Natumai umzima wa afya na unaendelea kuendesha gurudumu la taifa.
Nimekua mfatialiaji mzuri wa blog yako na nimejifunza mengi hivyo na mimi leo nikaona si haba nikiomba ushauri kutoka kwako na kwa wasomaji wengine. Mimi ni mke na mama wa watoto 2. Umri wangu ni miaka 31 na niko kwenye ndoa kwa miaka 3! Naomba kufahamu kama ni sahihi kumwambia mume atumie kinga endapo atahitaji au nitahitaji kufanya nae tendo la ndoa.
Na hii ni kwasababu unaona dalili za kuwa mume wangu ameanza kuchepuka. Sababu zilizopelekea kuhisi hivyo ni kuwa mume analala mzungu wa nne! Hataki kabisa niguse simu yake na hata nikibahatika akiwa kalala sikuti chochote kwenye inbox wala call history zaidi ya zinazonihusu mimi!
Pia kuna siku amerudi na alama kwenye bega wazungu wanasema 'love bite' huwa anakawaida ya kukaa na vest akiwa home lakin hii wiki alikua anavaa tshirt had wakat wa kulala. Na akirudi anakua na uso wa mbuzi yaani ameshajihami. Nikimsubiri chumbani nimuulize anakua ana panic na kuishia kususa!
Kwa kifupi mawasiliano yetu ni hafifu sana. Nimegundua ni mtu anayependa 'ndio bwana' kwa kila kitu hii inakua ni ngumu kwa upande wangu kwa sababu maisha ya kihalisia hayapo hivo.
Naomba ushauri tafadhali.
*************
Dinah anasema: Ni njema, Ahsante. Shukurani kwa ushirikiano.
Mwanamke! Umepata zaidi ya ushahidi kuwa Mumeo sio mwaminifu, huna haja ya kumuuliza bali ni kumuwahi kwa Talaka.....Kimbiaaaa (Well mimi ndio ningefanya hivyo). Haya mdada, ni kitu gani hasa kinakufanya uendelee kukaa na huyo mwanaume kama Mumeo ambae hana utu, hakuheshimu wewe na watoto wenu,kakudhalilisha? Usiniambie watoto....!!
Achana na mambo ya "nikitaka ngono" jipe mkono....yeye akitaka Ngono mtolee nje ikiwezekana ita Polisi. Halafu unawezaje ku-even fikiria kufanya mapenzi na mumeo wakati unajua kwa uhakika analala na mwanamke mwingine? Huoni kinyaa?!!
Ni sahihi kutumia Condom na mumeo (moja kwa moja ngono, hakuna kuwekeana vidole, kunyonyana n.k.) ikiwa unahisi anatereza nje ya ndoa yenu mpaka atakapopimwa na kupewa all clear!!hiyo ni kama unadhani kufanya mapenzi na mumeo asie thamini utu wako wala ndoa yenu ni muhimu sana kwako mpaka unataka kuendelea kulala na a cheater basi ni vema mtengane ili uwe huru ku-date mtu mwingine ambae ni muaminifu(na kutumia Condom) kuliko kuhatarisha maisha yako na huyo Mumeo asiejali afya wala hisia za mkewe na watoto wake.
Tuone wengine watashauri vipi, mimi nakushauri ukimbie....
Kila la kheri!
Mapendo tele kwako...
Comments
Wanandoa ndio wanaoongoza kwa maambukizi ya HIV kwasababu wanadhani sio haki kutumia Condom kwa mume au mke. Ushauri wangu hapa ni wewe kutofanya mapenzi na Mumeo mpaka akubali kujieleza na kukuhakikishia kwa vipimo kuwa amekuwa mwaminifu.
Pia angalia uzito wa maisha yako kama mama na maisha yako kama Mke. Kwanini unaendelea kuishi na mwanaume asiekuheshimu na kukuthamini, hataki kuwasiliana nawe na anakutenga na kulala na mwanamke au mwanaume mwingine? Hii ni 2014 huitaji kuteseka kwenye ndoa ambayo inatishia maisha yako. Una haki ya kufurahia maisha, una haki ya kuheshimiwa, kusikilizwa na kuishi huru kwa faida ya watoto wako.