinsi alivyokuaga mwema mtulivu.
Tulikua marafiki wa kawaida nilimheshimu sana nikaona she is the best. Nilitafuta mawasiliano yake nikapata tukawa tunaongea na kuchat sana kupitia Simu.
Nilimweleza hisia zangu akakubali akasema hata yeye alikua
akinipenda sana. Tuliendelea kuchat na kupeana ahadi nyingi.
Akasema wakifunga Chuo wakati anaelekea nyumbani atapitia kwangu kuna jambo la kuzunguma na ni vizuri tuonane.
Walipofunga chuo akaja, nilienda kumpokea kwa furaha coz ni muda wa kama 5yrs hutujaonana. Alizidi kuwa mrembo ila mkononi alikua amepakata
katoto kama kamiezi mitano doh!
Tulipo pata nafasi ya kuzungumza alisema tatizo ndio hilo ana mtoto
amezaa na Mume wa mtu na huyo jamaa ni baba wa watoto watatu na walikutana huko Chuoni.
Kwa mujibu wa maelezo yake Jamaa anatoa ushirikiano mzuri tu katika
malezi ya mtoto, matumizi na wanawasiliana.
Nikamuuliza ilikuaje mpaka mimba inamaana walikua hawatumii kinga! akadai ni utoto alikua hajui mambo ya uzazi.
Kweli nampenda natamani tuoane ila hili linakua zito, ahadi na viapo vyangu vinanisuta kumwacha, nifanyeje?
Kinacho niuma zaidi siwezi
kuzuia mawasiliano yao coz ni baba wa mtoto japo anasema hana uhusiano
naye tena. Kiukweli najenga picha mbaya kichwani akiwa huko Chuoni sijui
kinachoendelea.
Naomba msaada wa kimawazo nifanyeje. ASANTE!
************
Dinah anasema: Habari ni njema kabisa, ahsante na shukurani kwa ushirikiano.
Anasingizia utoto, angekuwa mtoto asingechanua miguu kwa Mume wa mtu na Baba wa watoto 3, angelala na kijana mwenye umri unaofanana na wake. Alijua alichokuwa akikifanya. Tangu hukuwa nae kipindi hicho, achana na hilo!
Natambua itakuwa ngumu sana kwako kuwa na amani Moyoni kila wakati Mwanamama huyo anapokuwa Chuoni na "baba mtoto" wake. Watu waliokwisha onana wakiwa Uchi (Exes) achilia mbali ku-share mtoto ni ngumu kuaminika wakiwa peke yao.
Mbaya zaidi huna nguvu kwenye maisha ya huyo Mdada kwasababu uhusiano wenu sio rasmi hivyo huwezi kumshauri/shawishi ahame Chuo ili awe mbali na Baba mtoto wake wala ku-demand mipaka kati yake na Ex wake.
Kama kweli unampenda na unataka ku-share maisha yako nae + mwanae basi anza kuweka "msingi" serious wa uhusiano wenu sasa huku ukiungulia maumivu ya kutomuamini anapokuwa na Ex wake na mtoto wao mbali ya macho yako.
Uhusiano ukikomaa angalau utakuwa na sauti au nguvu ya kumuwekea Mipaka mpenzi wako kuhusu Mawasiliano na Ex wake.
Kwasasa huyo Mdada anasoma which means hana kipato na hivyo hawezi kumtunza mtoto hali inayopelekea yeye kumtegemea huyo Mume wa mtu.
Usijemharibia "utaratibu" wa kujikimu alafu ukaja muacha huko baadae ateseke na mwanae akiwa mwanafunzi (hana kipato).
Kwenye Matunzo ya mtoto kunaweza kukatwa ikiwa wewe utakubali kumhudumia mtoto kipindi ambacho mama yake hana kazi....utakuwa umejipatia "ready made family"
Kwa upande mwingine itakuwa nzuri kipindi hiki mtoto bado mdogo sana so utakuwa kama umemuasili mwanae na hivyo kum-cut off baba yake (akikua mtamwambia ukweli).
Ila kumbuka kuwa kufanya uhusiano na mwanamke mwenye mtoto na mwenye connection ya karibu na Ex wake kama huyo wako ni ngumu sana, maisha yako yote yatakuwa ya wasiwasi na hofu kila wakati Baba mtoto anapotaka kumuona mwanae au mtoto (akikua) anataka kumuona Baba yake.
Weka "nampenda sana" na "viapo na ahadi zako kukusuta" pembeni kwanza halafu kaa chini na jiulize tena, katika umri wako ambao ni chini ya miaka 35, upo tayari kweli kulea mtoto wa mwanaume mwenzio?
Je, kweli gharama hizo za maisha (mtoto ni gharama) ndizo ulizokuwa ukizihitaji mara tu baada ya kuanza kazi au ni muhimu kujipa Muda, kujijenga alafu ndio Utafute Mwenza?
Fanya uamuzi kulingana na majibu yako.
Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...
Comments
Kwanza, inawezekana kabisa huyo mzazi mwenzie hakumuweka wazi kuwa alikuwa ameoa na watoto.Naamini kabisa aliwekwa giza na akaja kumuambia wakati mambo yameharibika ingawa pia namshangaa hakuweka tahadhari ya mimba walipopenzika.
Jambo la pili, ni kwamba kama kweli unampenda, naamini suala la mtoto haliwezi kuwa kizuizi. Muhimu ni kwamba umsome huyo bibie na umwelewe na umpokee moyoni mwako. Matunzo ya mtoto hayatakulemea maana naamini hata mama yake atakuwa na kipato mtalea tu mtoto bila shida.
Huwezijua, huyo mtoto anaweza kuja kuwa baraka kubwa kwako. "wahenga walisema, Usitukane mamba kabla hujavuka mto" Nina ushahidi wa ndugu yangu ambaye alimnyanyasa sana mke na mtoto aliyezaa nje kabla ya kuoana na kumfukuza nyumbani mtoto huyo wakati huo akiwa darasa la sita. Akaenda kukaa kwa bibi mzaa mama yake maana baba yake alikuwa alishafariki. Leo huyo mtoto(mtu mzima sasa)ana nafasi kubwa nzuri TRA.Na yule baba anaadhirika mitaani anatamani angemuomba hata sent lakini aanzie wapi.
Nakushauri kama Dada Dina alivyosema anza kujenga uhusiano wa karibu naye ili utenganisha muunganiko uliopo kati yake na yule mzazi mwenzie na hilo pengo ulizibe.Ukiweka nguvu zako na nia yako kama ni mpango wa Mungu kuwaunganisha naamini utasahau yote na badala yake utamwangalia mpenzio. Nakutakia kila la heri.HUyo amejifunza mengi na amejua kosa alilolifanya sasa mkumbatie kama mioyo yenu imeambatana vema.