Ananipenda but ni Jobless....

Da Dinah mie ni msichana nipo katika mahusiano ya mwezi mmoja sasa na huyu boyfriend wangu but kinachonkira ni yeye kuaw jobless.

Kutwa yuko home, I know love is not money but money is the part of love ukitaka kustawisha penzi tumia vyote.

Sijajua ni kwanini hajishungulishi hata kutafuta kazi ya kujishikiza tangu mtokeo ya form 4, 2011. Sijajua ni wazazi au yeye kwasababu nikimuuliza huwa hanielezi anapotezea.

Mie nampenda lakini sidhani kama kutakua na future nzuri kati yetu so nifanyaje?


He is 22 and am 24 and am student at_______(Dinah kahifadhi).


************


Dinah anasema: Ahsante kwa ushirikiano.


Aliyekuambia kuwa "money is the part of love na ukitaka kustawisha penzi tumia vyote" ni MUONGO.


Pesa ni muhimu maishani lakini sio sehemu ya mapenzi. Huitaji pesa ili kumpenda mtu....unahitaji hisia (Moyo/Akili/Mwili) na Utu.

Ukitaka kustawisha uhusiano wa kimapenzi unahitaji mambo kibao kama vile Mapenzi ya kweli, Ushirikiano, Heshima, Uelevu, Uvumilivu, Maelewano, Mawasiliano, Uwazi, Ukaribu, Usikivu,Huruma,Usafi nakadhalika....pesa is none of them.

Unapomuona mtu na kuvutiwa nae kisha kumdondokwa kimapenzi huoni Bank account yake, huoni kazi aifanyayo wala uwezo wa wazazi wake. Unamuone yeye kama mwanadamu sio?!! Anyways...

Ndani ya Mwezi tu umeisha anza kuwa pushy.....wala hujamjua kijana wa watu vizuri, hujui hali ya kimaisha/kiuchumi aliyonayo na mipango yake huko baadae baada ya kumaliza Sekondari 2011.

Usikute anakupotezea kwavile bado hajakuamini, I mean...ndani ya mwezi mmoja nani anaweka kila kitu chake wazi?

Isitoshe wewe ni nani kwake mpaka uanze kumuuliza na kumsukuma atafute kazi? Unless otherwise anakuomba pesa....still huna mamlaka ya kumsukuma akatafute kazi baada ya kuwa nae mwezi mmoja tu.....subiri mwaka hivi labda!

Kutokana na maelezo yako inaonyesha huyo bado ni mtoto ambae yupo chini ya wazazi wake....sana sana anataka ku-have fun na wewe na sio kukufanya uwe wa kudumu (kuwa na future).

Unajua wanawake huwa tuna-mature kiakili haraka kuliko baadhi ya wanaume, mwanamke wa miaka 22 ni tofauti kabisa na mwanaume mwenye umri huo(kiakili).

Kama wewe unaumri wa miaka 24 na bado ni mwanafunzi, yeye wa miaka 22 pia anahitaji Elimu zaidi ya kumpa ujuzi ili kumuwezesha kufanya kazi au kuajiriwa.

Kama pesa ni muhimu sana kwako au kwenye uhusiano wowote utakaoingia basi ni vema umuache mtoto wa watu, maana asijeshindwa kukuridhisha kipesa ukamuweka kwenye "remix" na Njemba wenye mahela.

Tangu umeweka pesa mbele ni vema uongeze bidii kwenye Masomo yako, umalize upate ajira kisha uanze kujichanganya na Vijana ambao tayari wapo kazini au wanabiashara(wanapesa) na wakubwa kiumri angalau kuanzia miaka 26 kwenda juu.

Achana na watoto wa Shule/Chuo, ukishika Mimba mtapelekana wapi?

Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...

Comments

Anonymous said…
Hey, dada!

Hakuna uhusiano kati ya mapenzi na pesa. Unahitaji kumpenda jinsi alivyo bila kuangalia uwezo wake wa kiuchumi. Itakuwaje ukimkuta mvulana ama mme mwenye kuwa na kazi na pesa, ila asikupe mapenzi ? Vivyo hivyo kuna wavulana wanaopenda wasichana wenye kutoka familia zenye kuwa na pesa, huko wakifikiri kwamba watarithi pesa za wakwe wao. Huo ni udanganyifu mkubwa sana.

Kwa kweli pesa ni muhimu kwani tunazihitaji kwa kufaulu mahitaji ya kimaisha. Ila wewe na mpenzi wako munaweza kukaa na kuongozana hata mupate njia ya kuzitafuta hizo pesa pamoja. Na mimi kwa upande wangu naona kwamba zile pesa watu wanazo sipata wakiwa pamoja ninafaa sana kuliko zile ulizozikuta. Lakini hayo ni mawazo yangu tu.

Ila neno la mhimu tu ninalopenda kulisema ni : umpende yeye njisi alivyo.

Ni mimi Lambert.