Shoga kipenzi hajui nimezaa na BF wake, nimwambie au niuchune?

Habari za kazi dada, nasoma makala zako sana, nna tatizo nahitaji
ushauri wako.

Nimekuwa na rafiki yangu wa muda mrefu sana kama best friend tunapendana sana kama miaka 4, ana mpenzi wake ambaye nilimfahamu
kupitia yeye, tumezoeana kupita kiasi.


Nilianzisha uhusiano wa siri na shemeji yangu kwa muda wa miaka 3 na
mpaka sasa nimezaa nae mtoto 1 na anamhudumia mtoto.

Rafiki yangu hatambui kama nimezaa na mpenzi wake mpaka sasa na pia bado tunawasiliana sana tu.

Mzazi wake baba wa mtoto anajua mimi ni rafiki wa mwanamke na nimezoeleka sana na mzazi wa mwanaume, anajua nimezaa lakini hatambui kama nimezaa na mtoto wake.

Naumia sana kila nikifikiria hili kwani natambua nimemkosea sana huyu rafiki yangu sielewi siku akijua haya yote itakuaje. Naomba ushauri dadangu.

*************

Dinah anasema: Habari ni njema na shukurani sana kwa ushirikiano.


Duh! Aren't you fast?!! Baada ya mwaka tu ukajisevia mpenzi wa mwenzio....alafu watu wananishangaa kwanini sina marafiki na inakuaje sina hata best friend!

Wala humpendi na hujawahi mpenda rafiki yako bali unadhani kuwa unampenda. Ungekuwa unampenda usingezoeana na Mpenzi wake hivyo na ungeheshimu mipaka ya urafiki na upendo kati yenu.

Basi ungetumia kinga usishike mimba angalau (labda angekusamehe)....au ilikuwa mambo ya PMU(Pata Mimba Uolewe), ukampiku mwenzio eti?!

Je bado unaendeleza uhusiano na huyo bwana au uhusiano umeisha baada ya Mimba....huyo bwana nae the shenzi kabisa.


Mwambie huyo mwanaume amuambie Mpenzi wake (rafiki yako) alichokuwa akikifanya kwa miaka yote 3 mpaka kuzaa na wewe.

Au wewe mwenyewe umwambie moja kwa moja kuwa kwa miaka 3 uhusiano wake ulikuwa wa watu watatu, yaani wewe, yeye na huyo mwanaume.

Usimwambie katika hali ya kujidai au kumnanga, kumbuka umemkosea mwenzio sana tena SANA.....go to the point...Mf: "nimeficha siri kwa muda mrefu, nisamehe kwa hilo! Huyu mtoto nimezaa na bf wako".

Na huko kwa mkwe wala usijipendekeze, mwenye kwao akitaka mzazi wake ajue basi atamwambia.

Fanya haraka ili mwenzio afanye uamuzi muhimu wa maisha yake kuliko kuendelea kupoteza muda na ninyi wanafiki.


Kila la kheri!
Mapendo tele kwako...

Comments

Anonymous said…
Aah jibu mujarabu! Nimelipenda hili jibu! Limegonga mulemule kwenye ukweli.Dada We noma kweli umewiva kwenye mambo ya mahusiano embu nipe no yako ya simu nikutafute!! Naona utanisaidia mambo mengine hatuwezi kuyaweka hapa...!
baraka80@ymail.com said…
Sasa hapo lengo lako lilikua nini? Mwambie huyo shosti yako akutoe macho maana hujafanya fair.Mimi ni mwanaume sijapenda hio tabia,hapo wote mnamakosa, wewe na huyo bf wa shosti yako,kwanini asimwambie tu binti wawatu aendelee na maisha yake? coz hata akimuoa bado yaelekea utaendelea kujirusha nae.Jaribu kujiweka kwenye nafasi ya shosti yako uone utamu au uchungu wa hio kitu, too bad.
Anonymous said…
Duh wewe mdada kiboko,ningekua mimi nikijua nakutoa macho,ndo nyie mnaomwagiwa tindikali,what was you thinking to betray your friend,tell the truth si we ndo umeyavukia nguo yaoge.
Anonymous said…
Dina nayapenda majibu yako sana. Hupepesi macho hata, jembe waliita jembe na kisu kisu. It is true hyu binti hampendi kabisa hyu anayemwita rafiki yake. Na nimnafiki wa kumwagiwa mafuta ya taa na kiberiti cha moto
Anonymous said…
Uwiii nimeumia mara dufu jamaniii, kwanini sisi wadada lakini????? why?
Tafadhali nyie wawili wanafiki mumwambie huyo mwenzenu jamani maana mnazidi kumpotezea muda tu jamani.