Nimtokee bila taarifa!

Da dinah shikamoo.! Pole na majukumu ya kusaidia mapenzi ya watu kila
uchao!

Da dinah nina age ya 22 nipo kwenye relationship na mwanaume kama miezi 3 saizi tatizo limeanza baada ya mimi kuwa mbali kama 3weeks hivi.


Nahisi anamwanamke zaidi yangu kwasababu hata namna ya kuongea
inanitia mashaka.

Kuna wakati akiongea na mimi anaongea vizuri sana but sometimes nikimpigia simu anaweza akaongea haraka haraka and mda huo najua yupo nyumbani kwahivo hayupo bize.


Nkimuuliza mbonahivo upo na nani? anakata simu then anafunga simu kabisa, kesho yake anaweza kuniambia simu imezima haikuwa na chaji au hapendi maswali yangu kwani
naonyesha kama simuamin.

Da dinah nataka nimfanyie suprise visit, sababu nimesharudi safari naye hajui kama nipo hapa mjini ili nijue kama kweli anakua bize au maswali yangu yanamkera na hamna kingine.


Je hii suprise ndio itaua kabisa mapenzi au nifanyaje da dinah.


**********


Dinah anasema: Marhaba mrembo, hujambo?


Haka kaumri huwa kanasumbua sana, high expectations na hofu nyingi kwenye uhusiano kabla uhusiano haujawa UHUSIANO.

Huyo nae wa wapi? Au ni utoto unaulizwa swali....unakasirika na kumkatia mtu simu...so rude!

Miezi mitatu ni mapema mno kuanza kumfuatilia bf....sana sana utakuwa unaumia na kupoteza muda kuwaza na kuwa paranoid kuhusu bf ambae uwezekano wa kuwa mumeo ni mdogo au haupo kabisa.

Sina maana usiwe na bf, la hasha! Bali ni kutomchukulia huyo mjamaa kuwa ndio atakuwa mumeo na badala yake enjoy ujisia wako kama mwanamke na ukumbuke kutumia Kinga ili usikamate Mimba au magonjwa ya zinaa.

Umri huu ndio mzuri kuanza kufurahia uanamke wako, kuzingatia masomo kama upo Chuoni au kuanza kutafuta namna ya kujikomboa kama mwanamke, sio kupoteza muda kuwaza na kuwazua kuhusu bf.

Hakuna sababu ya kumtokea kwake bila taarifa, isipokuwa ukipata nafasi zungumza nae kuhusu tabia yake ya kukukatia simu au kukuzimia kabisa it's kind rude.

Nae (kama ana kerwa) ataweka wazi kuhusu tabia yako ya maswali mwengi ya kijinga/kitoto....upo wapi? Upo na nani? Mbona unaongea hivyo kuna mtu hapo?....hivi unanipenda kweli n.k

Wote kwa pamoja mfanye mabadiliko ya tabia zenu kwa wakati wenu.


Nakubali maswali mengi yanaweza kuudhi hasa kama mtu kachoka au ana-stress za mizunguuko yake, lakini hiyo sio sababu ya kumkatia mtu simu na kumuacha kwenye limbo!



Kwa sasa mchunie (tufanye umekasirika), subiri mpaka yeye akutafute. Ni ngumu sana kama unampenda lakini itakusaidia huko mbele.


Wewe mwanamke bwana, unawindwa....hawindi. Hakuna sababu ya kupigapiga simu kila mara


Uhusiano sio lelemama, na at 21! Safari ni ndefu...


Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

Comments

lajk@ymail.com said…
uwe na ubavu wa kuhimili utakacho kikuta maana unaweza zimia.By the way uhusiano bado mchanga sana sidhani kama unahitaji kujihangaisha hivo kwa sasa pengine bado anachambua yupi ni yupi, relax kama wako ni wako kama sio wako sio wako hata kama ushampa utamu.Watu tushachukuaga flight unalipa pounds kibao ili uje ufanye surprise unakuta madudu, ptuuuu mapenzi ya siku hizi kamali ukipatia umepatia na ukikosea umekosea, so be careful usibweteke na neno baby wala nitakuoa hizo ni gia za kupatia k kwasisi men hehehe hio inaitwa mambinu plus

lajk@ymail.com