juu ya mahusiano.
Nina mchumba ambaye tumemaliza chuo pamoja na ananipenda sana tena kwa dhati na pia tunatarajia kufunga ndoa Novemba 2014.
Shida niliyonayo kwa mwenza wangu huyu wa kike ni mwembamba sana, nami nikikutana na vibiti namba 8 nachanganyikiwa kabisa.
Je kunahaja ya kubadilisha mwelekeo wakati huyu mpenzi wangu ananipenda sana na teyari kanitambulisha kwa nduguze.
Swali la pili nikiwa naye huyu mpenzi wangu na kuishi naye kama mke umbo lake litabadilika na kuvutia macho yangu?
Maana watu wengine hudai kuwa
mwanamke mwembamba pia flat akiolewa anaweza kuwa na figure nzuri
baadaye hasa akizaa. Samahani nitoe ktk utata huu.
****************
Dinah anasema: Aii Madam tena? Tafadhali niite Dinah inatosha....
Kutokana na maelezo yako inaonyesha kuwa huna mapenzi nae na wala hakuvutii kwa asilimia zote.
Umemchumbia kwa vile kupendwa feels good au kwa vile kakutambulisha kwao hang on!!! Mchumba wako ni mwanamke alafu yeye ndio kakutambulisha kwako?!!
Ni kweli baadhi ya wanawake kama sio wote wakishika mimba huongezeka na wakizaa hurudia maumbile yao ya awali (wakitaka iwe hivyo).
Hiyo sio guarantee ya Mchumba wako "kuota" makalio na kiuno chembamba ili kutengeneza namba Nane ikiwa hana asili hiyo.
Chunguza wanawake upande wake na wa Baba yake, ikiwa kuna waliojaaliwa basi uwezekano ni mkubwa umbo lake linaweza kufanana. Upande wa mama sio mara zote Binti anachukua Umbile (Baba ndio husababisha mbegu za mtoto wa kike).
Ni vema umekuwa muwazi kwangu, ila ingependeza zaidi kama ungekuwa muwazi kwake na kumwambia kuwa unapenda umbile la namba Nane na sio namba Tisa ikiwa anamatiti makubwa na ni bapa kama ulivyosema au namba Moja (mwembamba kote).
Au uvunje uchumba kwa kumueleza kuwa unahisi kuwa haupo tayari kuoa kwani bado unatamaa.
Weka wazi kwamba ukiona mwanamke mwenye umbile la Namba nane unaheuka na kulitamani.
Mwambie mkifunga ndoa unaogopa kuwa utam-cheat (obviously).
Kama huna moyo wa kuvunja moyo wa mwenzio ana kwa ana basi tumia watu waliopeleka Mahari(walioenda kuchumbia) kwao au ndugu zako ama mtu yeyote ambae anafaa kwenda kuvunja Uchumba.
Sio sahihi kufunga ndoa na mtu kwa kigezo cha yeye kukupenda kwa dhati, wakati hakuvutii na wala huna mapenzi ya dhati kwake.
Fanya, haraka kabla muda haujafika na watu kuanza vikao vya Ndoa.
Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...
Comments