Aisee! Nimerudi, Nilikuwa Busy making babies....

Haa! Asikuambie mtu....ukitaka kujua utamu wa ku-make babies panga. Yaani wewe na mwenza wako mnajua kabisa bao litakalopatikana  leo linaenda tengeneza Mtoto. Basi ile "thought" ya  "vimelea" vinaenda kuungana na Yai na kutengeneza Mwanadamu inakuongezea amani, utulivu, Mahaba na mapenzi.

Nadhani ni tofauti na ile ya kushitukizia, kwamba mnafanya tu kila siku bila Kinga....alafu hujui kama mimba imetunga au la!...well ningejaribu hiyo lakini nadhani tumemaliza KUZAA*.


Anyway, Asanteni wote kwa Ushirikiano, mmekuwa mkitembelea na kunitumia maswali, maoni na salamu bila kuchoka. Sikutegemea kuendelea kupata watembeleaji kati ya 2,000-7,000 kwa siku....ukizingatia Blog haikuwa "active". Hakika najua ikiwa "active" nitarudi kwenye 100,000+. Mungu awabariki sana kwa Upendo na Ushirikiano wenu kwangu.


Kuwa mama/mzazi ni jambo jema na baraka lakini pia ni kazi ngumu sana na inachukua muda wako mwingi (vingine vinakuwa havina maana isipokuwa mtoto/watoto). Natambua wengi mnalijua hilo lakini mimi ndio kwanza najifunza au niseme napata uzoefu mpya.


Pamoja na kuwa ni busy mam-astic(hehehehe) kwa wanangu, nitajitahidi sana sana kuwaletea mambo/uzoefu mpya wa kimapenzi, mahusiano na ngono(kama ilivyokuwa awali) sitotumbukizia masuala ya watoto.


Kuwa mzazi au kuwa na watoto ni Baraka ya Ndoa/Matunda ya uhusiano, haipaswi kutufanya tusahau kuwa sisi ni Wapenzi, hivyo basi nitaendelea kuwa nawe sambamba tukielimishana, kumbushana, ambizana na kuelekezana ili sote tufurahi katika Ulimwengu huu Mtamu.

Nasikitika tu kuwa sitoweza kujibu Maswali ya nyuma, nitajitahidi kujibu yaliyoingia kuanzia wiki iliyopita. Samahni kwa usumbufu.

Endelea  kuwa nami na asante kwa Ushirikiano.

Mapendo tele kwako...

Comments

Anonymous said…
Waoo yani nimeingia kwenye hii blog yako wakati haupo active lakini kila siku nimekuwa nasoma makala zako za nyuma na nimemshauri mpz wangu asome pia
Anonymous said…
karibu
Anonymous said…
Wala usijali.Ninaamini upo kwa ajili yetu!!.Ila we ni mkali aiseeeee!!!.Welcome
Anonymous said…
Nimejifunza mengi sana, na nilishauliwa na mpenzi wangu lakini mimi sasa ndo nimekuwa mtaja tarehe za makala "mumy pitia makala ya tarehe fula" coz tupo mbali kidogo ila chuo kikifugwaga nakaa mkoani kwao wiki nzima ndo narudi home... Chezea mapenzi wewe.. Asante dada dinah