Moyo umekubali, Akili imegoma!

Shikamoo dada, pole na majukumu na ufanisi mkubwa wa kazi unayofanya. Dada dinah problem yangu naileta kwako nafikiri itakuwa solved.





Ni muda sasa tangu niachane na ex wangu na bado sijapata mahusiano mengine, shida ni kuwa muda mwingine nikiwa nimetulia nashangaa namkumbuka tu yeye.




Kuna wakati hadi jina lake nalitaja hali ambayo sipendi na ninataka nisiwe nayo kwani nishakubali matokeo kwamba hanifaii  ila naona akili yangu kama imestuck kwake.




Sitaki memory yoyote ije kichwani kwangu kuhusu yeye, nifanyeje? Thanks inadvance dada.


***********


Dinah anasema: Marhaba mrembo, nashukuru kwa ushirikiano.



Inategemea ulimpenda kiasi gani? Uhusiano wenu ulikuwa wa Muda gani? na mliachana katika Mazingira gani?




Ni hali ya kawaida kwani ni mtu uliekuwa nae karibu na pengine ulitumia muda wako mwingi kuwa nae. Itakuchukua muda ili kumsahau yeye kama Mtu na kusahau kile mlichokuwa nacho(Uhusiano).




Kuacha au kuachwa kote kunauma sawa kwani hivyo haijalishi kama umekubali kuwa hakufai na kumuacha au yeye kakuacha wewe....vyovyote vile Hisia(Moyo) na Akili vinahusika.





Maumivu ya Mapenzi hayana ujasiri....Unahitaji kujipa muda wa "kufanya Msiba wa Uhusiano wako" na kuzika yote yaliyopita ili uweze kusonga mbele ukiwa huru na mwenye furaha. (Rejea majibu yangu kwenye Post niliyoelezea namna ya kusonga mbele baada ya Ex Wiki 2 zilizopita).





Kama tayari Mwaka umepita tangu muachane basi jipe tena Miezi Sita au hata miaka mingine miwili ili kupona kabisa.




Pamoja na kujipa Muda, uponaji wako unategemea zaidi juhudi zako za kutaka kusahau yaliyopita ili uweze kuendelea na maisha yako kirahisi.





Jitahidi kutumia muda wako mwingi na watu waliokaribu na wewe na kufanya activities za pamoja, kucheka na kufurahi pamoja.





Hakikisha siku yako inakuwa imejaa shughuli ili kuepuka kukaa peke yako na ukifika nyumbani unakuwa hoi (hupati muda wa kumuwaza Ex).




Jipe muda na ifunze akili yako "kuzima" au "ku-switch" mawazo ya Ex kwenda kwenye kitu kingine.


Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

Comments