D'hicious leo ni Mwaka wa Saba!

Hongera na Ahasnte kwa kuichagua Blog hii siku ya leo ambapo inatimiza Miaka Saba.




Napenda kuchukua nafasi hii kukushukuru wewe Msomaji, Mtembeleaji, Mchangiaji na zaidi ni wewe unaenitumia Mwaswali kwa kuamini kuwa nitakupatia Ushauri ambao kwa namna moja au nyingine utasaidia kupanua mawazo yako na hivyo kufanya uamuzi sahihi.





Kwa dhati kutoka Moyoni nasema ahsante sana kwa kunipa nguvu ya kukaa chini na kufikiria nikupe ushauri gani na Changamoto ya nikushauri vipi?





Kuna Baadhi ya Watu hunipa Changamoto kweli kweli, wakati mwingine nashindwa ku-switch off "kichwani" swali/maelezo husika na hivyo kabla usingizi haujanipitia naanza kufikiria namna ya kujibu/shauri.





Kumbuka tu kuwa Ushauri unaotolewa kwenye D'hicious sio sheria, hivyo ni hiari yako kufuata yote, kuacha yote au kuchukua unayodhani yatakusaida kwenye kutatua issues zako.





Mwisho kabisa napenda kusema ahsante kwa my little ones kwa kulala mapema so that I can write this Post.




Mungu aendelee kutupa afya njema, atupe akili na upeo wa kuweza kuona na kukabiliana na issues kwenye Ndoa/Mahusiano yetu ili tuishi kwa Amani na furaha.


Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

Comments

Anonymous said…
Hongera Sana, uongezeke maarifa na busara ili kuisaidia jamii kwenye mambo ambayo kwetu ni ya siri
Anonymous said…
Mungu akubariki sana da dina kwa kazi ngumu ya kutuelimisha nakutakia kila la heri mamii
Unknown said…
Hongera sana dada blogu yako inanielimisha sana.Hakika wewe ni babu kubwa. All the best
Anonymous said…
Hongera mom upo juu
Anonymous said…
Hongera sana sana! Ujaaliwe zaidi...
Anonymous said…
Hbd our lovely blog, Mungu ibariki blog na dada Dinah kwa kujitolea kutuelimisha, mimi nimejifunza sana sana hapa kwenye blog yako,sina cha kukulipa ila Mungu ndio akulipe lililo zuri, AMEN!!Love you Dinnah!
Mama H & I!
Anonymous said…
Hongera Dada dina blogu yako ni nzuri sana Mungu azidi kuwa na wewe
Anonymous said…
Nami napenda kutoa shukrani zangu za pekee kwako kwa kupara wazo la kuanzisha blog hii na kutoa ushauri na kuelimisha jamii juu ya maswala ya jandoni na unyagoni kwa upeo mkubwa na ulobobea. Nakutakia kila jema ktk maisha yako na blog pendwa yetu idumu dawamu.
Anonymous said…
Kila lenye kheri Sister!
Anonymous said…
hongera sana