Na pia ni kweli mwanaume mtu mzima ndio anajua kujali kwenye Mapenzi kuliko kijana?
**********
Dinah anasema: Hi! Bila ya samahani.
Kumjua mtu kabla hujawa nae karibu (bila uhusiano) sio jambo rahisi kwani hata nafasi ya kumuuliza haitokuwepo.
Hata ukiwa kwenye uhusiano haikupi "guarantee" kuwa huyo mtu ni mkweli na anataka siku moja mfunge Ndoa. Lakini inakurahisishia kumsoma mhusika na kujua kama anapoteza muda tu(anapita) au anataka Uhusiano wa kudumu na hatimae Ndoa.
Pia inakuwa rahisi kumuuliza kuhusu uhusiano wenu unaenda wapi? Mf; miaka 3 imepita hakuna dalili ya kuposwa, unaeza uliza "Mpenzi unadhani tutaishi kienyeji mpaka lini?" Akijibu kwa hasira au akizunga au akisema "tuangalie itakavyokuwa" ujue huyo hana mpango na Ndoa kwa wakati huo.....ni mfano tu.
Sio kweli kuwa wanaume watu wazima ndio wanajali kwenye Mapenzi kuliko Vijana. Kujali nadhani inategemea na mtu na sio umri.
Asilimia kubwa ya Wanaume watu wazima 40+ wenye wake zao ndio wanaongoza kwa kuwa na Vimada.....wanaacha wake na watoto wao wanakula kwa kujinyima, kusoma kwa shida huku wao wakisomesha na kulisha Familia za Vimada wao....sasa kujali hapo kupo wapi eti?
Sielewi unamaana gani unaposema "mtu mwenye nia na Malengo na wewe" kwani wewe ni "object"?!!....Ndoa ni muungano wa watu wawili wanaopendana/waliokubaliana kuishi pamoja kwenye "commitment" ya kutotanga-tanga na watu wengine mpaka mwisho wa Maisha yao.
Utamjuaje; inategemea na mhusika ila maongezi yake kwako tangu mwanzo wa uhusiano yatakuwa yanalenga Maisha ya baadae kama ninyi na sio yeye(kwamba inakuwa wewe na yeye).
Hatokuwa mtu wa kuzungumzia mambo ya starehe (outings sana) na utaona dalili za yeye kutaka familia....atakusogeza kwa watu wake muhimu (Mama, Baba, Kaka)....dada ni muhimu ila sio kivile.
Kutamani kuolewa kwa baadhi ya wanawake ni kitu cha kawaida au niseme ni moja ya Malengo waliojiwekea Maishani na wangependa yatimie......Kama ilivyo kwenye Kifo, hujui ni lini lakini unauhakika kuwa ipo siku utaondoka....sasa Ndoa nayo wakati mwingine ichukulie hivyo....wacha haraka.
Jaribu kutafuta kitu kingine ambacho ni muhimu kwako ili uweze ku-focus on wakati unaendelea kusubiri kukutana na mtu atakae kupenda na wewe kumpenda na mengineyo.
Umri wako kuna wengi watajitokeza, vijana na wazee, wenye wake na watoto, wanene na wembamba.....muhimu ni kutulia na kufuata Moyo wako na usisahau Akili....kwa maana epuka mwanaume wenye familia na epuka kuwa Mke wa pili hata kama Dini inaruhusu na Moyo unataka kwenda huko.
Kuwa na mume wako peke yako ambae hajawahi kuoa(hana uzoefu na ndoa au kuishi na mwanamke nyumba Moja) kuna raha yake atii.
Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...
Comments