Wake kwa Waume hunyanyaswa na Wenza wako lakini naamini Wanawake tunanyanyaswa zaidi.....pamoja na kusema hivyo, haijalishi kama wewe ni Mwanaume au Mwanamke....Unyanywasaji/Unyanyaswaji(aiii chagua lililo sahihi) ni Kosa Kijamii na Kisheria, hakuna visingizio.
Wengi huvumilia Vitendo viovu na vya Kikatili (Kinyanyasaji) kutoka kwa wapenzi kwa kutumia visingizio kama "nampenda sana"...."Ni moja ya matatizo madogo tu ya Ndoa, vumilia"...."Nikitoka hapa nitaenda wapi?"...."Nimeisha zaa nae, sitaki watoto waishi bila Baba/Mama" n.m (na mengineyo).
Nisikupotezee muda, nitakuorodheshea vitendo vichache kadri ninavyokumbuka as I go(write) ambavyo ni vya Kinyanyasaji lakini wewe hujui au unachukulia tu kuwa "ni sehemu ya maisha ya ndoa/Mapenzi" hivyo ni lazima Uvumilie.....Hapana! Ndoa sio Mateso....ndoa ni Furaha na inapaswa kuendelea kuwa yenye furaha.
*Mpenzi kutwa/kucha (anatumia muda mwingi na watu wengine) yupo nje na marafiki ambao huwajui....au online kwenye Social media ana chat, haonyeshi kukujali na ukijaribu kuongea nae anakujibu kwa mkato.
Au Akiwa nyumbani yeye na Simu yake au Tablet huku akionyesha kufurahi na kucheka na watu wake.....wewe ukimsemesha au kujaribu kuwasiliana anakujibu kwa hasira na haonyeshi furaha; Unakunyanyasa Kihisia.
*Badala ya "kulianzisha" kimahaba kwa kukushika au kukuita kwa Huba na Mapenzi, yeye anasema "nataka/nipe haki yangu ya ndoa".
Unaponyesha kukataa ama unampa sababu kwanini hutaki Tendo (unaumwa, umechoka) lakini yeye hajali anapanda na kuendelea.
Anajua hutaki tendo Kinyume na Maumbile, lakini anategea ukiwa umejisahau au umelewa "Kilele" yeye anajiingilia "Tigoni" bila ridhaa yako(anakubaka); Unanyanyaswa Kijinsia na Kimwili.
*Kila mnapozungumza, yeye hujibu kwa kufoka....kosa dogo tu lazima ufokewe, ususiwe kama ni chakula au nyumba.
Anapenda kukufananisha na Ex au watu wengine kwenye familia yake au jamii mf: "Wanawake wengine wanafanya hivi, sio kama wewe unafanya hivyo". Au hakuna mwanamke alewahi kunifanyia hivi, wote walikuwa hivi na vile, sio kama wewe.
Anakusimanga, anakutukana na kukuita majina mabaya Mf; Malaya, Mvivu, Mchafu, Unaroho mbaya, Unanuka, hujui kulea, kwenu Masikini, Goli kipa, hujasoma(huna Elimu) n.k; Unanyanyaswa Emotionally.
*Anakupiga au kukushika kwa nguvu, anakusukuma na kukupiga masingi; Unanyanyaswa Kimwili na ki-emotional.
*Anakupangia namna ya kutumia pesa zako au pesa anazokupatia kwa ajili ya matumizi na mara zote anataka aone orodha ya vitu ulivyofanya kwa kutumia Pesa husika....akiona umenunua kitu cha kike kama Vipodozi, Nguo n.k anakuwa Mbogo....anaweza kuvitupa au kuviharibu; Unakunyanyaswa Kiuchumi na Ki-emotional.
*Anakupiga stop usiwe karibu na Ndugu zako, anakataza usiende kwenu ila analazimisha uende kwao; Unakunyanyasa Ki-emotional.
*Mnaweka pesa(Mishahara yenu) pamoja, lakini yeye ndio mwenye Mamlaka na Akaunti husika....siku zote hujui Balance na huambiwi pesa zimetumikaje na kwanini? Huoni wala hujui pesa zinapokwenda, lakini kila mwisho wa mwezi Akaunti haina Hela wakati wote mnapiga mzigo(fanya kazi) na pesa zinalipwa Direct kwenye Akaunti; Unanyanyaswa Kiuchumi, Kihisia na Ki-emational.
*Watoto wakifeli au wakifanya makosa makubwa mf: Kupata Mimba au kumpa Mimba Binti.....Baba anakasirika na kukususia akisema "wanao hao" badala ya kukaa chini na kujadili namna ya kumsaidia mwanenu kama Wazazi; Unanyanyaswa Kijinsia.
*Bila makubaliano unaletewa Mtoto/Watoto wa Nje au waliozaliwa kabla hujaolewa/Oa na kulazimishwa kuwapenda au kuwalea kwasababu Mume/Mkeo ni Baba/Mama yao; Unanyanyaswa Kihisia, Ki-emotional na Kiuchumi (ikiwa kama unatumia pesa zako au mlizotunza pamoja bila Mchango wa Mama zao).
*Anatereza Nje ya Ndoa/Uhusiano; Unanyanyaswa Kihisia na Ki-emotional.
Baadhi ya watu wamelelewa katika Mazingira ya Kinyanyasaji (Baba anamnyanyasa Mama au Mama anamnyanyasa Baba) hivyo wanakuwa wakiwa "wameaminishwa" kwa kuona kuwa hivyo ndivyo watu wanapaswa kuishi, bila kujua kuwa ni Kosa Kisheria kumnyanyasa mwenzio.
Kwa leo naishia hapa, lakini kama una hofu na vitendo vya Mwenza wako kwako, tafadhali usisite kuongezea kwenye Comments.
Natumaini maelezo haya yatakupa mwanga mpya kwenye maisha yako ya Kimapenzi na Mhusiano na hivyo ku-fight back au kutoka kwenye Uhusiano/Ndoa rather than kuwa "ndio bwana".
Tunakubali kuishi na tunaowapenda ili kwa pamoja tufurahie maisha, lakini kama hakuna furaha kwanini uendelee kuwemo kwenye Maisha na an abuser?
Shukurani.
Mapendo tele kwako...
Comments
Joe