blog yako!
Hakika unatoa elima endelevu kwa watu mahsusi. Dada Dinah ni takriban miezi 8 tangu Mwenyezi Mungu atujalie na
kutupatia zawadi ya mtoto kidume (kiume) mwenye umri wa miezi nane (8)
sasa.
Kila nikijaribu kumchezeshea na kujaribu kuamsha hisia zake
yaani hakuna response yoyote na haoneshi dalili zozote za kuhitaji
kupeana tendo la Ndoa.
Yawezekana ndivyo ilivyo kwa mama mzazi anayenyonyesha na kwa kuwa ndio mara yangu ya kwanza naingia kwenye Ndoa pengine ni hali ya kawaida waweza kunisaidia katika hili.
Mke wangu hajisikii kufanya tendo la ndoa na zaidi hajapata siku zake
tangu alipojifungua hadi hii leo miezi nana na ushee....!
Alishapima mara kadha wa kadha kujua labda kuna mimba au la, kwa kweli hana mimba.
Tumejaribu kumwona Dokta naye hajatupa sababu zaidi ya kutuambia ni uwezekano wa mabadiliko ya diet na hali ya hewa. Pengine unaweza kunisaidia zaidi labda utueleze tatizo hili linatokana na nini?
Mtoto wetu ni wa kwanza na katika ujana wake hajawi kushika mimba. Mimi nilihisi labda kuna tatizo huko ujajani kama kuna chochote huko nyuma labda liliwahi kutokea! Kwa maelezo hakuna!
Tunaomba msaada wako.
***************
Dinah anasema: Huyo Dakari nae eti hali ya hewa na Diet wakati mtu katoka kujifungua.....afukuzwe kazi khaa!
Hiyo ni hali huwatokea wanawake wengi baada ya kujifungua inaweza kuondoka baada ya miezi mitatu mpaka Mwaka, inategemea na mwanamke husika maana wanawake tumetofautiana.
Kuna sababu nyingi ambazo zinaweza kumfanya mwanamke apoteze hamu ya kufanya mapenzi ila kuu ni UCHOVU siku zile za mwanzo (unaruhusiwa kufanya ngono baada ya Wiki sita a.k.a 40 tangu kujifungua kiasili).
Hebu pitia topic hii
http://dinahicious.blogspot.co.uk/2008/10/ngono-baada-ya-kujifunguazaa-kiasiliii.html?m=1
Ili niweze kuelewa tatizo liko wapi ni vema kama Mkeo akanieleza mwenyewe kama mwanamke ili niweze kumpa mbinu za kurudisha Mojo.
Maana kuna wakati mtu unahisi kama vile umepoteza "ze mojo" ya kunanihii kumbe ni Uchovu + Mapenzi kwa mtoto = Baba take back seat.
Kuhusu Hedhi ni kawaida kwa Mama anaenyonyesha kutopata Hedhi mpaka atakapo anza kumuachisha mtoto kunyonya.
Kila la kheri.
Mapendo tele kwako...
Comments
Kuzaa kunamfanya mwanamke abadilishe priority anahisi mtoto ndio muhimu na wewe mtu mzima utajisaidia mwenyewe lakini ukimsaidia vijishughuli utaona unaanza kupata attention am just saying!
Daktari mtoto anapita sehemu inayotumika kufanya ngono huoni kuna uhusiano hapo?
Muulizaji toa attention ya kutosha kwa Mkeo maana kuzaa kunaweza kumuathiri mwanamke kiakili na kisaikolojia pia. Anahitaji ukaribu wako, usaidizi na kuhakikishiwa kuwa unampenda na kumjali sio kudai tendo tu.