hafikirii maisha.
Kila nikimshauri mambo ya maana huitikia lakini kutekereza hatekerezi. Tumejaaliwa mtoto Mmoja muda mwingine nawaza labda mwenzangu ana mwanamke mwingine.
Kila tukikubaliana tuweke pesa ili tuweze kufanyia vitu vya maana mwenzangu anakubali ila
utekezaji hamna naomba ushauri wako dinah.
************
Dinah anasema: Habari there!
Labda vitu vya maana na muhimu kwako, kwakwe sio hivyo....si unajua watu tunatofautiana!
Ila kuna wakati tofauti inawekwa pembeni na kukubaliana kufanya mambo kama Team(mke na mume) kwa faida yenu kama familia.
Kabla hatujamshutumu kuwa na mwanamke mwingine nje ya ndoa yenu....je? Unajua kipato chake na kama ndio kipato kinaendana na matumizi yenu?
Je? Wewe unashughuli inayoingiza pesa (kazi/biashara) na je? Kipato chake JUMLISHA Kipato chako TOA matumizi muhimu (Pango, Bills, Chakula, Mtoto) mnabaki na kiasi gani?
Inabidi mkae chini na mzungumze tena kwa kuhimiza na sio kwa hasira (usichoke wanaume wengine wanachelewa kukua kiakili)....muanze kubajeti matumizi yenu ili kupatikane pesa ya kutunza kwa ajili ya mambo muhimu kwa wote kama familia.
Mkubaliane kuwa mwenye Kipato kikubwa afanye arekebishe mahitaji yote ya mwezi na mwenye Kipato kidogo atunze (weka Akiba Benki) kwa ajili ya Emergencies na mambo mengine ya maana.
Mkubaliane kwenye matumizi yenu ya kila mwezi, mfano kwa miezi 3 hakuna luxuries (pombe, gauni jipya n.k) na senti itakayotunzwa muda huo itumike kununua Sementi...kwa mfano!
Kama mwanaume ni mzembe kwenye utekerezaji mwanamke inabidi uchangamke na umsukume kwa ushauri na wakati mwingine umuongoze au kumuonyesha mifano halisi.
Ikishindikana basi jaribu kubana matumizi kwenye pesa za matumizi anazokupa kila Siku/Mwezi/Wiki na utunze kibindoni.
Watu tumetofautiana kimalezi, huwezikujua alikulia mazingira gani....si unajua wale watu wa "kila mtoto anakuja na bahati yake, na tutajua hukohuko muda ukifika" sort of people.
Pamoja na kusema hivyo, kama hujui Kipato chake na hakuna cha maana anachokifanya kwa familia yake (wewe na mtoto) basi inabidi utafute ukweli wa wapi anapeleka kipato chake kila mwezi.
Ni mumeo, ninyi ni mwili mmoja lazima ujue kipato chake na yeye ajue chako eti!...Kama hujanielewa tafadhali usisite kunicheck tena.
Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...
Comments