Sikati Ngono, lakini nampenda.

Shikamoo da dinah, pole na kazi. Nashukuru kwa msaada wako katika masuala haya.

Kwa kuanza mimi ni binti wa miaka 21 sijawahi fanya mapenzi kabisa hadi hivi sasa nipo Chuo Kikuu mwaka wa kwanza.

Nina mpenzi wangu ambaye anamiaka 27 na anampango wa kuoa miaka miwili ijayo kuanzia sasa! Anakazi nzuri na kimaisha kajiweka vizuri.


Tokea kuingia katika Uhusiano wetu ni miezi minne(4) sasa tunachat ila kuonana ni mara chache siku za weekends kutokana na kubanwa na shughuli zake.
 


Sasa imefikia wakati anaomba tufanye Mapenzi, ameshaniomba mara nyingi na kunihimiza nikamuambia sipo tayari kuanza mapenzi ningependa tusubiri.


Da dinah kijana huyu tumesha kiss mara kadhaa na kiukweli nimempenda ila naogopa kuanza ngono, halafu isitoshe sijui kwao, ndugu ,wala rafiki zake yaani tunajuana sisi wawili tu (mimi na yeye).
   

Kwa kuwa tu muazi kwako da dinah ni kwamba naogopa kuanza mapenzi nikiwa bado Mwanafunzi na familia inanisomesha, Pili naogopa kupoteza Bikra au Usichana wangu kwake.


Tatu naogopa maambukizi na Mimba zisizotarajiwa. Sijawahi kuumizwa katika mapenzi na ninavyohisi anavyo nga'ngania kufanya hivyo na mimi je tukifanya na akiniacha na kuingia mitini?


Da dinah naomba ushauri wako maanake kijana huyu hasikii wala haelewi. Na je ni sahihi kweli kufanya hayo mapenzi mkiwa bado bf na gf na je ni wakati gani bora wa kuanza hivo???

Ntashukuru kwa Your help.


Dinah anasema: Marhaba Mrembo, shukurani kwa Ushirikiano.


Kabla ya yote, Kazi yake nzuri na kujijenga kwake kimaisha hakukuhusu wewe (kunamhusu yeye na aliyemsomesha labda na ndugu zake)....usifanye uamuzi kwa ku-base kwenye material thingizi*


Nae kama ni mwizi vile eti! Atafunga Ndoa in Two years time....kukuoa wewe (ambaye huijui familia yake na wala haijui yako) au tayari anamchumba Kibindoni?


Maana kujipangia kufunga ndoa ndani ya miaka Miwili wakati sasa ni Mwezi wa Saba ni ama anakupa matumaini in a "ushawishi" way ili ukubali kumpa Ngono ukitarajia kuolewa au tayari anamchumba/mtu anaetarajia kumuoa.

Halafu mrembo unanichanganya, unasababu nyingi na za Msingi na Msimamo mzuri wa kutotaka Ngono sasa (unahitaji muda) ila sielewi kwanini unasema unampenda lakini hutaki usichana wako upotezwe na yeye?!!

Uhusiano wenu hauna miezi Minne kwasababu mnakutana mwisho wa Wiki(Weekends) tu....ikiwa kwa mwezi mnakutana mara Nane kwa mfano! Hiyo inafanya uhusiano wenu kuwa na Siku 32 which ni less than miezi 2!

Ikiwa umemuambia kuwa haupo tayari kwa Ngono lakini anashindwa kukuelewa na kuendelea kulazimisha ni wazi kuwa hakufai au "hamfaani"....yeye anataka uhusiano wenye kuhusisha Ngono na wewe hutaki kupoteza Usichana wako kwake.

Au labda ni vema kumwambia ukweli kuwa hutaki yeye awe mpenzi wako wa kwanza Kingono, hii itawapa nafasi nyote wawili kufanya mtakayo kwa uhuru.

Wakati mwingine Mapenzi ni bahati nasibu, ukiamua kujiingiza kwenye haya mambo hutakiwi kutegemea sana utakaeanza nae ndio atakae kuwa Mumeo.


Kama umeamua kujihusisha na Mapenzi ni wazi Ngono itahusika at some point lakini ili usiwe disappointed ni vema kuchukulia kila siku kama inavyokuja na kufurahia Maisha yako kama mwanamke.

Mimi siwezi kujua kama akipata Ngono ataingia mtini au Mtafunga Ndoa. Maumivu ya Mapenzi hayaepukiki, inawezekana Mwanaume asikuache lakini wewe ukagundua kuwa hakufai na hivyo ukaamua kuachana nae....bado utaumia, haijalishi unaacha au kuachwa, mapenzi yanauma sawa.

Kutokana na Maisha yalivyo hivi sasa, kwamba wengi tunabaki shule kwa Muda mrefu na tuna "uhuru" wa kuchagua tuwapendao wengi tunaanza Ngono tukiwa kama Bf na Gf....ila sio lazima, inategemea na Msimamo na Uamuzi wako binafsi.


Suala la Mimba, Maambukizi na hofu nyingine zote ulizonieleza ambazo hazihusu "uhusiano" nadhani ni vema ukizungumza na Mama yako kwa uwazi, yeye yupo kwa ajili hiyo.


Kamwe usifanye jambo kwa ajili ya kusukumwa au kulazimishwa, wewe ndio mwenye Mamlaka na Mwili wako na si mtu mwingine yeyote hivyo kama hutaki huo ndio Uamuzi wa mwisho!


Kama anakupenda kweli basi ataheshimu Uamuzi na Msimamo wako na kusubiri mpaka utakapokuwa tayari.....mmh lakini umesema hutaki upoteze Bikira kwake....Mwache aende zake basi!

Muda mzuri wa kuanza Ngono:

Miaka 21 nadhani ni umri mzuri kwavile mwili wako kama mwanamke unakuwa ume-settle lakini kama unaweza kusubiri mpaka 28 pia sio mbaya...ni uamuzi na msimamo wako. Usijitunze kwa ajili ya mwanaume bali kwa ajili yako wewe mwenyewe.

Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

Comments