Mimi ni msichana wa miaka 20na naishi Dar. Ninatatizo, hapo mwaka 2010 nilijihusisha na mahusiano na kijana mmoja ambae hakua na kazi alikuwa anaishi na rafiki yake.
Ila mara nyingi alipokuwa akiumwa nilimhudumia kwa matibabu, chakula na hata pesa ya matumizi wakati mwingine nilikuwa nampatia sababu mimi nilikuwa nafanya kazi.
Baada ya Mwaka mmoja nikaanza kuwa namfanyia surprises mara nyingine naenda anapoishi bila kumwambia nikawa nafuma sms za mapenzi nakuta amemtumia msichana. Akawa ananiomba msamaha namsamehe.
Baada ya muda tena nakuta sms za mapenzi mwishowe nikachoka nikaamua kuachana nae. Japokuwa niliachana nae ila bado alikuwa ananifuatilia na kuniomba msamaha.
Hivi karibuni alinifuata tena na kuniomba msamaha na kuomba turudiane sababu anakumbuka wema wangu nilomfanyia wakati hana kitu.
Sasa hivi yeye ni General manager wa kampuni fulani Dodoma.
Anasema anajisikia vibaya kutumia na msichana mwingine wakati nipo niliyemvumilia wakati wa shida. Sasa sielewi dada nifanyeje kiukweli bado nampenda ila naogopa kuumizwa tena na mapenzi.
*************
Dinah anasema: Marhabaa Mrembo, shukurani kwa Ushirikiano.
Nina chuki ya kipekee na Exes (wajinga-wajinga) ila huyu wako tumpe robo Moyo (nafasi) kama rafiki kwanza ili tuone kama yaliyomo yamo kabla ya kutoa Moyo wote.
Maana ukikurupuka ukatoa Moyo wote alafu ukaja kugundua kuwa jamaa anamtoto au mpenzi mwingine utaumia mpaka upoteze hamu ya kuwa na Mwanaume mwingine maishani mwako.
Sasa kabla ya yote ni vema mkae chini na kuzungumza kuhusu mnachokwenda kukifanya.....weka hisia zako wazi kuwa mlipokuwa pamoja hakuwa muaminifu na tabia hiyo ilikuumiza sana na unahitaji kuthibitishiwa kuwa ni muaminifu ili umuamini.
Hoji (huku unachunguza taratibu) ili kupata ukweli kama yupo "single" au anataka kulipa Wema wako (kutumia na wewe) wakati ana Mpenzi mwingine. Ukigundua yupo ni m-clean (hana mpenzi wala baby mama) basi ongeza robo iwe Nusu Moyo.
Mkiendelea vizuri na akawa muaminifu basi mkabidhi Moyo wote ila ubaki na akili zako.
Mambo yasipoenda vizuri basi songa na maisha yako na utapenda tena.
Inaonyesha ni binti unaejielewa, unajitegemea kiuchumi, Mvumilivu na mwenye utu na huruma (kutokana na maelezo yako).
Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...
Comments