Zawadi ya kumpongeza Mke!

Da Dinah hi,
Pole na majukumu yako ya kila siku na hongera kwa moyo wako usio na kinyongo kwa ushauri katika kuboresha Penzi langu na laazizi wangu, MUNGU AKUBARIKI SANA KWA MOYO WAKO HUO.



Nimekuwa kwenye mahusiano na Mdogo wako wa kike kwa miaka takribani mitano na tuna umri unaokaribiana na tumeishi kwa upendo na Amani.




Kila mtu hubuni mbinu mpya ya kumshika vilivyo mwenzake ili afurahie umbaaji wake Mola kwa bidii na maarifa.



Kwa upande wangu huwa sipendi kwenda kumuona nikiwa mikono mitupu hasa nikiwa nina nafasi ya pesa mf. humnunulia Viatu kama Magauni, Nguo za ndani Peremende na kila aina ya zawadi ambayo moyo wangu utaniongoza.



Mke wangu huwa anashuru sana bila kujali ukubwa wala udogo wa zawadi kwa kweli namshuru MUNGU kwa hilo!



Sasa ni kwamba ameshika Mimba nami nataka nimpongeze kwa hatua hiyo je! ni zawadi gani ambayo wewe ungenishauri nimpe ambayo wanawake wengi huwa mnapendelea nawe ukiwa mmoja wapo?


Ni hayo tu kwa leo.


************

Dinah anasema: Hello! Ahsante kwa kujali na shukurani sana kwa ushirikiano.



Hongera kwako na kwa mkeo kwa kuwa wazazi wa kijacho, Mungu awakuzie na kuwalinda.


Mmh! Hilo litakuwa gumu kwani wanawake tunatofautiana, pia mimba zinatofautiana.



Mimi nadhani zawadi ambayo kila mwanamke mjamzito angependa kuipata ni Uelevu na uvumilivu (akinuna, akilia n.k), Ushirikiano(kwenda nae Kliniki n.k) Huruma(maumivu,kutapika n.k), Usaidizi na kuwa karibu kila anapokuhitaji.



Katika hali halisi sio zawadi bali ni jukumu lako kama Mume wake.


Vinginevyo Mnunulie nyumba au Shamba....

Kila la kheri!
Mapendo tele kwako...

Comments

Anonymous said…
ningemshauri amnunulie gari la kutembelea kama hana, kama analo aende dukani akataute magauni ya wajawazito amnunulie, amtafutie na viatu flat vingi design mbali yaani usitoke kwenye mstari kaa humu humu kweye mahitaji ya mama mjamzito naamini atafurahi sana, halafu angalia vile vitu anavyopenda ndio uwe unamletea, uongeze upendo sana.