Ex anigombanisha na Mama

Habari yako dada dinah, hongera kwa kazi nzuri yakuelimisha jamii. Mungu akuzidishie upeo wako. Mimi ni mwanamke wa miaka 25 na pia ni Mwanafunzi wa Mwaka wa mwisho Chuoni.


Naishi Marekani na familia yangu (mama na wadogo zangu). Kukata maelezo ni hivi; nilijuana na Ex wangu kupitia Mitandao ya Kijamii. Yeye anaishi Dar na kufanya kazi kwenye Kituo kimoja cha Radio.


Ni Mkaka alienizidi miaka 7, tulizoeana kwa muda na hatimaye tukawa wapenzi. Najua unaweza usinilewe kwa nini nilianzisha mahusiano kwenye Social Networks while am miles away.

Basi tulipendana kama ujuavyo mapenzi akanieleza maisha yake ambayo kwa alivyoyaeleza kama ya kawaida na mimi nikamweleza ya kwangu vile vile.

Nikiwa bado sijaonana nae nilifanya mpango wa yeye kuonana na Mama yangu mkubwa ambae amenilea tokea mdogo. Kweli alienda kuonana na Mama yangu mkubwa ikawa rahisi kwa mimi kuzidi kuweka imani na huyu kijana.

Mwaka ukapita nikasema nitajibana hivyo hivyo ilimradi nirudi nyumbani nikamwone. Kweli tulionana mwaka jana mwezi wa Pili nia na madhumuni ilikuwa tujuane zaidi lakini nikagundua matatizo yake kwa kipindi kifupi nilicho ishi nae ambayo ni Miezi Minne. ‎


Niligundua kuwa ni Mvivu sio maisha tu mpaka na mambo ya chumbani. Sikuwa free na yeye maana hakutaka nijiachie alisema hapendi kusikia miguno kwa kuwa anahofu majirani watasikia. nikamsikiliza kwakuwa nilikuwa nimezimika kwake.

Kero ya pili ikaja hataki niongee usiku yaani nisiwe free anaasema napiga kelele. Nikajipa moyo nivumilie kwa sababu nilivichukulia vitu vidogo.


Kero ya ya tatu ilikuja ni kwamba familia yake inamtegemea yeye kwa kila kitu hali inayofikia mpaka Mkate wa ahsubuhi apeleke na sio kwamba kwenye familia yake hakuna Vijana wapo kama wa 5 wakubwa na wadogo kwake lakini hawataki kazi hivyo yeye ndio aliebeba Msalaba.


Kabla sijaondoka akaniambia kuwa ameridhika na mimi nakutamani siku moja niwe Mkewe. Nilifurahi hivyo tukawekana kwenye mikakati ya maisha nini tufanye na nini tuepukane nayo.
Muda ‎wangu ukafika nikaondoka zangu na kurudi huku.


Nilipofika familia yangu ikamwambia akajitambulishe rasmi kwetu hivyo akatoa Posa lakini kabla hajafanya hivyo nilimsihii asifanye mambo kwa papara au kwakuwa familia yangu imesema ndio afanye akajibu anafanya hivyo kwakuwa anamalengo na mimi.


Basi baada ya miezi michache baada ya posa nikamwambia kwa kuwa saivi anawaza mimi kuwa Mkewe ajipange atafute Biashara afanye maana kazi yake inalipa Mshahara mdogo kulipia Kodi ya Nyumba yake plus familia yake.


Akanijibu sawa lakini hakuna kilichofanywa nilijitahidi kila wazo kumshauri afanye haikuwezekana. Ni mtu aliezoea kuingia Kazini jioni muda wa masaa matatu kamaliza kipindi anarudi Vijiweni/Bar kwa washkaji zake.

Ile hali iliniumiza maana ni mtu anaejulikana mjini lakini hataki kusaidiwa na watu zaidi ya kujionesha ana kitu ilahali anakufa na tai yake shingoni.


