Kurekebishana!

Habari ya Sasa!


Unapofundwa, unaelekezwa namna ya "kumrekebisha" mumeo, pamoja na kuwa wewe ni mkewe pia wewe ni "Mama" yake kwani akiendelea kuwa na mwenendo mbaya ambao labda Mama yake hakufanikiwa kumrekebisha akiwa mikononi mwake basi wewe kama mke unachukua jukumu hilo.


Hali kadhalika Mumeo achukua nafasi ya baba yako, ikiwa Baba hakukunyoosha ulipokuwa mikononi mwake basi jukumu hilo achukua mumeo (sina hakika kama wanaume huambiwa hili, lakini wanawake tunapokuwa mafunzoni huambiwa hivyo).



Ikiwa mumeo au mkeo anatabia mbaya, aibu ni yenu wawili na watoto wenu na sio ya Wazazi wenu.....Kila mmoja wetu hupenda/Ombea kupata Mke/Mume/Mpenzi mwema na bora wa kuishi nae, japo sio mara zote unabahatika kumdondokea mpenzi bora atakaekufaa maishani, mpenzi mwenye "values" kama zako, alielelewa vyema na mwenye heshima na adabu(iwe mwanaume au mwanamke, inategemea na jinsia yako).



Kabla hujamdondokea mtu, unaanza na kutamani unachokiona Mf: umbile au muonekano wake, sauti pia inawezekana harufu kama sio mwendo (miondoko yake) na mara chache sifa njema anazotupiwa na majirani au watu wanaomfahamu.



Ukibahatika kumshawishi na yeye kukubali kuwa nawe na kuanza uhusiano, hapo ndio unapokwenda kumjua zaidi na yeye kukujua zaidi. Uhusiano huo utakufanya ufanye uamuzi wa kudharau "habits" mbaya na kuendelea kuwa nae au kuukatisha kwa vile kuna "vijitabia" vyake havikufurahishi na huoni kama unaweza kuvivumilia ikiwa utaamua kuishi nae Daima Milele (only if Milele exists hihihihi)!



Kwa kawaida huwa tunajinadi na "kujiaminisha" kuwa hatuwezi kubadilika kwa ajili ya mtu mwingine, lakini tunasahau kuwa unapokuwa kwenye uhusiano (sio dating stuff, nazungumzia UHUSIANO kuanzia Miezi 6 kwenda mbele) nia na madhumuni ni kuwa na furaha, kupeana imani na matumaini, kusaidiana na kushirikiana katika kila jambo (kimaisha na kimwili) ili kufurahia Maisha yenu pamoja.



Sasa ikiwa kubadilika kwako ni sehemu ya kumfurahisha mwenza wako na kuongeza imani kwenye nyumba yenu, kwanini usibadilike?Huwezi ukaishi maisha yaleyale uliyoishi na watu wengine na pengine yakawashinda na ndio maana ukawa "single" na hatimae kukutana na huyo uliyenae....perhaps!



Mimi binafsi naamini kuwa watu tunatofautiana, sio kijinsia tu bali kiakili, kielimu, kiuelevu, kimalezi, kimazingira n.k.Hivyo basi unapoamua kuishi na mtu mwingine usitegemee yeye kukubali "habits" zako na yeye asitegemee wewe kukubali vijitabia vyake... Hapo ndipo suala la kurekebishana huingia.



Ni rahisi sana kwa mtu ku-pretend kwa muda fulani alafu akisha kuzoea au akiwa comfortable anajiachia...Kurekebishana huko ni kuanzia kwenye vitu vya kawaida mf:

-Matumizi ya pesa, Mmoja wenu anaweza kuwa anafuatilia kila Senti imetumikaje na kwanini (which inaudhi) hasa kama wewe ume-relax kimatumizi....lakini ukiangalia kwa undani utagundua kuwa ni vema kubadili tabia yako ya ku-relax na kutumia pesa vema.


-Ulaji wa chakula, kula huku mdomo upo wazi au unaongea na chakula mdomoni, kubeua/Cheua kwa sauti, kuchokonoa meno wakati watu wengine wanakula.-Namna anavyokuandaa na kufanya mapenzi hupendezwi, hupendi weka wazi ili ajue wapi pa KUREKEBISHA....tulishaambizana hili Mwaka 2007!



-Uvaaji, Vazi au mavazi humfanya Mwanamke ajisikie "safi"/mwenye furaha, anavutia au bado Kijana...usipokuwa muangalifu hapa unaweza kuitwa (bully)!


-Unywaji wa pombe, Pombe sio nzuri kwa afya yako kimwili (kigono) na kiakili, ni vema ku gadually punguza intake yako kwa wiki, na kama ni mwanamke na hutaki kuwa na kitambi, basi wacha kabisa.


-Ulalaji wake, wavuta shuka/Duvert Mpo!!! -Marafiki, "umekuja kabla ya marafiki zangu hivyo siwezi kuwaacha kwa ajili yako"...."Kama marafiki zangu huwapendi basi hatuwezi kuwa pamoja"...."Marafiki zangu kwanza, mengine (including mpenzi/Mke/Mume) baadae"...."Mpenzi huja na kuondoka lakini marafiki are for life" NIENDELEEE?!!!


Hizo ni sentensi ambazo tumezoea kuzisikia, mtu anafanya maamuzi ya maisha yake na familia yake(mke/mume) based on what a rafiki kashauri.


**Kumbuka kuna tofauti kati ya Watu unaofahamiana nao na Marafiki, huwezi kuwa na Marafiki 3 na wote wakakupenda the same. Kati yao lazima kuna adui.


Heri ya Mwaka Mpya!

Mapendo tele kwako...

Comments

Anonymous said…
Afadhali umerudi. Tulikumiss sana.
Anonymous said…
Ubarikiwe,unatukumbusha mengi saana na ya muhimu.