Simjui mwenye Mimba!

Dada Pole na Majukumu, 

Sorry kwa yaliyo nikuta kwani unaweza kuona kama sina heshima kama mtoto wa kike.

Ni hivi nilikua na mpenzi wangu kwa mwaka mzima ila akawa hana mpango wa kunioa nikaanza kufanya mpango nipate mtu ambaye anaweza kujenga familia na yeye.

Kilichofuata sikumwacha mpenzi wangu wa zamani nikawa nadate na wote, sasa nimepata UJAUZITO na sijajua ni wa nani kabisa nachanganyikiwa sana.

Kwani nilipata Hedhi tarehe 10.12.2013, ndiyo ilikua mwisho wa kwenda hedhi. Ila tarehe 21,12,2013 nililala na kitu kipya hadi Asubuhi.

Nikarejea 22 kwetu. Tarehere 24 mkesha wa Xmas nikakesha na wa zamani hadi Asubuhi, najua ni tabia mbaya ila ilibidi kwa sababu mpenzi wangu wa zamani aling'anga'nia nikesha nae.


Sasa January sikuona siku zangu nilipo pima ni mjamzito. Je hapo nani anaweza kuwa ndiye mwenye mtoto.

Nimewaza sana nimekosa jibu sasa nina ujauzito wa miezi miwili.

Naomba ushauri.

**********************

Dinah anasema: ahsante, ila ungekuwa karibu ningekuchapa viboko za miguuni akyanani vile. Khaa! Kuna wanawake wa Bongo mnaujasili wa ajabu na wa kijinga....unaMix wanaume na kwa USHENZI hutumii Kinga!!


Kama ni miezi miwili na ushehe yaani Wiki 9 na siku fulani ni ya huyo Mpya na kama ni miezi Miwili kamili au na siku kadhaa ni ya huyo wa zamani.

Hayo ni mahesabu ya haraka haraka ili kujua mahesabu halisi ni vema kama ungenipatia Mzunguuko wako wa Hedhi je ni wa kawaida, Mrefu, Mfupi au unabadilika kila mwezi.

Hii itasaidia kujua ni tarehe gani kati ya 21-22 au kabla na 24-25 ni lini ulikuwa umepevusha yai....

Mbegu za Mwanaume hukaa ndani kwa muda wa Masaa 72 mpaka Wiki moja, inategemea na ubora/afya za Manii husika.

Sasa kwa vile uliwachanganya itakuwa. Ngumu sana kujua unae share nae Mimba ni nani kwani hatujui "speed" na ubora wa Mbengu za wa kwanza au wa pili kufanya nae ngono.

Mbaya zaidi umewachanganya ndani ya siku chache kati yao.....kwanini usitumie CONDOM jamaniii (*hitting my table*).


Anyway, pole...piga mahesabu tena ili ujue ukaribu wa tarehe za kupevuka na tarehe za kushika Mimba halafu ukifikisha miezi 3 umjulishe unaedhani ndio Mwenyewe, hilo moja.


Pili waambie wote, atakae kubali ndio huyo kwa kipindi hiki cha ujauzito na atakaekataa ndio hivyo tena.


Mtoto akizaliwa fanya utaratibu wa DNA test najua Bongo kwenye Hospitali kubwa Binafsi wanatoa huduma hii.

Vipimo hivyo vitasaidia kujua ukweli halisi na kumpa haki Baba wa mtoto na mtoto husika ikiwa unaamua kuendelea na Ujauzito huo.


Tuone wengine watakushauri nini?
Mapendo tele kwako...

Comments

Anonymous said…
Kutaka familia ni uamuzi wa pande mbili, sio kushtukizwa na mimba wakati mtu haupo tayari. Hao washkaji nao wanachovya tu bila kinga daaaah. Mie nakushauri kaitoe mimba kama huogopi kufa lol.
Anonymous said…
Duh dada umebugi vibaya sana hapo ndio kibaba unalea mtoto asie wako na huambiwi ng'o. Achana nao wote, lea mimba na mtoto akizaliwa waambie wanaume wote kisha mkafanye DNA.
Anonymous said…
Anonymous said.
DNA test ndiyo iliyo na uhakika kuliko Hesabu za mzunguko wa hedhi. Japo ni gharama kidogo lakini dhamira yako itakuwa umempata baba wa kweli wa mtoto wako. Litakalo kuhamgaisha zaidi katika maisha yako yote ni kumsingizia baba wa mtoto wako ambae si wa kweli.
Anonymous said…
mimba ya uyo wa kwanza!
Anonymous said…
ingependeza sana kama ungetulia na mpenzi mmoja, sikushauri kutoa mimba ni dhambi jipange baadaye kupata vipimo vya DNA baada ya kujifungua ingawa kuna uwezekano mkubwa sana wa kumvunja moyo mpenzi wako wa kwanza akigundua kuwa hukuwa mwaminifu na uliingia pekupeku bila kinga,atahofia usalama wake,wako na wa huyo mtoto.
Kirungu said…
Duuuh dada umeniua moyo kabisa huyo wa kwanza kwanini umpe kavu? umempima kwa macho tu ukamkenulia kabisa usiku kucha? Na kama kaathirika ngoma ushapata maana msuguo wa usiku mzima na mashahawa kakumwagia basi tena.Ujue hio ni tabia mbaya saana.zaa tu then go for DNA maana hapo tayari atasingiziwa mtu, hakuna kitu kibaya kama kulea mtoto si wako.Imemtokea kaka yangu kalea mtoto si wake na sasa yuko form 5 only to find out sio mtoto wake yaani baba mtu (infact baba mlezi maana kasingiziwa) mzuka umeisha anamsomesha tu kwani ana uwezo na pia alikua na uhusiano na mama huyo kwa muda mrefu na hawakuoana lkn akimaliza shule achukue time kwani baba mtoto ashajulikana na keshaanza kuleta mbwembwe kibao Yaani nabaki njia kuu!!!
Anonymous said…
Huu mtihani ila nakushauri usubiri tu DNA. Ila kwa mahesabu ya mzunguko, kuna probability kubwa akawa the brand new


Last periods started on 10.12.2013

If it's a 28 days cycle then danger days

From 21.10.2013 To 26.10.2013


Huyo wa tarehe 21.12.2013 ndie aliyewahi that is kama mbegu zake ziko poa