Nikaona nisimng'aninize sana nikamshauri afanye basi chochote anachokipenda ili mradi kimwingizie Kipato. Ikawa hola! Hakufanya. Muda ukaenda kuna hela nilipata ya Mkopo nikanunua mzigo Nguo, Viatu na Accessories za kike tufanye biashara hapo Dar ili tusogeze maisha lakini pia ili mshinda aliuza robo tu na vyengine kubaki navyo huku akiwa na sababu nyumbani biashara ngumu.

Kuanzia hapo ndio nilipoanza kumtoa Moyoni maana niliona najitahidi kupanga nae mipango ya maisha lakini mwenzangu ananiangusha hivyo nikawa mchungu maana nimetoa hela ya Mkopo yote kwenye biashara while yeye hata Sumni yake sioni mtu anaejita mchumba kwangu.


Nikaanza kumpotezea hali iliofikia mpaka tukawa tunagombana kila siku. Yeye akawambia familia yangu waongee na mimi ambapo mama yangu aliniambia nimvumilie nisiwe haraka na maisha.


Nikawasikiliza familia yangu lakini still yale mapenzi na hisia zilizokuwepo before zikatoeka sikuwa namuona kama bwana wangu tena. Nikamvumilia hivyo hivyo kwakuwa sikuwa na mtu wa kunisupport upande wangu zaidi ya wadogo zangu tu. 

Baada ya miezi mitatu‎ nikiwa na fanya shopping na familia yangu nikakutana na mkaka ambae ni Mwafrica ila si Raia wa Tanzania. Tukabadilishana namba na kuanza mawasiliano.


Nikaanza kutoka nae maeneo mbali mbali yote kupunguza stress kichwani mwangu na wala sikuwa na wazo la kuja kufall kwa huyu jamaa mpya ambae amekuwa karibu na mimi pamoja na familia yangu.

Ex wangu akaanza kero maneno maneno yakawa mengi baada ya kuona na mpuuza maana sikuwa tena na ile kumshauri kama ilivyokuwa ada yangu nilimwacha afanye ajisikiavyo yeye.


Akaanza kuambia familia yangu na other relatives kwamba nimebadilika simjali kama zamani kitu ambacho kilinipiss off maana kila mtu ikawa mimi ndio mbaya.

Nikamwomba ex wangu kistaarabu tuachane maana sioni kinachoniweka na kero zimeashakua too much. Yeye akasema nisahau icho kitu hawezi kuniacha labda kama nataka kusikia kajiua.


Mara akawa ananiambia jamii itamcheka akiachana na mimi. Ilimradi nikawa simwelewi na threatens kibao‎.
Mbaya zaidi izo threatens zake kawaeleza mpaka familia yangu hali iliyofikia kwetu hasa mama yangu mzazi kunilazimisha nijari‎bu kukaa na huyo jamaa hata kama mapenzi yamepungua kwake.


Ukweli nigombana na mama yangu kwenye hili suala na hii hali imechangia mimi kukaa na huyu kijana mwengine muda mwingi maana nyumbani kwetu kuna waka moto.

Kwa sasa najiona nimeshaanza kumpenda huyu mwengine. Ila ndio hivyo Ex wangu vitisho vingi, sijui hata nimweleze vipi anielewe.

Hata Mama yangu nimweleze vipi akae upande wangu kama mwanae. Maana sasa hivi mama yangu amemchukia Kijana wa watu as if yeye ndio alieanzisha ugomvi mimi na ex wangu wakati ugomvi uko tokea zamani.


Nitashukuru mawazo yako maana sina wakumuelezea hisia zangu akanielewa.

Ahsante.


***********


Dinah anasema: Wee niamkie....Habari ni njema tu Mrembo, shukurani kwa ushirikiano.


Huyo nae wa wapi?!!....wacha ajiue bana, Msiba ukiisha life goes on without him....kwani mlikuja wote Duniani? Kila mtu kaja kivyake na ataondoka kivyake. ( I hate Exes with passion....that's all)!!


Nadhani kuchekewa kwako kumaliza/ua Uhusiano ndio tatizo kuu. Ulipoanza tu kuhisi kuwa "hakufai" maishani basi ungeomba kwenu warudishe Posa ya jamaa na kuua Uchumba there and then.

