Katika mahusiano kumekuwa na ups and downs nyingi katika miaka yote nilikuwa namsisitiza atoe Mahari lakini wapi but mwaka juzi ndio alienda kujitambulisha rasmi na Mahari akatoa akaahidi tutafunga ndoa baada ya miezi tisa toka alipotoa Mahari.
Lakini sasa umepita mwaka na ushee hamna kitu, kila nikimwambia ananiambia gharama ngoja nijipange.
Nikimshauri tufanye simple basi hataki na Kanisani kwenyewe kituo cha polisi sasa namuuliza hiyo ndoa tutafungia wapi kama Kanisani hauendi?
Mimi naenda ila ni dhehebu tofauti. Kinachoniumiza ni hivi sasa nina Ujauzito wa pili lakini mwenzangu ndio kazidi kubadilika nimemshika na sms za mapenzi mara tatu.
Ukifungua whatssap yake ndio utalia ni wanashushana kwa sms na video clips lakini namuona mwenzangu haoneshi mshituko kuwa amekosea.
Mara ya kwanza aliniomba msamaha sana ila wakarudiana tena nimekuta sms tena za mwanamke mwingine nikachukua simu nikampigia huyo mwanamke cha ajabu na kipigo nikapigwa.
Sasa hivi ananiambia wameshaachana lakini bado huyo mwanamke huyo anapiga simu kwake nimetafuta njia yoyote ile ya kuiblock hiyo namba ya mwanamke lakini mwenzangu haoneshi ushirikiano anachukulia simple tu.
Imefikia hatua wakiwa wanawasiliana anajirekodi kabisa, nimeona juzi nimeumia sana ili hali sasa ivi nina Mimba ya miezi saba.
Kila nikimuuliza ananiambia nimeshaachana naye. Huu ni mwaka wa tatu toka tumepata ajira yeye na mimi wote tunafanya kazi ila mie nipo Wilayani yeye Mkoani hivyo tupo mbali kidogo ingawa najitahidi kila weekend naenda lakini bado akaniambia hayo yote yanasababishwa na me kuwa mbali hivyo niwe naye karibu muda wote.
Sasa hapa nilipo sielewi niache kazi nimfuate ndio itakuwa suluhu au basi tuaachane tu nianzishe maisha mapya?
Najitahidi sana kumfanyia mazuri kumpa suprise kama zawadi mbalimbali lakini ndio hivo .
Kwa upande wa mapenzi ananipa vizuri kabisa tena bila kinyongo na huwa ananisifia sana pia kwa upande wangu kwani yeye ndiye aliyeniingiza kwenye Ulimwengu huu kwani mwanzoni nilikuwa mgeni sana maumivu kila tendo.
Hiyo yote ilikuwa kwasababu ya ubikira lakini siku hizi ameappriciate nafurahia naye nayeye anafurahia but tatizo ni hilo hapo juu sijui nimemkosea wapi.
Naomba ushauri wako mapema sana kwani nipo kwenye lindi kubwa sana la mawazo.
Asante
*****************************
Dinah anasema: Pole sana kwa yote unayokabiliana nayo. Kwanza kabisa USITHUBUTU KUACHA KAZI KUMFUATA huyo mwanaume...kamwe kamwe I beg you!
Humuhitaji Mwanaume bali Unamtaka mwanaume maishani mwako ili kukuongezea au kukupa furaha, kukupa ushirikiano, kusaidiana, kushauriana na pengine kuanzisha familia na kuitunza.
Kutokana na maelezo yako inaonyesha kuwa wewe ni Mwanamke unaejiamini ila Miaka sita ya uhusiano wenu na yeye kuwa mwanaume wako wa kwanza ndio vinavyokufanya uendelee kuvumilia visivyovumilika.
Mwanaume hana Mapenzi ya kweli, hana Utu, hana Huruma wala Shukurani, iweje wewe ufanye yote hayo kwa ajili yake....mpaka kumsamehe alipokusaliti na kukupiga na bado anataka uache kazi kwa ajili yake!!
Hajasema wazi kuwa Uache kazi lakini aliposema uwe karibu nae inamaana hiyo, acha kazi unde huko aliko.
Kuachana/Talaka sio kitu ambacho huwa napenda kushauri, lakini kutokana na matendo ya huyu Bwana (Cheating haisaameheki kwangu) hakika nitakushauri uchukue hatua hiyo.
Hapo hajafunga ndoa na wewe hakuthamini wala kujali hisia zako, sasa "akimilikishwa" Kisheria si ndio utakoma kabisa!
Mmekutana wewe ukiwa na miaka 22, sina hakika na umri wake ila nahisi alikuwa Chini ya miaka 30....katika umri huu wanaume wengi huwa hawajatulia kichwani, hawako tayari kuoa japo wanadhani kuwa wapo tayari.
Huenda alidhani amekupenda lakini baadae(baada ya kukua, akagundua kuwa hakukupenda kivile bali alikutamani tu).
Wewe ulimpenda na huenda uliamini unapendwa au utapendwa zaidi kwa vile amekukuta Bikira (kiuweli hii haiongezi mapenzi zaidi ya kufurahisha Ego ya mwanaume).
Ikiwa mwanaume huyo ameshindwa kubadilika ndani ya Miaka mitatu tangu umsamehe ni wazi kuwa hatobadilika daima na utaishia maisha ya taabu kihisia.
Kabla ya uamuzi wowote Jiulize maswali haya:-
Nini muhimu katika Maisha yako? Kuolewa na huyo mwanaume na kuendelea kuishi maisha yaliyojawa na Hofu, huzuni, maumivu ya hisia na mawazo?
Au Kuishi kwa amani na furaha ukiwa peke yako na watoto wako?
Kumbuka happy mummy, happy kids. Lolote utakalo amua hakikisha watoto wanakuwa na uhusiano mzuri na Baba yao.
Tuone wengine watakushari nini....
Kila la kheri!
Mapendo tele kwako...
Comments
Muache na maisha yake, nenda ulee watoto wako na ipo siku utakutana na mwenye mapenzi na kujali kuliko huyu wa sasa.
Maisha ya siku hizi Wanawake tunaolewa na Kazi zetu wanaume ni luxury tu, hatuwahitaji ili kuishi lakini tunahitaji kipato au kazi ili kuishi.
Kabla hujaachana nae weka sawa masuala ya Matunzo kwa watoto. Nenda Ustawi wa jamii kwa ushauri zaidi.
Lakini mimi ningekushauri uwe single mum bila kuwapa watoto baba mwingine asijekukutesea watoto. Kuwa tu na uhusiano na kiserengeti maisha yaendelee.