Napendwa na wawili

Pole na kazi, samahani naomba ushauri wako. Kuna Wanaume wawili wananipenda sana na wote wanania moja ya kutaka kunioa, sasa sijui mkweli ni yupi?





Mmoja wapo nilishakuanae kwenye uhusiano miaka ya nyuma na tuliishi vizuri sana ila mimi ndie niliemsaliti. Sasa amerudi tena na kudai bado ananipenda.





Moyoni bado nampenda ila naogopa asije nifanyia revenge baadae na pia naogopa kuhusu ndugu zake wakijua kuwa mimi ndie niliye muumiza ndugu yao itakuaje?




Japo yeye amenihakikishia kuwa hakuna baya litakalotokea. Please dada nisaidie kwa ushauri wako.


*******

Dinah anasema: Ahsante kwa ushirikiano.



Kabla hujaanza kujipa mastress kuhusu Ndoa na Ex uliemtenda....unapaswa kurudi nyuma na kukumbuka kilichokufanya umsaliti mwenzio, je unadhani hakipo tena? Unadhani kabadilika? Je wewe umebadilika na unauhakika ukiwa kwenye Ndoa hutoshawishika tena na kumsaliti mwenzio pale atakapokuwa Mumeo?





Kutokana na maelezo yako inaonyesha unamtaka uliemtenda (Ex) kwasababu ume-claim wazi kwamba Moyoni unampenda na maelezo yote yameegemea kwake kuliko huyo mwingine.





Lakini pia maelezo hayo yanakubana, kwani yanaashiria kuwa hujabadilika kwa maana kuwa unao wote kwenye Uhusiano ila hujui ni yupi wa kubaki nae.





Kama hiyo ndio case basi ni vema kuachana na huyo ambae inaonyesha hujamfia kiviiile (Haiwezekani kupenda watu wawili kwa wakati mmoja huku una Moyo Mmoja tu) ubaki na huyo uliewahi kuwa nae (Ex) alafu uangalie mambo yanavyokwenda kabla ya kukimbilia Ndoa.





Huna haja ya kuhofia ndugu zake so long umejirekebisha na unauhakika hutorudia kumsaliti mwenzako tena. Sidhani kama atakurudishia Kisasi ila hofu yako kutokana na ulichomfanyia inaweza kukusumbua na kukufanya uhisi anakusaliti ili akurudishie maumivu uliyompa.




Ijue thamani ya Mwili wako, tambua tofauti ya kupendwa na kutamaniwa kisha fanya uamuzi wa busara.


Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

Comments

Anonymous said…
mmoja anatosha, mwingne wanin? bt 4me namuunga mkono da dina endelea na yo x boy huyo mwingne mpotezee, ucumize sana kichwa
Anonymous said…
Kuna x huwa wanajidai wanapenda tena ila ukijiingiza huko utajuwa kwanini watu hukojoa wakati wa kuoga. maamuzi na ukweli unaujua wewe. kuwa muangalifu.