Usijali wala kufuatilia anasema nini kwa nani, yaani kaa mbali na kila kitu kinachomhusu. Alafu muweke chini Mama yako....Mama haitaji kukuelewa, anahitaji kukubali uamuzi wako with or without her support.


Kwanza wao (Familia yako) ndio walikuwa na kiherehere kutaka huyo Ex ajitambulishe na kutoa Posa, sio wewe. Sasa wasianze kukulazimisha uvumilie sijui nini na nini....hii ni 2014 sio 1974....hatulazimishani wala kuolewa ili kulinda "heshima" ya familia....tunaolewa ili kufurahia Maisha na tuwapendao, kama hakuna mapenzi na furaha Ndoa ya nini?.


Au kama vipi mtokee Mdingi na umuombe kurudisha Posa....kama unaweza ilipe mwenyewe via Baba, Baba huwa waelevu sana kwa sisi watoto wa Kike hasa kwenye issue za Maisha na Mapenzi/Ndoa kuliko Mama.

Piga marufuku Mama yako, Familia na ndugu zako kujihusisha na huyo Mtangazaji na wakiamua kuendeleza "Mahusiano" ni wazi kuwa wanakana undugu wao kwako na ku-claim undugu na Mtangazaji....weka wazi kuwa hutaki kusikia lolote kutoka kwa huyo Ex.

Hayo yote hayawahusu, Mapenzi ni ya wawili....ukihitaji ushauri wao utawaambia lakini kwasasa waachane na huyo Ex kwani huna mpango wa kurudi huko. Wasikufuatilie na huyo kijana wa sasa unless wewe mwenyewe utake kuwahusisha.

Mama akiendelea kukuletea habari za Ex, mlie bati....yaani piga Kimya aka mnunie. Unamsalimia na unaendelea kumheshimu lakini hupigi nae stori(kama mnaishi pamoja).

Lakini kama upo kwako, na Mama kwake basi huna haja ya kumsalimia hata kwa Text....Mchunie mpaka agundue kuwa anachokifanya ni kosa na halikupendezi.....akikupigia mpe majibu mafupi na makavu ili kufikisha ujumbe kuwa hunafuraha na tabia yake ya "kushikilia Bango" issues zako binafsi...(works all the time).


Kama unahisi mapenzi na huyo Kijana mpya, hakuna haja ya kujibana....jiachie uone kama yaliyomo yamo ila usikimbilie mambo ya Posa na makorokocho Mengine kama vile Kuzaa mpaka uwe na uhakika na unachokwenda kukifanya na huyo Mwafrika (Asijekukutumia kwa ajili ya Makaratasi....Mjini hapa...)!


Hakuna haja ya kuwa stressed na maisha yaliyopita.....akijiua ni kutokana na matatizo yake mwenyewe na ataiumiza zaidi familia inayomtegemea na si wewe wala familia yako so akili kichwani mwake.


....fanya kama vile hujawahi kukutana nae....furahia maisha yako na kila la kheri katika kumalizia Masomo yako.


Kila la kheri
Mapendo tele kwako...

Comments

Dawa yao said…
Sista pole kwa yote, wel said Dina.Kuna msemo Wa Maya Angelou Dat wen a person show u who ril he Is for the first tym believe him.Sista uctegemee anything new kwa uyu mburullah go on with Ur lyf
Anonymous said…
Bibie, wote wa bongo na huyu wa kwa Obama ninyambafu watupu.Tena utakuja kugundua kuwa heri wa bongo kuliko huyo unayetaka kumzimia sasa.Mimi nakushauri tulia kwanza endelea na kuandaa maisha yako binafsi pasipo kuhusisha vibweka vya mahusiano.25 yrs can not make you run fast to find someone for your future.You are still young.You need more time to think out of your box. Don't allow such stuff to stress you right now.TULIA BINTI make good life for on your own without involving in such relationships. I know exactly that you are in need of a man, but just take it slowly because you will mess up and get lost if you are not careful in searching for men. It is God who can give you the man you are looking for.So pray and stick on improving your life. I wish you all the best and God bless you!!
Anonymous said…
Huwa nakupenda sana dinah.unajua kushauri kweli