Je Mwanamke yupo kwa ajili ya kupendwa?

Nimepitia blog yako imenifundisha mengi keep it up! Unasaidia jamii kwa kweli ktk masuala ya ndoa.


Mi ninakijiswali kidogo je mwanamke anapenda au yeye yupo kwa ajili ya kupendwa tu?

*********************

Dinah anasema: Ndio mwanamke anapenda kama ambavyo mwanaume anapenda, tofauti ipo kwenye kutongoza....mwanamke hatongozi kama wanaume wanavyotongoza.

Mwanamke akikupenda anaweza kutumia njia tofauti "kukutongoza" badala ya kukuambia moja kwa moja.


Kumbuka Mwanamke anawindwa, Mwanaume anawinda, hivyo sio "natural" Mwanamke kumtokea Mwanaume na kumtongoza lakini mapenzi yakimzidi juu ya mwanaume hutumia njia nyingine kushawishi ili mwanaume husika amtongoze (aanzishe)....

Njia hizo ni:

-Kujichekesha kila akikuona.

- Kujipitisha mbele yako mara kwa mara.


-Kukuangalia kwa wizi/haiba.

-Kukusalimia.

-Kuwa mwema kwako.

-Kutokezea mahali unapopenda kuwepo mara kwa mara.

-Kuongeza maringo akikuona....N.k


2) -Je akipenda anachukua hatua gani?

*************************

Dinah anasema: Anachukua hatua hizo hapo juu....

3) -Kwanini Upendo wake hadi alazimishwe ndio apende, je hawezi penda mwenyewe?

**************

Dinah anasema: Upendo wa Mwanamke kwa mwanaume haulazimishwi, inategemea kama anakupenda kabla hujamtokea.....

Kumbuka upendo takes time na unahitaji kumjua mtu vema, angalau kwa mwezi hivi only kama mnakutana kila siku, vinginevyo kuanzia miezi sita.

Huwezi muona tu mtu ukasema unampenda bali unapendezwa nae au unavutiwa na ungependa kuwa nae ili mjuane vema.


Mwanamke ni tofauti na mwanaume, unapomtokea na kumtongoza mara nyingi atahitaji muda.


Ni mara chache sana mwanamke anakubali haraka haraka, hata kama alikuwa anakupenda kabla hujamtokea bado hatokubali hapo hapo.


Mwanaume kama Muwindaji inabidi uongeze bidii ya kumfuatilia na kumshawishi ili akubali kuwa kweli unania ya kutaka kuwa nae au kuanzisha uhusiano nae.

Jinsi unavyo ongeza bidii kumfuatilia (kwa maana ya kumsalimia, kuongea nae kuhusu hisia zako kwake, kupiga stori nakadhalika) ndivyo ambayo mwanamke huyo ataanza kuvutiwa nawe na hatimae kuanza kukupenda.


Kama hakupendi utaona dalili moja kwa moja kuwa haupo akilini mwake....kama haupo akilini (Kuvutiwa) basi ni ngumu kuingia Moyoni mwake (Kupenda).

Mwanamke hubembelezwa, mwanamke halazimishwi...

Kila la kheri!
Mapendo tele kwako...

Comments